JF
Leo ilikua siku kubwa sana kwa Mweshimiwa Edward, kutangaza nia. Kwa wale mnao mjua vizuri pamoja na rafiki zake tutakubaliana na jinzi pesa ilivyo na nguvu ya kuwatia upofu watu wasio weza hata kutafakari mbele kwa mita hata kumi.
nguvu kubwa iliyotumika kuandaa mkutano wa kutangaza nia inazihirisha hali halisi ya Mweshimiwa kuutaka uraisi kwa njia yeyote ile. Watanzani lazima mjue kuwa Ikulu si pango la wezi.
Kila rahia ana haki ya kutangaza nia ya kuwa kiongozi, kwangu mie ni mtihani mkubwa uliobaki kwa CCM kufanya maamuazi ambayo yatakua kipimo sahihi kujua kama chama ni cha mafisadi au cha wafanyakazi na masikini wakulima. Itashangaza sana endapo umakini wa chama utaamua bendera kufuata upepo kwa kuaangalia tu kukubalika kwa mtu bila kujali uadilifu na uwezo wa mgombea. Kwetu sisi tunahamu sana kusikia hatima ya mgombea wa CCM ili tuone kama mafisadi wameamuamua kumeza walio wengi wadilifu ndani ya chama chetu.
Ni lazima turuhusu bongo zetu zifanye kazi na wala tusifanye maamuzi kutokana na misukumo ya hisia au ya kutengenezewa mazingira ya kuaminisha umma kuwa fulani ndio chaguo bora.
Nawasilisha