Inategemea na unapenda kuwa nani maishani. Ziko fani ambazo tayari zimekwisha wekewa vigezo tayari hivyo inakubidi uufuate utaratibu na utafute kwa kusoma sifa wanazozitaka. Fani hizo ni kama uhasibu.uhandisi.ugavi na manunuzi.nk
Ziko fani ambazo bado unaweza ingia na ukapata kazi ndani ya muda mfupi. Fani hizo ni kama hotel management.ufundi ngazi ya kati.kilimo. nk.
Hotel management mara nyingi ukianza na cheti haichukui muda utakuwa na diploma ndani ya muda ambao hata form 4 ungekuwa hujafika.
VETA nayo inategemea uelewa wako na utayari wa kujiajiri.
Vyote ni pumzi yako.mahali ulipo kama fursa zipo na uwezo wa kugharamia.
Dunia hii ina nafasi kwa kila mtu na sio kama wengi wanavyofikiri ni lazma uwe na degree !!