Tunamuomba Allah azikubali amali zetu, azikubali funga zetu, azikubali sala zetu, atuzidishie imani na mapenzi ya dini yetu, atusamehe makosa yetu tuyajuwayo na tusiyoyajuwa.
Tunamuomba Allah awape nusra waislam popote duniani, awape nusra waislam wadhaliliwao, wadhulimiwao na wateswao. awape wao ushindi na sisi kwa jumla.Ushindi utakaowatia watu katika dini yake makundi kwa makundi.
Tunamuomba Allah atuunganishe na sio tutengane, atupe mapenzi baina yetu na sio tuchukiane na atuepushe, atuepushe na unafiki na wanafiki pia.
Yaa Rabb tia kwenye nyoyo zetu imani iliyo ya kweli ifanane na vitendo vyetu na iyowane na fikra zetu.
Yaa Rabb twakuomba utuongoze katika njia iliyonyooka, njia ya wale uliyowaneemesha na sio ya wale uliyowaghadhibikia au ya waliyopotea.
Tunakuomba Yaa Rabb utujaaliye uwezo wa kufanya uliyotuamrisha na kuyawacha uliyotukataza, tujaaliye tuwe ni wenye kuamrishana mema na kukatazana mabaya.
Twakuomba Yaa Rabb uviongoe vizazi vyetu, uzipambe nyoyo zao kwa imani na namapenzi ya dini ya Kiislam, uwape ujuzi wa kupambanua baina ya haki na batil na uwaondoshee khofu dhidi ya maadui wa Uislam.
Yaa Allah wasemeh na warehemu wazazi wetu waliyo hai na waliyotushatutangulia.
Yaa Allah tukubalie dua zetu...AMIN
TUNAWATAKIA KILA LA KHERI
EID MUBAARAK