SoC03 Elimu bora inayoendana na wakati na mahitaji ya jamii ni kichocheo cha uwajibikaji na utawala bora

Stories of Change - 2023 Competition

Mtowo

New Member
Jul 22, 2023
1
0
UTANGULIZI.
Suala la Uwajibikaji na utawala bora limekuwa tatizo kubwa nchini Tanzania.viongozi wa serikali,watumishi wa umma, wafanyakazi na hata wananchi wote wanalalamikiwa.swali la kujiuliza hapa nini kimepelekea tatizo hili kuongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma?.majibu unayoweza kupata pamoja na mambo mengine ni aina ya mfumo wa elimu ambao upo umepelekea kuzalisha kizazi cha aina hii.tukirudi nyuma baada ya Uhuru historia inaonyesha tulikuwa na jamii ambayo ilikuwa na viongozi wanaowajibika na kufuata misingi ya utawala bora mfano mzuri Baba wa taifa mwl Julius.K.Nyerere, Edward Moringe Sokoine na wengine wengi ambao walipelekea kuwa na jamii au umma wenye mwamko wa kushirikiana na viongozi wao katika kukabiliana na mambo mbalimbali yaliyojitokeza wakati ule,hvyo kupelekea taifa lenye wazalendo wanaowajibika katika jamii.na hii kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na elimu ya wakati ule.

Elimu ya sasa inazalisha wasomi wenye ufaulu mkubwa wa kitaaluma lakini kiuhalisia hawana uwezo wa kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.elimu inayotolewa ni nadharia haiendani na uhalisia wa matatizo, mabadiliko na mahitaji yanayojitokeza kwenye jamii ilhali dunia inabadilika Kwa Kasi,mabadiliko katika teknolojia,hali ya hewa na athari zake,mifumo ya maisha n.k.ili kukabiliana na hali hii hatuna budi kujiuliza tunahitaji nini kama taifa?,nini kifanyike?,na Kwa njia gani ili tuendane na mahitaji ya mifumo katika kuchochea uwajibikaji na utawala bora ambao ni chachu ya maendeleo katika nchi.

Mambo ambayo yanaweza kufanyika katika sekta ya elimu ili kuchochea uwajibikaji na utawala bora katika nchi.

1: Kiundwe chombo huru na maalumu kitakachosimamia elimu; chombo hichi kihusishe watalamu na wadau kutoka sekta mbalimbali, ambacho wajibu wake iwe ni kusimamia, kuboresha na kubadilisha mfumo wa elimu uendane na mahitaji ya jamii. Kihusike kukusanya maoni kutoka wadau mbalimbali kuhusu namna gani bora ya kuboresha elimu. chombo hichi ni muhimu kuwa huru kuepusha migongano na maelekezo kutoka Kwa wanasiasa ambao pengine wanaangalia maslai yao, hii itachochea uwajibikaji na utawala bora Kwani kitazingatia mahitaji ya kisekta na kijamii Kwa maana ya kwamba watalamu na wadau katika chombo hichi wataboresha Kwa kuzingatia uhitaji na ufanisi kwani wao Wana ujuzi kwenye mambo mbalimbali ya kijami.

2: Elimu ya kiraia na uzalendo ifundishwe katika ngazi zote za elimu na iwe kigezo cha lazima Kwa mtumishi wa umma, viongozi wa serikali n.k; elimu hii iangazie mambo mbalimbali kama vile historia ya nchi yetu, wajibu wa kila raia, misingi ya utawala bora, Sheria, haki za kila raia na mambo mengine yahusio ustawi wa jamii. Hii itachochea uwajibikaji na utawala bora Kwani tutapa viongozi na watumishi wa umma ambao wanajuwa wajibu wao na pia umma wenye kujuwa na kutambuwa wajibu wao na haki zao na namna ya kuzidai.

3: Kuanzishwe somo la uongozi na maadili katika ngazi za msingi za elimu. Jamii inayowajibika na kufuata misingi ya utawala bora ni jamii yenye viongozi bora ambao wanajuwa misingi ya uongozi. Hivyo bhasi ili tuwe na viongozi waadilifu, na wenye uwezo pamoja na kufuata misingi ya utawala bora ni muhimu elimu ya uongozi na maadili ikatolewa katika ngazi za msingi Kwani itapelekea kuandaa viongozi wa aina hiyo, uongozi ufundishwe katika ngazi zote kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla

4: Kuanzishwa Kwa masomo mbadala kulingana na uwezo na mahitaji ya mwanafunzi.jambo hili litapelekea kuwa na watu wenye ujuzi na ufanisi katika sekta fulani Kwani itakuwa imezingatia uwezo na takwa la mwanafunzi hvyo kuepusha wasomi wasokuwa na uwezo na ufanisi katika kazi walizosomea kutokana na ukweli kwamba wengine wanasomea vitu ambavy hawana uwezo navyo na hii inatokana na mifumo iliyopo. Masomo hayo yazingatie mahitaji ya jamii na stadi nyingine za maisha.

HITIMISHO; Ni dhahiri kuwa mfumo bora wa elimu unaoendana na wakati na mahitaji ya jamii ni kichocheo cha uwajibikaji na utawala bora ambao ni msingi wa maendeleo katika jamii. Serikali pamoja na wadau wengine hawana budi kufanyia kazi maoni chanya na yenye tija katika kuboresha mfumo wa elimu uendane na mahitaji ya nchi yetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom