Edo Kumwembe: Onyango mbuzi wa kafara, Bacca anachafua hali ya hewa

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
998
NAMNA maisha yanavyokwenda kasi. Ijumaa usiku wa manane dunia ilikuwa imemwangukia mlinzi wa kati wa kimataifa, Josh Onyango mara baada ya kumalizika kwa pambano kati ya Simba na Raja pale Casablanca.

Asubuhi tuliamka picha zake katika mitandao ya jamii na alikuwa akishambuliwa kwa kejeli na mashabiki wa pande zote mbili. Simba pamoja na watani wao Yanga. Kisa? Alihusika na mabao mawili ya Raja katika kichapo cha mabao 3-1 ambacho Simba walipokea Casablanca.

Ni kweli alihusika. Wengine walienda mbali kwa kudai kwamba muda wake umefika mwisho Simba na aondoke zake. Wengine wakadai aondolewe katika kikosi kinachoanza. Waliotoa kauli hii ya pili hawajui kwamba katika walinzi wanaokaa benchi hakuna anayemfikia Onyango.

Bao la kwanza hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya Onyango na kipa wake Aishi Manula. Labda angalizo kwake ni kwamba siku nyingine asimuamini kipa wake. Ahakikishe anautoa mpira nje au achukue uamuzi kwa kadri anavyoona.

Bao la pili ni kama ile penalti ambayo aliitoa Dar es salaam. Alibakia na Mwarabu mmoja akamzungusha kisha akaingia katika boksi na Onyango akajikuta anamchezea rafu kwa nyuma. Mara zote mbili hizi ungeweza kuwasifu maadui kwa utundu wao. Lakini zaidi ungelaumu watu wa safu ya ulinzi ya Simba pamoja na viungo kutocheza kwa karibu karibu.

Kama kuna mlinzi angekuwa anamsaidia Onyango kwa karibu (compactness) si ajabu asingeona umuhimu wa kumgusa mpinzani au kuendelea kusuguana naye katika mwili. Wenzetu katika mazingira yale, wakati Onyango anaachwa kwa ujanja na mpinzani tayari kungekuwa na mchezaji mwingine wa Simba amejitokeza kumsaidia Onyango na sasa kelele zimekuwa nyingi kuhusu Onyango.

Kitu ambacho siamini ni kwamba mchezaji anaweza kwisha ghafla. Mfano tu ni kwamba msimu uliopita Onyango alikuwa bora, halafu ghafla sasa hivi amekwisha. Kinachotokea kwa sasa ndicho ambacho kitammaliza kabisa Onyango.

Hizi shutuma ndizo ambazo zitamfanya aanze kutojiamini. Wenzetu huwa wanamnyanyua mchezaji kutoka hapa alipo ili arudishe ubora wake. Sisi huwa tunamzamisha zaidi kwa kuendelea kumshutumu kuwa “Ni mzee atupishe” na maneno mengine ya kejeli.

Kuna mambo mawili. Ama Simba iende sokoni na kumnunua beki mwingine ambaye atakuwa kama bahati nasibu tu. Anaweza kuja akafanya makosa mengi kuliko Onyango. Lakini jambo la pili wanaloweza kufanya ni kumtia moyo Onyango arudi katika kujiamini na ubora wake ili waokoe pesa na muda.

Kama Onyango akistaafu soka leo hauwezi kumkumbuka kwa makosa mawili matatu ambayo ameyafanya hapa karibuni. Utamkumbuka Onyango kama mlinzi bora wa kati aliyetoka kwao Kenya akiwa mchezaji bora wa Ligi ya Kenya kisha akahamishia makali yake Msimbazi.

Utamkumbuka kwa kuwa mlinzi shupavu ambaye wakati Simba ina walinzi watatu wa kigeni, Yeye, Pascal Wawa na Henock Inonga, yeye ilikuwa lazima acheze na mlinzi mmoja kati ya hao. Hauwezi kumkumbuka Onyango kwa kashfa.

Kwa sasa naona tunataka kumtoa mchezoni kama ilivyo kawaida yetu. Sio jambo jema sana. Mchezaji haishi ghafla. Huwa anaisha taratibu. Nasimama kumtetea mpaka pale atakapozidisha makosa tena na tena. Kwa sasa bado ana nafasi ya kutamba Simba. Kama tunadhani hafai basi tumpange Mohamed Ouattara. Mbona hachezi?

Wakati maisha yakiwa hivi kwa Onyango, siku moja baadaye Yanga wakacheza pale Lubumbashi. Maisha yanakwenda kasi kwa walinzi wa kati wa hizi timu kubwa mbili za Kariakoo. Na sasa tuna mlinzi wa kati anayeitwa Ibrahim Bacca. Anakipiga Yanga.

Juzi Bacca alianza katika pambano lake la pili kubwa la kimataifa ngazi ya klabu. Alianza katika pambano la marudiano dhidi ya Monastir ya Tunisia pale Uwanja wa Taifa. Akaenda Misri na timu ya taifa pambano dhidi ya Uganda akaanza. Akarudi Dar es Salaam pambano la marudiano dhidi ya Uganda akaanza.

Nafasi yake katika timu ya taifa huwa inachezwa na walinzi wawili wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job. Kama anapata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa dhidi ya walinzi hawa hawa, kwanini akose nafasi klabuni dhidi ya walinzi hawa hawa?

Tatizo limeanzia hapo. Katika pambano dhidi ya Uganda pale Ismailia na kisha Temeke, Job alipelekwa kulia kwa ajili ya kumpisha Bacca katikati. Na juzi pale Lubumbashi Job alipelekwa kulia kwa ajili ya kumpisha Bacca. Nasema alimpisha Bacca kwa sababu Mwamnyeto amerudisha nafasi yake kikosini.

Katika pambano la juzi, Djuma Shaabani alikaa nje kwa sababu labda Yanga walikuwa wanahofia asipate tena kadi ya njano na hivyo kulikosa pambano la kwanza la robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Swali ni kama Djuma akirudi. Job atarudishwa katika nafasi yake? Atarudishwa kwa gharama za Mwamnyeto au Bacca?

Ni mpaka lini Job anaweza kupangwa kulia kwa gharama za Djuma na rafiki yake, Shomari Kibwana kukaa nje? Binafsi sioni kama Job atakuwa anapangwa kama mlinzi wa kulia kwa muda mrefu. Kinachowaumiza kichwa Nasreddine Nabi pamoja na kocha wa timu ya taifa, Adel Amrouche ni ukweli kwamba Job ni mchezaji mzuri na hawataki akae nje.

Hata hivyo, naweza kumuona Djuma akirudi katika nafasi yake kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kushambulia. Ni hapo ndipo ambapo Nabi atalazimika kuchukua uamuzi mgumu. Atamuweka nje Job au atamuweka katika nafasi ya Mwamunyeto?

Sioni kama Bacca atakaa nje kutokana na ubora ambao anauonyesha hewani na miguuni. Nabi atalazimika kufanya uamuzi mgumu. Lakini zaidi kuimarika kwa Bacca huku pia Mwamnyeto akiwa amerejea na Job angali akiwa imara kunasababisha sasa Yannick Bangala arudi kaika nafasi yake anayoipenda kuitumikia. Nafasi ya kiungo.

Hili nalo litaleta vurugu katika eneo hili kwa sababu Yannick ataenda kuungana na Sure Boy, Khalid Aucho, Mudathir Yahaya, Gift Mauya na Aziz Ki kwa mbele yao. Kichwa kitakuwa kinamuuma Nabi namna ya kupanga kikosi.

Hata hivyo, kwa namna moja au nyingine hii ndio faida ya kuwa na wachezaji wengi bora katika kikosi kimoja. Si ajabu ndio maana Yanga wanafanya vizuri katika michuano mbalimbali ambayo wanashiriki kwa sasa. Wana ubora mwingi katika maeneo mengi.

Juzi walikuwa wakishinda pale Lubumbashi bila ya uwepo wa Djigui Diarra, Khalid Aucho, Aziz Ki, Djuma Shaaban, Bernard Morrison na Feisal Salum ambaye ameisusia timu. Kwenda Lubumbashi na kushinda pambano dhidi ya TP Mazembe ni jambo ambalo lisingefikirika miezi 24 iliyopita. Kocha Nabi ana machaguo mengi kikosini.

Mwananchi
 
NAMNA maisha yanavyokwenda kasi. Ijumaa usiku wa manane dunia ilikuwa imemwangukia mlinzi wa kati wa kimataifa, Josh Onyango mara baada ya kumalizika kwa pambano kati ya Simba na Raja pale Casablanca.
Asubuhi tuliamka picha zake katika mitandao ya jamii na alikuwa akishambuliwa kwa kejeli na mashabiki wa pande zote mbili. Simba pamoja na watani wao Yanga. Kisa? Alihusika na mabao mawili ya Raja katika kichapo cha mabao 3-1 ambacho Simba walipokea Casablanca.
Ni kweli alihusika. Wengine walienda mbali kwa kudai kwamba muda wake umefika mwisho Simba na aondoke zake. Wengine wakadai aondolewe katika kikosi kinachoanza. Waliotoa kauli hii ya pili hawajui kwamba katika walinzi wanaokaa benchi hakuna anayemfikia Onyango.
Bao la kwanza hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya Onyango na kipa wake Aishi Manula. Labda angalizo kwake ni kwamba siku nyingine asimuamini kipa wake. Ahakikishe anautoa mpira nje au achukue uamuzi kwa kadri anavyoona.
Bao la pili ni kama ile penalti ambayo aliitoa Dar es salaam. Alibakia na Mwarabu mmoja akamzungusha kisha akaingia katika boksi na Onyango akajikuta anamchezea rafu kwa nyuma. Mara zote mbili hizi ungeweza kuwasifu maadui kwa utundu wao. Lakini zaidi ungelaumu watu wa safu ya ulinzi ya Simba pamoja na viungo kutocheza kwa karibu karibu.
Kama kuna mlinzi angekuwa anamsaidia Onyango kwa karibu (compactness) si ajabu asingeona umuhimu wa kumgusa mpinzani au kuendelea kusuguana naye katika mwili. Wenzetu katika mazingira yale, wakati Onyango anaachwa kwa ujanja na mpinzani tayari kungekuwa na mchezaji mwingine wa Simba amejitokeza kumsaidia Onyango.Na sasa kelele zimekuwa nyingi kuhusu Onyango. Kitu ambacho siamini ni kwamba mchezaji anaweza kwisha ghafla. Mfano tu ni kwamba msimu uliopita Onyango alikuwa bora, halafu ghafla sasa hivi amekwisha. Kinachotokea kwa sasa ndicho ambacho kitammaliza kabisa Onyango.
Hizi shutuma ndizo ambazo zitamfanya aanze kutojiamini. Wenzetu huwa wanamnyanyua mchezaji kutoka hapa alipo ili arudishe ubora wake. Sisi huwa tunamzamisha zaidi kwa kuendelea kumshutumu kuwa “Ni mzee atupishe” na maneno mengine ya kejeli.
Kuna mambo mawili. Ama Simba iende sokoni na kumnunua beki mwingine ambaye atakuwa kama bahati nasibu tu. Anaweza kuja akafanya makosa mengi kuliko Onyango. Lakini jambo la pili wanaloweza kufanya ni kumtia moyo Onyango arudi katika kujiamini na ubora wake ili waokoe pesa na muda.
Kama Onyango akistaafu soka leo hauwezi kumkumbuka kwa makosa mawili matatu ambayo ameyafanya hapa karibuni. Utamkumbuka Onyango kama mlinzi bora wa kati aliyetoka kwao Kenya akiwa mchezaji bora wa Ligi ya Kenya kisha akahamishia makali yake Msimbazi.
Utamkumbuka kwa kuwa mlinzi shupavu ambaye wakati Simba ina walinzi watatu wa kigeni, Yeye, Pascal Wawa na Henock Inonga, yeye ilikuwa lazima acheze na mlinzi mmoja kati ya hao. Hauwezi kumkumbuka Onyango kwa kashfa.
Kwa sasa naona tunataka kumtoa mchezoni kama ilivyo kawaida yetu. Sio jambo jema sana. Mchezaji haishi ghafla. Huwa anaisha taratibu. Nasimama kumtetea mpaka pale atakapozidisha makosa tena na tena. Kwa sasa bado ana nafasi ya kutamba Simba. Kama tunadhani hafai basi tumpange Mohamed Ouattara. Mbona hachezi?
Wakati maisha yakiwa hivi kwa Onyango, siku moja baadaye Yanga wakacheza pale Lubumbashi. Maisha yanakwenda kasi kwa walinzi wa kati wa hizi timu kubwa mbili za Kariakoo. Na sasa tuna mlinzi wa kati anayeitwa Ibrahim Bacca. Anakipiga Yanga.
Juzi Bacca alianza katika pambano lake la pili kubwa la kimataifa ngazi ya klabu. Alianza katika pambano la marudiano dhidi ya Monastir ya Tunisia pale Uwanja wa Taifa. Akaenda Misri na timu ya taifa pambano dhidi ya Uganda akaanza. Akarudi Dar es Salaam pambano la marudiano dhidi ya Uganda akaanza.
Nafasi yake katika timu ya taifa huwa inachezwa na walinzi wawili wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job. Kama anapata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa dhidi ya walinzi hawa hawa, kwanini akose nafasi klabuni dhidi ya walinzi hawa hawa?
Tatizo limeanzia hapo. Katika pambano dhidi ya Uganda pale Ismailia na kisha Temeke, Job alipelekwa kulia kwa ajili ya kumpisha Bacca katikati. Na juzi pale Lubumbashi Job alipelekwa kulia kwa ajili ya kumpisha Bacca. Nasema alimpisha Bacca kwa sababu Mwamnyeto amerudisha nafasi yake kikosini.
Katika pambano la juzi, Djuma Shaabani alikaa nje kwa sababu labda Yanga walikuwa wanahofia asipate tena kadi ya njano na hivyo kulikosa pambano la kwanza la robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Swali ni kama Djuma akirudi. Job atarudishwa katika nafasi yake? Atarudishwa kwa gharama za Mwamnyeto au Bacca?
Ni mpaka lini Job anaweza kupangwa kulia kwa gharama za Djuma na rafiki yake, Shomari Kibwana kukaa nje? Binafsi sioni kama Job atakuwa anapangwa kama mlinzi wa kulia kwa muda mrefu. Kinachowaumiza kichwa Nasreddine Nabi pamoja na kocha wa timu ya taifa, Adel Amrouche ni ukweli kwamba Job ni mchezaji mzuri na hawataki akae nje.
Hata hivyo, naweza kumuona Djuma akirudi katika nafasi yake kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kushambulia. Ni hapo ndipo ambapo Nabi atalazimika kuchukua uamuzi mgumu. Atamuweka nje Job au atamuweka katika nafasi ya Mwamunyeto?
Sioni kama Bacca atakaa nje kutokana na ubora ambao anauonyesha hewani na miguuni. Nabi atalazimika kufanya uamuzi mgumu. Lakini zaidi kuimarika kwa Bacca huku pia Mwamnyeto akiwa amerejea na Job angali akiwa imara kunasababisha sasa Yannick Bangala arudi kaika nafasi yake anayoipenda kuitumikia. Nafasi ya kiungo.
Hili nalo litaleta vurugu katika eneo hili kwa sababu Yannick ataenda kuungana na Sure Boy, Khalid Aucho, Mudathir Yahaya, Gift Mauya na Aziz Ki kwa mbele yao. Kichwa kitakuwa kinamuuma Nabi namna ya kupanga kikosi.
Hata hivyo, kwa namna moja au nyingine hii ndio faida ya kuwa na wachezaji wengi bora katika kikosi kimoja. Si ajabu ndio maana Yanga wanafanya vizuri katika michuano mbalimbali ambayo wanashiriki kwa sasa. Wana ubora mwingi katika maeneo mengi.Juzi walikuwa wakishinda pale Lubumbashi bila ya uwepo wa Djigui Diarra, Khalid Aucho, Aziz Ki, Djuma Shaaban, Bernard Morrison na Feisal Salum ambaye ameisusia timu. Kwenda Lubumbashi na kushinda pambano dhidi ya TP Mazembe ni jambo ambalo lisingefikirika miezi 24 iliyopita. Kocha Nabi ana machaguo mengi kikosini.

MWANANCHI
Duh
 
gsm wamemwaga mpunga usajili umeanzaa kulipa, sisi simba mudi analialia tunampa hasara, ila usajili wa kubahatisha, tujifunze maana robo fainali ndio mwisho wetu, wakati yanga ana weza kufika fainali msimu huu
 
Sasa unalinganisha CAF CHAMPION LEAGUE na ligi ya malooser shirikisho
 
gsm wamemwaga mpunga usajili umeanzaa kulipa, sisi simba mudi analialia tunampa hasara, ila usajili wa kubahatisha, tujifunze maana robo fainali ndio mwisho wetu, wakati yanga ana weza kufika fainali msimu huu
Unalipa kwasababu mnakutana na timu dhaifu za kombe la loosers. Ingekuwa huku kwa vigogo wa soka la Afrika huo usajili wenu mngeuona hauna cha ajabu. Ukitaka kulijua hilo angalia mlipokutana tu na aly Hahaly ya sudani mlivyofuruhushwa kwenye haya mashindano ya CAFCL kwa aibu
 
mwaka jana mlishiriki kombe gani la kimataifa we KOLO?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom