kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,734
Walimu wanne, wafundisha wanafunzi 500,
Shule za mjini, moja ina walimu zaidi ya 20WAKATI serikali ikisisitiza kauli ya elimu bure, wanafunzi wapatao 602wa shule ya Msingi Magamba, iliyopo Jimbo la Songwe, wilaya ya Chunya mkoani hapa wanalazimika kukaa chini. Kalulunga blog imebaini.
Hali hiyo imebainika wakati wa ziara ya mwanadishi wa habari hii,
inayoendelea mkoani Mbeya kuona utekelezaji wa kauli ya Rais JohnMagufuli kuhusu elimu bure
Shule hiyo ina wanafunzi 700, ambapo idadi ya madawati ni 98, ambayoyanakaliwa na wanafunzi wa darasa la saba na darasa la sita.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanafunzi wamebuni mbinu mpya yakukalia matofali huku baadhi yao wakilazimika kutoka na vigoda
majumbani mwa wazazi wao na kwenda navyo shuleni kwa ajili ya kukali kisha mchana hurudi navyo.
Ofisa mtendaji wa Kijiji hicho, Sabina Shitundu, alikiri kuwepo kwa
adha hiyo ambayo alisema ni changamoto kubwa kwasababu pia ili kutatua tatizo hilo inawawia vigumu kwa madai kwamba suala la kuchangia madawati limeingiwa na siasa.
“Ni kweli tuna upungufu mkubwa wa madawati kutokana na wingi wawanafunzi na wazazi tulipoitisha mkuytano wa kijiji ili wachangia angalau Shilingi 2500 kwa mwaka lakini waligoma” alisema Ofisa huyo.
Alipoulizwa nini hatima ya upatikanaji wa madawati hayo 602, alielezakwamba, kutokana na wananchi kugomea zoezi la kuchangia madawati katika shule hiyo, wamewataka wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, kuwa kila mzazi achangia kiasi cha Shilingi 20,000, ambazo wazazi wawili watalazimika kununua dawati moja lenye thamani ya Tsh.40,000.
Mbunge wa jimbo hilo, Philipo Mulugo, alipotafutwa kwa njia ya simu ili kutaka kufahamu kama anajua tatizo la wananchi wake, simu haikuweza kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya kiganjani hakuweza kujibu, ambapo taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya watu wake wa karibu zilisema alikuwa kwenye ziara na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, eneo la Saza Mine, ambako kuna mgogoro kati ya wananchi na wawekezaji (Makaburu).
Wakati huo huo, upungufu wa walimu katika baadhi ya shule wilayaniChunya limeendelea kuwa tatizo sugu, huku suala la upataji mimba kwa wanafunzi nalo likitajwa.
Katika shule ya Msingi Kasasya kata ya Mtanila, yenye wanafunzi zaidiya 500, ina walimu wanne tu, huku shule ya Msingi Kalangali yenye wanafunzi 300 nayo ina walimu wanne ambapo mmoja wapo ni mzee na anasumbiliwa na maradhi hiyo ikifika saa sita analazimika kuondoka shuleni, huku shule zilizopo mjini, shule moja ina walimu zaidi ya 20.
Wakati huo huo, kuna “majipu” yanaendelea kuchunguzwa kama yameiva, kuhusiana na malalamiko ya walimu kuhusu fedha za uhamisho na likizo ambazo baadhi inaonyesha kuwa zilifanyika malipo lakini wahusika hawajapata.
Afisa elimu wa mkoa wa Mbeya, Charles Mwakalila, ambaye kabla hajapata nafasi hiyo alikuwa afisa elimu wa wilaya hiyo, alipoendewa ofisini kwake kwa ajili ya mahojiano, alimfukuza Mwandishi wa habari ambapo alimwamuru Katibu wake Muhtasi amwelekeze Mwandishi kuenda katika chumba cha wasaidizi wake namba 12 wanaoshughulikia masuala ya uhamisho wa wanafunzi!