Eliud Kipchoge ateuliwa kuwania tuzo la mwanaspoti bora duniani(2019 Laureus World Sportsman of the Year)

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,923
13,344
7018838-0-image-m-6_1543967935177.jpg
DxIooM_X0AUSQ7Y.jpg
https://www.capitalfm.co.ke/sports/2019/01/18/kipchoge-to-battle-mbappe-lebron-for-award/ Baada ya kushinda tuzo la IAAF, la mwanariadha bora duniani hivi majuzi. Mkenya mwenzetu Eliud Kipchoge ameteuliwa tena kuwania tuzo lingine, la mwanaspoti bora duniani, 2019 Laureus World Sportsman of the Year. Ameteuliwa pamoja na wanaspoti wengine mashuhuri, kama Lebron James wa NBA(U.S), Lewis Hamilton wa Formula1(U.K), Novak Djokovic wa tennis(Croatia), FIFA Best Young Player Kylian Mbappe(Ufaransa) na mshindi wa World Cup Golden Ball Luka Modric(Croatia). Hongera zake kwa kuiwakilisha Kenya vilivyo kwenye ulingo wa spoti duniani. Bendera ya Kenya na iendelee kupepea kote kote. Wakenya tujivunie, kwenye michezo Afrika bila kutaja jina la Kenya inabaki tu kuwa hadithi za uongo njoo, utam kolea.
 
Hongera kwake namuombea atuwakilishe vyema Africa na east africa.. Je, kuna link yeyote ya kupiga kura
 
Hongera kwake namuombea atuwakilishe vyema Africa na east africa.. Je, kuna link yeyote ya kupiga kura
Uteuzi wa watakaowania ushindi wa tuzo tofauti za Laureus huwa unafanya na 'Nominations panel' ya wanaohusika kwenye michezo kwa njia moja ama nyingine kutoka nchi mia kote duniani. Kisha washindi huwa wanachaguliwa na 'delegates' kutoka Laureus World Sports Academy ambao wengi wao ni wanaspoti wa zamani kutoka sehemu tofauti duniani. Mashabiki wa michezo huwa wanapiga kura ya kuchagua Best Sporting Moment of the Year.
 
Big up eliud.... lazima atashinda. His record is extra ordinary... berlin marathon 2018 at 2.01.39 is super amazing... despite this world record the guy is still very humble and hardworking. He truly deserves...
Wabongolala hapa ndo wanaposhindwa..kijana wao moja alphonce simbu alienda NYC marathon akashindwa katikati.... very dissapointing.
 
Big up eliud.... lazima atashinda. His record is extra ordinary... berlin marathon 2018 at 2.01.39 is super amazing... despite this world record the guy is still very humble and hardworking. He truly deserves...
Wabongolala hapa ndo wanaposhindwa..kijana wao moja alphonce simbu alienda NYC marathon akashindwa katikati.... very dissapointing.
Humble guy indeed, reminds me of David Rudisha. Jina lake linatajwa kwenye sentensi moja na wanaspoti ambao wamebobea kwenye nyanja zao, sio mchezo! Huyo Simbu uliyemtaja niliona mazingara duni anayoishi na kufanyia mazoezi jombaa hadi inatia huruma. Jamaa hapewi support, isipokuwa kumtaja taja tu.
 
hongera kwake.
Am waiting to see how bongolalas will turn this thread up-side down into a SGR , kibera , hunger tag war
Jombaa utangoja sana, hapa hutawaona wakileta kiherehere chao. Hawa watani wetu huwa wana allergy ya michezo yote, isipokuwa bedminton, na domo domo.
 
Baada ya kuteuliwa kwa tuzo la Laureus World Sportsman of the year Award pamoja na wanaspoti wengine wanao ongoza kwenye nyaja zao duniani, na kufika hadi fainali. Mshindi wa tuzo la IAAF, la mwanariadha bora duniani, mkenya Eliud Kipchoge amekuwa mtu wa nne duniani na wa kwanza bara la Afrika kukabidhiwa tuzo la Laureus Academy's Exceptional Achievement Award, kwa juhudi zake kwenye riadha. Hongera zake. Kenya hoyeee! https://www.nation.co.ke/sports/ath...ievement-award/1100-4988446-jic6w0/index.html
 
Back
Top Bottom