Hii ni hatua ya mafanikio kwa mazayuni wa kiyahudi. Kwa miaka mingi wamekua wakiogopa uwepo wa Hamas ambayo ndiyo kimbilio la ukombozi kwa wapalestina. Hamas ilizaliwa Misri tena ubavuni mwa Muslim Brotherhood(MB), uwepo wa MB madarakani ulimpa mashaka sana Israeli, na hata wakamtumia kibaraka Al-Sisi kufanya mapinduzi haramu kwa uoga kwamba MB wakiwa madarakani Hamas itapata nguvu.
Kibaraka Al-Sisi anafanya kazi yake vizuri kama anavyoagizwa na mabwana zake. Kwanza, alifunga mpaka wa Rafah kipindi cha vurugu za mwisho za Gaza(kitu ambacho ni kinyume na sheria za kimataifa), Pili ameendesha mauaji yasioyosemeka kwa wanachama wengi mno wa MB, Tatu anashirikiana kijeshi na mazayuni na mwisho zaidi ndio hili la kuharamisha vuguvugu pekee la kiislamu ambalo ndio tumaini la raia wa Palestina, hususani Gaza.
Mengi yataendelea kutokea, jamaa jamaa zetu wanafki wa magharibi wamekaa kimya na kuendelea kufanya kazi na serikali iliyoingia kwa njia ya mapinduzi haramu. VERY ABSURD...