Edward Lowassa: Ahadi ya 1. elimu, 2. elimu,3. elimu

Edward Lowassa: Ahadi ya 1. elimu, 2. elimu,3. elimu

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,302
Tunakumbuka wakati wa mchakato wa kura za maoni mgombea wa CHADEMA kabla hajahama kutoka CCM alisema kipaumbele chake cha kwanza hadi cha tatu ni elimu, pia alisema alifuatisha kutoka kwa aliyekua waziri wa uingereza kipindi fulani na akaifanikisha sana uingereza. Mimi ninachouliza ni kwamba matatizo ya elimu ni mengi hapa nchini kama vile...

1. Kukosekana kwa madarasa, nyumba za walimu pamoja na miundominu migine

2. Walimu wetu kuwa na uwezo mdogo ukizingatia ni wale watu waliopata madaraja ya chini ndio wanakua walimu

3. Walimu wetu kua na maslahi duni na kusababisha migomo ya mara kwa mara

4. Kukosekana kwa syllabus nzuri inayoendana na hali inavyobadilika kwa sasa

5. Kukosekana kwa maabara za kisasa na wataalamu wazuri katika masomo ya sayansi

6. Wanasayansi wetu hasa wahandisi na wakemia kutokua na masomo ya vitendo ya kutosha ili kutuwezesha kuwa na teknolojia ya kisasa alafu ndio tuwe na viwanda vyetu

7. Ukosefu wa utaalamu kwa wahitimu wetu wa vyuo kutokana na kulipua lipua kwa elimu yetu ya vyuo

8. Mengineyo mengiii...

Sasa huyu mzee wetu sijawahi kumsikia akiainisha matatizo gani yanayoikabili elimu yetu ili tusiendelee na ni jinsi gani atakavyoyatatua badala yake amekua akisisitiza ahadi nyingine za kusaidia machinga, bodaboda, mama ntilie ahadi ambazo haukati mzizi wa tatizo bali ni kupunguza tu majani yake.

Alitakiwa atuambie atafanyaje ili kuzuia vijana wengi kufanya bodaboda ndio kimbilio lao na umachinga kwa kutumia hii elimu
 
Tatizo lako huna elimu. Ndo maana lowasa atahakikisha unapata elimu ya kujua na kutambua anaposema elimu anamaanisha nini.
Usiwe kilaza.
 
We jamaa natamani ungekuwa na elimu kama hata ya kwangu tu..ungejielewa sana
 
Mbaya hata video kuhusu kampeni zake zimekuwa adimu kwenye mitandao wakati ana team kibao za kumrusha.!
 
tatizo lako huna elimu. Ndo maana lowasa atahakikisha unapata elimu ya kujua na kutambua anaposema elimu anamaanisha nini.
Usiwe kilaza.
mimi nina elimu kubwa tu lakini sio bora na nataka iboreshwe ndio maana nahoji, mambo ya vyama pembeni
 
mimi nina elimu kubwa tu lakini sio bora na nataka iboreshwe ndio maana nahoji, mambo ya vyama pembeni

Ndo unatakiwa ujue elimu ni package nzima, kuanzia mdawati, kujenga shule, nyumba za walimu, kugawa vitabu, mabara bora, kulisha watotto shuleni n.k.
 
Acheni ujinga tanzania kuna elimu gani?
1.hao wasomi kukremisha..na kukimbilia kuwa maofisini badala ya kwenda field?
2.mbona hao wasomi mlikimbia jumuia ya africa mashariki?
3.jiungeni wa wasomi wengine basi muone pamoja na degree zenu za kupewa kama hamkufananishwa na mahouse boys na girls..come on!
Nb.
Elimu ovyo..bongo haina soko...toka nayo ndio utaelewa kuwa lowasa yuko sawa..
 
Mkuu hata kuishi vizuri na Mumeo, unahitaji elimu.

Elimu ni suala mtambuka. Ni msingi wa kila jambo. Ndio maana wasiokuwa "WAPUMBAVU" na "MALOFA" wanawapeleka watoto wao Ulaya kwa kujua elimu ya Tanzania ni ya kukaririshana tu basi.
 
Ndo unatakiwa ujue elimu ni package nzima, kuanzia mdawati, kujenga shule, nyumba za walimu, kugawa vitabu, mabara bora, kulisha watotto shuleni n.k.
yap ni kweli lakini mbona sasa yeye hazungumzii ni vipi ataiboresha sasa? anataka tumwamini tu? itakua ajabu sana huzungumzii vipaumbele vyako vitatu unazungumzia vingine alafu unataka tukuchague
 
Mkuu hata kuishi vizuri na Mumeo, unahitaji elimu.

Elimu ni suala mtambuka. Ni msingi wa kila jambo. Ndio maana wasiokuwa "WAPUMBAVU" na "MALOFA" wanawapeleka watoto wao Ulaya kwa kujua elimu ya Tanzania ni ya kukaririshana tu basi.
na yeye ataiboreshaje sasa? atuelezee bayana ili tumchague, sio kuzungumzia kila siku bodaboda, mama ntilie na machinga, hawa wangekua na elimu bora wasingekua wanafanya shughuli wanazofanya
 
Acheni ujinga tanzania kuna elimu gani?
1.hao wasomi kukremisha..na kukimbilia kuwa maofisini badala ya kwenda field?
2.mbona hao wasomi mlikimbia jumuia ya africa mashariki?
3.jiungeni wa wasomi wengine basi muone pamoja na degree zenu za kupewa kama hamkufananishwa na mahouse boys na girls..come on!
Nb.
Elimu ovyo..bongo haina soko...toka nayo ndio utaelewa kuwa lowasa yuko sawa..
kila mtu anajua elimu ya bongo inahitaji maboresho tatizo ni kwamba anayegombea wala hajawi kuzungumzia bayana ataiboreshaje
 
yap ni kweli lakini mbona sasa yeye hazungumzii ni vipi ataiboresha sasa? anataka tumwamini tu? itakua ajabu sana huzungumzii vipaumbele vyako vitatu unazungumzia vingine alafu unataka tukuchague

Unasikiliza mikutano yake yote mkuu?
 
Huwa nikisikia mtu anasema ili neno elimu nafadhaika kwakweli, najiuliza wale vijana wanashinda vijiweni na kwenye mikutano ya wanasiasa japokuwa wamesoma ni kweli hawana elimu?

Nakumbuka interview mbalimbali kama ile uhamiaji ambapo walijitokeza waombaji zaidi ya 10,0000

Naomba mnisaidie hii elimu anayozungumzia lowasa ni ipi na hatua gani atachukua kwa ambao mimi naaamini wamesoma lkn hawana ajira

Tafakari acha ushabiki wa kisiasa
 
na yeye ataiboreshaje sasa? atuelezee bayana ili tumchague, sio kuzungumzia kila siku bodaboda, mama ntilie na machinga, hawa wangekua na elimu bora wasingekua wanafanya shughuli wanazofanya

Kwanini usilaumu CCM yako uliyoichagua miaka yote nabado unataka kuichagua tena
 
Back
Top Bottom