GE2010 Election Public Polls: Joke!!

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
18,021
Reaction score
24,972
Kila jioni baada ya kazi ngumu za kutafuta ugali huwa napitia blogu na magazeti yote ya Tanzania yanayopatikana kwenye mtandao na kusoma karibu makala zake zote. Kubwa iliyonifurahisha leo ni hii hapa ambayo niliona ni vizuri niigawane na wana JF ambao hawajaisoma, au walipitia taito tu bila kuisoma yote.

 
Na habari zimfikie Njaa Kaya pamoja na wajomba zake popote walipo.
 
Doh! Nimeipenda hii sana. Imekaa kiuchunguzi, kiudadisi, kisayansi. Ni mada chokozi kwa wale wote wanaotaka kudodosi maoni ya watu kuhusiana na hoja fulani. REDET na Synovate wametia aibu jamii ya wanataaluma na hata watafiti. Hata aina ya maswali waliyouliza yalikuwa hasi. Huyu Profesa emeritus ametoa kila ambacho kilipaswa. Kama katika kampeni, kubwa lenye kuleta mvuto kwa mgombea ni Ahadi, iweje REDET na mwenzie wasigusie kabisa swala hili katika mahojiano? Wangeuliza kama wanaohojiwa wanaridhia ahadi zilizowahi kutolewa. Leo hii JK anapita kila mahali akisema CCM imetekeleza ahadi zake 2005 kwa asilimia 90, Jamani nani asiyeona haya kwamba si kweli!? Na hapa hakuna mdahalo kwa hivyo kauli yake ndiyo mshiko. Mdadisi yeyote mtafiti angetaka kujua hawa wa kaya wana maoni gani kuhusiana na concept hii ya ahadi.

Natamani kuwatukana lakini ngoja niache tu, ila BURE KABISA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…