Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Zaidi ya wanafunzi 5000 walioandikishwa darasa la kwanza katika shule za msingi Ludete, Lutozo na Nywawilimilwa.
wilayani Geita wanalazimika kusomea chini ya miti kutokana na uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa kufuatia uandikishwaji kuwa mkubwa kutokana na Serikali kutangazaelimu bure.
Channel ten imetembelea shule za Lutozo kata ya Katolo na kata ya Ludete na shule ya msingi Nyawilimilwa kata ya Nyawilimilwa na kushuhudia ya wanafunzi wa darasa la kwanza walivyorundikana chini wakati wa masomo huku walimu wanaofundisha wakiwa hawana pa kukanyaga wakati wa kundika ubaoni.
Walimu hao na viomgozi wa shule hizo wameiambia Channel Ten kuwa tangu tangazo la elimu bure kutolewa wazazi wamegoma kuchangia kitu chochote na hapa wanaeleza.
Kwa upande wao,wanafunzi wa shule hizo wamepaza sauti kwa Serikali kuzitazama shule hizo zilizoko pembezoni mwa mji kwa jicho la huruma ambapo pia wakaeleza jinsi wanavyoweza kushindwa kutimiza ndoto zao.