Mkuu unaweza kutudadavulia tofauti ya CE, CS na IT tuelewekipi ni kipi hasa vijana wanakutaarifu kwamba wanataka kusoma "computer" bila hata kujua kunatofauti gani katika program hizo kuanzia level ya certificate, diploma hadi degree.
Ili mtu aelewe vizuri inabidi uigawanye computer katika levels
Lets assume level zipo 4
1.Level ya hardware
2.Level ya chini ya software(level inayodeal na jinsi gani computer inaenda kufanya kazi katika level hii zaidi kuna algorithms za jinsi hardware inavyotakiwa kufanya kazi)
Mfano kama unatumia android smartphone...android OS ina operate katika level ya chini ya software
3.Level ya kati ya software(level ambayo software inapitia kuhakikiwa kabla ya kwenda kweny level ya juu)
Mfano Kwa android DVM ndio hutumika
4.Level ya juu ya software (level ambayo mtumiaji wa mwisho anaiona mfano application ya jamiiforum ni level ya juu)
Computer engineer ana deal na designing na maintenance katika level ya hardware
computer engineer anasoma module za engineering nyengine kama electronics na electrical engineering ili kufanikisha kazi yake kwa upande wa software anadokoa kidoko software engineering ambalo ni tawi la computer science
Computer scientist anadeal na theoretical part ya jinsi gani software itafanya kazi katika level zote hizo japo anaweza specialize katika level moja
Mfano computer scientist wa level ya chini ya software atadeal na machine learning na vitu kama AI
Wa level ya juu atadeal na vitu kama application software programming, database,computer networks,computer system,computer security
IT anadeal na utumiaji wa level ya juu ya software katika matumizi mbalimbali mfano biashara
Lakini kwa vyuo vingi mtu wa Computer engieering anasoma pia module za IT
Computer science anasoma pia module za IT na chuo kama MIT anasoma pia electrical engineering