FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 304
- 236
Dhana ya ‘Elimu Bure’ kwa kila mtoto wa Tanzania imeshindwa kuendana na uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ambapo wanafunzi wa shule za msingi Kasindaga na Mshanje wilayani Muleba katika Mkoa wa Kagera wako katika hali mbaya, FikraPevu inaripoti.
Uchunguzi unaonyesha kwamba, mazingira ya utoaji wa elimu bora katika shule hizo ni magumu kutokana na kukosekana kwa miundombinu, hususan ya madarasa, madawati pamoja na vyoo.
FikraPevu imebaini kwamba, katika Shule ya Msingi Kasindaga iliyoko Kata ya Kyebitembe, wanafunzi wanalazimika kujisaidia vichakani na kwenye vyoo vibovu, hali ambayo inahatarisha usalama wao wa afya na kudunisha taaluma.
FikraPevu ilishuhudia wanafunzi wakipanga foleni kwenye vyoo vya makuti, huku wengine wakikimbilia vichakani kujisaidia.
Hali hiyo ipo pia katika Shule ya Msingi Nshanje ambayo iko ndani ya Kata hiyo ya Kyebitembe, ambapo licha ya kwamba vyoo hivyo vimesilibwa kwa makuti, lakini pia mazingira ya ndani si salama kwa kuwa kuna magogo tu yaliyowekwa na sehemu kubwa ya mashimo ikiwa wazi, hali ambayo ni ya hatari zaidi.
Inaelezwa kuwa, usalama mdogo katika kutumia vyoo hivyo vinavyoweza kusababisha wanafunzi wakatumbukia, ndio unaowafanya wanafunzi wengine, hasa wa elimu ya awali ambao ni wadogo, wakimbilie vichakani kujisaidia.
Zaidi, soma hapa => Elimu Bure: Wanafunzi wajisaidia vichakani, wasomea chini ya miti Muleba