Electric fence

Electric fence

Mr Electric

Member
Joined
Apr 26, 2019
Posts
10
Reaction score
28
ELECTRIC FENCE
Hii ni fence ya umeme yenye kupiga shoti, pindi mtu yeyote atakapojaribu kukatiza fence kuingia au kutoka nje ya kampound kupitia either juu ya ukuta au mahali ilipofungwa fence.
King'ora pia kitalia kwa sauti kubwa endapo mtu atajaribu kukatiza, kukata au atakapopigwa short na mashinine za energizer.. Maahine ya Energizer ina zaidi ya 500V Dc
Kuna aina mbili za fence.

1.Top wall Electric fence( juu ya ukuta)
2.Free stand Electric fence(juu ya aridhi)

TOP WALL ELECTRIC FENCE hizi zinafungwa majumbani juu ya ukuta wa fensi.
FREE STAND ELECTRIC FENCE hizi mara nyingi zinafungwa mashambani,

Standard Electric fence (Top wall) inakuwa na line 8 minimum otherwise kuna sababu zingine.

Materials like Poles(nguzo) standard ni Aluminium poles kwasababu hazishiki kutu, na pia zinamuonekano mzuri, pia kuna aina nyingi za wire kama (Galvanized wire, Aluminium wire na Stanley steel wire)

Fundi mzuri lazima afunge Earth load zaidi ya moja, kuipa nguvu fence ya kupiga short na kulinda mashine.

Kwa wateja wangu wa DAR huwa tunawashauri kufunga Aluminium poles,(nguzo), Aluminium wire au Stannely steel wire kutokana na mazingira ya chunvi, faida zake ni kwamba;
1.Hazishiki kutu
2.Hazipati layer ya chunvi inayopunguza uwezo wa kupiga shoti
3.Zinakaa muda mrefu sana
4.Zina muonekano mzuri

Gharama kufunga fence zinategemea mambo yafuatayo
1. Ukubwa wa ukuta ( material yatatumika mengi au machachekulingana na ukubwa wa ukuta)
2.Shape ya fence je? Ukuta wako umenyooka au upo straight, au unakonakona au ngazi ngazi, ukuta ulionyooka materials yatatumika machache hivyo bei itakuwa chini ukilinganisha na ukuta wenye kona kona au ngazi.
Watu wengi wamekuwa wakitapeliwa na mafundi jua kali, kwa kufungiwa fence zisizo na ubora kwa vifaa visivyoendana na mazingira. Au ufungiwa vifaa used na kuaminishwa ni vipya kwasababu tu either tajiri haelewi lolote, tamaa za mafundi, tajiri amelazimisha, au mteja kutaka bei rahisi,
Madhara yake yapo hivi, unaweza amini kuwa fence inafanya kazi kumbe ilishakufa siku nyingi, fence inakufa baada ya miezi sita au chini ya hapo tangu ifungwe, mwizi anauwezo wa kupita kwenye hiyo fence bila kupigwa short.
Karibu nikufanyie kazi nzuri bora na ya uhakika kwa usalama wa nyumba na mali zako.. 0620320089
Screenshot_20190801-163119.jpeg
Screenshot_20190801-163041.jpeg
Screenshot_20190801-162948.jpeg
Screenshot_20190801-162915.jpeg
 
Oooh,its nice to know about electric fence, sorry hiyo shot inaweza kuua? ama just inampa mtu mshtuko tu?. Je ikiua si unapata kesi ya mauaji hata kama alikua mwizi,

Je si hatari Kwa mazingira ya home mfano ikitokea labda wire zimeloose somewhere,ikaleta maafa mfano moto? Najifunza kwako mkuu

Gharama zake Kwa top wall electric fence ni sh ???
 
Haiui unapigwa tu short kubwa ambayo hutaweza kuendelea ku attempt chochote. Pia king'ora kitalia kuashiria kuwa kuna jambo limetokea. Mashine ina vitu viwili fence status na fence condition ambavyo kazi yake ni kukagua fence kama ipo katika hali gan. Ikihisi tofauti king'ora kitalia then ww utakagua kuona nn cha tofauti kimetokea.. Hakuna madhara yoyote ya moto yanayoweza kusababishwa na fence hii.. Muhimu tu kuweka zile sign zinazoonyesha Danger HiGh voltage hii iamuonyesha yoyote kuwa huruhusiwi kugusa ni hatari. Pia mara nyingi wateja wangu huwasha fensi usiku wakati wa kulala then asubuhi wanazima.
 
Thank you for the good explanations Mr Electric, no doubt any more. . siku nikifanikiwa kuwa na mjengo ntakutafutaa. Kazi njemaa
 
Stanley steel wire....ndiyo wire gani huo? Au ulitaka kusema Stainless steel wire?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom