Elimu yetu itatufikisha wapi na lini?

More problems

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
432
257
Elimu ni maarifa, mila na desturi zinazopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Utoaji wa elimu ni lazima uzingatie mahitaji na mazingira yanayotawala jamii inayohusika.
Utoaji wa elimu usipozingatia mila na destur, mahitaji pamoja na mazingira ya jamii basi haitoweza kufikia lengo LA ukombozi wala kumpa uwezo mwanadamu kuijenga na kuyamudu maisha.

Niamini kuwa wazazi wanatupeleka shule wakiamini wanatujengea uwezo wa kukabiliana na mazingira (watu na vitu) katika maisha.
Na kila mzazi atafurahi iwapo mwanae baada ya shule ataweza kuyamudu maisha ikiwa ni pamoja na kuweza kujitegemea katika nyanja zote za maisha.

Naandika habari hii nikiwa nimesukumwa na suala la elimu ya msingi katika nchi yangu ya Tanzania. Hasa changamoto ambazo zinanifanya niione elimu hii hauna msaada na imewekwa mazingira yasiyo sahihi.

Elimu ya msingi inampa mtu mwanga wa elimu na taaluma mbalimbali mbeleni na ni lazima kila mwananchi aipate. Hata kama asipoweza kuendelea na masomo ya juu zaidi lazima awe amepata mbinu za kukabiliana na changamoto za maisha.

Nasikitika kwamba nikiaangalia namna mfumo wa utoaji elimu ya msingi umelenga kumwezesha mwanafunzi kujua kusoma na kuandika badala ya kumjengea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Na ni bahati mbaya kwamba elimu yetu ya msingi imerefushwa bila sababu yoyote ya msingi ya kumkomboa mwanachi.

Nijikite kwenye mfumo wa utoaji elimu ya msingi katika nchi yangu.
Narejea kwenye wimbo wa mwanahiphop BONTA unaoitwa ZERO. Moja ya mashairi yake anasema,"tatizo sio madawati kama wasemavyo wadodoma tatizo ni mfumo mbovu kama TFF".

Nchini kwetu wabunge wamekazana na madawati na majengo tu bila kujadili namna elimu inavyotolewa na mahitaji ya jamii.
Mbaya zaidi wale watunga sera wanafuata matakwa ya wanasiasa na kuweka ujuzi na uahlisia wa mambo pembeni.
Lazima tukumbuke kuwa wanasiasa wanatatua matitizo yao na wanataka wapate wao hivyo wanawekeza kwenye vitu vinavyoonekana kama madawati na majengo ili kwenye kampeni spate cha kusema.

Tatizo letu kubwa hasa katika elimu ya msingi ni walimu na mahusiano kati ya walimu na wanafunzi.
Walimu wanaotoa elimu ya msingi hawana weledi na kazi hiyo.
Walimu hawa hawana uwezo wa kufundisha mtoto akaelewa kwani wao wamekariri kutoka vitabuni na hawajui inakuwaje mpaka kile wanachosema kipatikane.
Picha ya chini inaonesha barua iliyoandikwa na mwalimu kama swali katika mtihani wa darasa la sita
IMG_20170517_081829.jpg


Ni mfano tu mmoja mwalimu hajui na hawezi kuandika barua mwanafunzi anayemfundisha atakuwaje?

Uhusiano kati ya serikali wazazi, walimu na wanafunzi. Hakuna mahusiano yaliyo mazuri kati ya makundi haya. Kujifunza kunaenda sambamba na nidhamu. Wanafunzi wengi ni watovu wa nidhamu na walimu wamewaacha kwa kuwa wazazi nao wapo upande wa kuwatetea watoto wao.
Serikali pia haimthamini mwalimu na ndio mfanyakazi anayedharaulika hivyo walimu nao wanahangaika kutafuta heshima mtaani kwa kusaka hela.

Ikumbukwe wanafunzi wengi katika elimu ya msingi hawajitambui hivyo wanahitaji kusukumwa kwa nguvu sana ili wafanye kilichowapeleka shule vinginevyo watakuwa wanashangilia tu siku zinakwenda mda unapotea. Hasara kwao

Namalizia na jambo linalonipa ukakasi la kurefusha mda wa elimu msingi.
Mpaka sasa sijaona sababu ya kuongeza mda wa elimu ya msingi kwani zamani (1960 -1990) walioishia darasa la nne na la saba wana uwezo mkubwa wa kuzikabili changamoto za maisha kuliko wanaomaliza kidato cha nne sasa.

Ni vema serikali ingepunguza mda wa elimu ya msingi na kuifanya miaka 6/7 na kutengeneza mtaala utakaoendana na mazingira bila kusahau mahitaji ya jamii. Kwa kufanya hivi itasaidia kutopoteza mda wa wanafunzi.
Si zaidi ya 20% ya wahitimu wa elimu ya msingi wanaendelea na elimu ya kidato cha 5&6.
Hapo unaona kuwa zaidi ya 50% wanarudi nyumbani wakiwa watupu kabisa zaidi ya kujua kusoma na kuandika.
30% ya wanafunzi hao angalau wanpata kitu kiasi kichwani mwao.
Hili linachangia kuwalemaza kufanya shuguli na kujiingiza katika makundi mabaya.

Nawasilisha kwenu wakuu mawazo yangu mchangie kuhusu elimu yetu ya msingi. Ahsante.

Na, More Problems
 
Back
Top Bottom