Kumekuwa na malalamiko sana kwa watu wengi katika kipindi hiki kuhusu ulipaji wa kodi, hasa katika matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD katika ulipaji wa kodi. Binafsi sina uelewa kamili kuhusu haya mambo.
Mfano katika matumizi ya hizo mashine za EFD, ni vigezo gani vinatumika mpaka mfanyabiashara atakiwe kutumia hiyo mashine, je ni kiwango cha mtaji? kama ni kiwango cha mtaji basi ni sh. ngapi? je ni aina ya biashara? Je ni mahali biashara inapofanyika? Au kipi?
Naomba wajuzi wa haya mambo mtumwagie somo hapa hasa katika masharti / vigezo vya kutakiwa kutumia hizo mashine, na kama kuna mashine zingine pia mtuambie. Mimi sijui kwa kweli.
Haingalii kiwango cha mataji bali ni mauzo yoyote yale lazima utumie EFD, sema zipo aina tofauti si kwamba zote zina fanana. Kuna za wale waliko kwenye mfumo wa kukusanya VAT na kuna za kawaida.
Kama ni mgahawa mfano unakuwa na EFD ila inakuwa haicollect VAT bali mauzo pekee ya siku.