Elimu kubwa ni nini?.

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
5,186
Reaction score
5,455
Kwa sasa watumishi wa umma wenye elimu ya chini wameonekana kudharauliwa mno mahala pa kazi huku mafanikio ya aina yoyote au kudorora kwa kampuni au shirika kunategemea hawa watu wa chini ambao wengi wao ni wa stashahada, cheti na wengine hata cheti hana bali semina elekezi tu.
Kila mtu ana faida yake ktk kazi. Kila hatua ktk kujifunza ina umuhimu wake na inahitaji watu maalumu kwa hatua hiyo.
Leo asilimia kubwa tumesoma shule ambazo walimu waliotufundisha hawakufika elimu ya sekondari. Hao ndiyo waliotuwezesha kufaulu shule za vipaji na kwingineko.
Ni ajabu kuwanyanyapaa hawa walimu. Wamelitoa taifa hili mbali.
Vivyo hivyo ktk idara nyingine hali iko hivyo hivyo. Serikali iache kuwanyanyapaa watumishi wa umma kisa elimu yao kwani wakati inawaajiri haikujua kuwa wana elimu ya cheti tu au stashahada!?.
Kuwanyanyasa watumishi hawa ni sawa na mtu anayeenda kuitupa kondomu jalalani baada ya kumsaidia ktk shida yake.
Wapo maprofesa na madaktari wengi nchi hii lakini msingi wao wa elimu ulijengwa na hawa wa chini ambao leo serikali inawanyanyapa pasipo kuwajengea misingi mizuri ktk kuongeza maarifa.
Serikali inawahamasisha watumishi kujiendeleza huku ikijua haiwezekani kutokana na hali ngumu ya miundombinu ya watumishi hao sehemu za kazi na uhalisia wa vyuo umbali wake.
Natoa rai kwa serikali kuwatambua watumishi wote wa umma na michango yao kwa taifa hili siyo kuwanyanyapaa kila mara kwa figisu za uhakiki usio tija wa elimu huku stahili zao zikibakia kwenye matamko.
Kila mtumishi ni mhimu kwa mahali alipo hivyo aheshimiwe na kuthaminiwa kwa mchango wake badala ya kudhihakiwa kama alivyowahi kuwadhihaki watumishi wa umma aliyekuwa mkuu wa wilaya ya mbeya jiji Dr. Sigala ambaye sasa ni mbunge huko makete.
Huwezi kufanikiwa bila kumtegemea mwingine kwa namna yoyote iwe kisiasa, kiuchumi, kidini,kijamii ama kitamaduni.
Hata wewe unayejiona tajiri umepata utajiri huo kwa kunyonya wengine na kama unabisha nenda kaishi kisiwa cha pekee yako miaka kumi uwe tajiri tukuone.
Tuheshimiane hakuna elimu kubwa bali kuna maarifa makubwa hayo ndiyo yakitumika vyema mtu unajua kusoma na kuandika, unajua kurusha ndege, unajua kupasua kutibu watu na mengineyo.
Nawatakia tafakuri njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…