Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Miaka ile ya 1960's na 70's pale chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kulikuwa na Jarida maarufu lililoitwa CHECHE. Jarida hili lilikuwa na slogan yake ya "JIFUNZE KUPAMBANA,PAMBANA KUJIFUNZA".
Miaka hiyo akina Profesa Shivji, Profesa Chachage S. Chachage, Prfofesa Mwesiga Baregu, Jeneral Ulimwengu etc wakiwa wanafunzi wa "undergraduate".. Jarfida la CHECHE lilikuwa linaandika mijadala mikali sana.
Jarida hili lilikuwa na makala kali zenye kujenga hoja kinzani juu ya falsafa na sera za nchi. Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam walikuwa wanaandika makala zenye kuchambua sera za nchi na kuziangalia kama zinaweza kweli kufanikisha ujenzi wa nchi ya ujamaa na kujitegemea.
Ukumbi wa Nkrumah ulikuwa hauishi mijadala mikali juu ya mwelekeo wa nchi. Mara nyingi Mwalimu Nyerere alikuwa anakwenda Nkrumah kusikiliza mijadala na hata kutoa mihadhara na kujibu hoja juu ya falsafa na sera za nchi ambazo serikali yake ilikuwa inaziamini.
Mwaka mmoja Mwalimu alialikwa Nkrumah, katika kujibu hoja za wasomi hao akijua kabisa walikuwa wanapigia chepeo falsafa za Karl Max. Nyerere aliwaambia "kama Karl Max angezaliwa Sumbawanga angeandika azimio la Arusha."
Miaka hiyo mwalimu Nyerere alijenga tabia na utamduni wa kuhakikisha kila kiongozi mkuu wa nchi anayefanya ziara nchini, alipewa fursa ya kwenda kutoa mhadhara chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mwalimu aliamini kuwa CHUO KIKUU NDIYO SEHEMU PEKEE AMBAPO MUSTAKABARI WA NCHI UNAJENGWA. NDIYO SEHEMU PEKEE AMBAYO MAWAZO MAPYA HUZALIWA. CHUO KIKUU NI SEHEMU YA MIJADALA.
Lakini kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwa viongozi wa sasa. Si hapa Tanzania bali hata nchi nyingine barani Afrika. Viongozi wa serikali wapo mbali na vyuo vikuu. Hawaendi tena kutetea sera zao, hawaendi tena kushiriki mijadala ya wanafunzi. Vyuo vikuu vingi barani Afrika sasa siyo visima vya mijadala kama ilivyuokua zamani.
Msingi wa ujenzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ilikuwa ni kuzalisha jamii ya vijana wadadisi, wanaohoji mambo kwa tafiti na takwimu, wanaotoa mwelekeo wa nchi bila woga, wasio ndumilakuwili.
Huu lazima ubaki kuwa msingi mkuu wa vyuo vikuu vingine vyote vilivyoanzishwa au vinavyotegemewa kuanzishwa. Viongozi wetu wajenge tabia ya kwenda vyuo vikuu,wakaongee na vijana, wakawasikilize, wapeleke sera za maendeleo za nchi zikachambuliwe huko.
Naanza kuona dalili za vyo vikuu vingi Tanzania kugubikwa na matamasha ya muziki na kujenga tabaka la wasomi wanaopenda starehe, waoga na wasiopenda kudadisi. Leo ukitembelea vyuo vikuu vingi utakutana na matangazo ya matamasha ya wasanii, sherehe mbalimbali, lakini sio mijadala kuhusu mustakabali wa nchi.
Nitafurahi sana kama Raisi Magufuli atafufua utaratibu ule wa Nyerere wa kufanya vyuo vikuu kuwa vitovu vya mijadala yenye tija kwa taifa. Aweke utaratibu wa kwenda vyuo vikuu na kuzungumza na wasomi na kuwaeleza ni aina gani ya Tanzania anayotaka kuijenga.
Pia awape nafasi ya kuwasikiliza wanasema nini kuhusu sera za nchi yetu, kama zinaweza kutimiza azma ya kuijenga Tanzania yenye uchumi unaojitegemea. Kama sera zetu zimechoka, awape fursa wasomi hao kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kuifanya Tanzania ifike kule tunakotaka.!
dotto Bulendu