Ebu tushauriane kwenye hili wanangu

Ebu tushauriane kwenye hili wanangu

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,309
Reaction score
7,857
Ni hivi wewe ni kijana upo kwenye umri wa 20's unaishi Dar wazazi wapo mikoani huko Kila mtu kivyake, Dar una miaka minne na huna mchongo wa maana (Namaanisha unaungaunga sana), Lakini bado una malengo ya kufika mahali fulani kwa mfano: Una mpango wa kumiliki Duka la bidhaa fulani ambazo kwa Sasa upo kama dalali kwenye Duka la watu.

Kama unavyojua maisha ya Dar yalivyo juu 5000 kwa siku Kutoboa kwenye kula tu lazima ujue kujibana haswa(Wanazengo wanajua Ile ya kuunganisha Break fast na Lunch) Yaani hauli kutwa mara tatu ni kutwa mara 2, 2500 mchana, 2500 usiku.

Katika harakati zako kuna Kipindi unabutua hata 30k kwa siku, ila siku nyingine unakosa hata 100 Yaani kiufupi bado sana ili utimize malengo yako maana hapo kati Kuna Kodi ya chumba, Umeme na makorokoro kibao Yani, Then Wazazi wako bado wapo na nguvu tu Mzee anacheza kwenye 40+ na Maza kwenye 30+....

Lakini simu zao nyingi za vizinga na ukisema huna Kila mmoja analalamika kivyake (namaanisha wazazi pia walishaseparate Baba kivyake na mama kivyake) So Kila mmoja akikuomba hela ukakuta huna ukimjibu kuwa huna analalamika au anakubali Ile kishingo upande, Ukicheki Elimu uliyokuwa nayo ni O-level Yaani kiufupi Ukizembea kidogo tu unarudi kimbiji..... Ila wazazi hawalioni Hilo wao wanaamini kwa kuwa upo Dar basi una hela sema unawabania tu.

Mtu Hadi unajishtukia kuwapigia Simu ya kuwajulia Hali wazazi kwa kuwa unajua kinachofuata ni kizinga, Basi siku mkiongea wanalalama mbona huwapigii kuwajulia Hali, Basi kutokana na uzoefu uliokuwa nao na uchovu w aswali Hilo la Kila wakati unaamua kuwachana kuwa huwapigii Simu kwa kuwa unaona aibu wakikuomba hela unawajibu huna Kila siku (Lengo la kuwaambia hivyo likiwa ni kuwataka wabadili fikra zao hizo na kuelewa kuwa ni kweli huna kitu),

Badala washuke ndo Kila mmoja anapanick hivi Yani mzazi anakuwa kama anakuachia laana hivi "Kwahio kumbe hunipigii simu ili nisikuombe hela, Sawa usipige Tena ishi Kama huna wazazi na Wala sitohitaji hela yako" unajaribu kumfafanulia vizuri kwanini umemuambia hivyo anakukatia Simu,

Sasa jamani Wanazengo embu Naombeni Ushauri Kwani wazazi wa kisasa wametuzaa watoto kuja kuwasaidia wao au wao kuwasaidia watoto kutimiza malengo ili kizazi kiendelee kudumu? Ninachojua Mimi ni kwamba mimi ndo ningetakiwa niwadai wao haki ya kutonisomesha au kunihakikishia nakuwa na kazi ya maana, Au ebu ninyi nisaidieni wakuu, Maana wazazi wao ambao ndo mababu zao atleast wamewaachia mashamba na nyumba hata kama ni za msonge.... Ila wazazi wetu Hadi leo asilimia kubwa ndo nyumba za kupanga alafu wanatufanyia hivi watoto wao je, ni Nini matokeo ya yote haya?
 
Nitarudi kukomenti baadae now nipo bize na liverpool
 
Muhimu achana na anasa kama unafanya.

Waambie wazazi wako ukweli wa shughuli zako na kipato chako.

Kama wazazi wako ni waelewa watakuelewa tu.

Mimi wakati nafanya kazi za ulinzi nilikuwa nalipwa Tsh 250,000 kwa mwezi. Mama sikumwambia kazi niliyokuwa nafanya.

Alijua sina mchongo, bado nahangaika tu, hivyo hata nikimtumua Tsh 15,000 au 20,000 au nikisema sina amtafute ndogo wangu anashukuru tu.
 
Jifunze kuwasaidia wazazi wako hata kidogo ukipatacho utapata baraka zaidi ,
Usikute unalalamika hivi kumbe kuna kadem kakikupiga kiziga unakapa tena kwa unyeyekevu tu
Shukuru kama una wazazi waelewa mkuu,
 
Jifunze kuwasaidia wazazi wako hata kidogo ukipatacho utapata baraka zaidi ,
Usikute unalalamika hivi kumbe kuna kadem kakikupiga kiziga unakapa tena kwa unyeyekevu tu
Kumsaidia demu ni lazima. Mbona naye ananisaidia? Au mnataka tubake kuku ndio mfurahi
 
Kijana wekeza kwa wazazi unaweza rudishwa hujiwezi hata kunyanyua mkono na hao mademu washkaji ukipata tatizo utajua kwamba hujui wekeza homs mi sina kawaida ya kusalimiaga nyumbani tangu zamani ila kila mwisho wa mwezi ni lazima tuwasiliane na wazazi wangu unaweza kuta kwa miezi mitatu nyuma siku nimeombwa hela na baba tena amevuta sana mpaka siku nakaribia kupata pesa ndo akaniambia tatizo

Ila kila mwisho wa mwezi lazima kwa mama muamala usome na baba pia sina tatizo swala la kupigiana simu sio sana ila kwa kujua afya zao ni kilometer zimeenda nimkatia bima mzee mother nae so naona mafanikio asikwambie mtu since nipo chuo japo nilipoanza nilipangiwa chumba kulipiwa ada nusu hapo nikanyanyuka mpaka leo na chuo boom nilikuwa natuma home
Saidia wazazi ndo wao huu hakuna baraka zaidi ya hyo duniani
 
Kama hawaelewi ishi kwa nadhiri yako. Nadhiri ikikwambia hiki kitu ni sahihi, basi ni sahihi kweli. Hata kama huendi kanisani au msikitini nadhiri hukuelekeza nini uishi.

Wasipoelewa kabisa bora wapige pending kwanza then ukisimama kimaisha ndio uwabebe. Yani uhangaike mtaani, kazini kisha wazazi wakutishie. Mbona wao yaliwashinda
 
Kumsaidia demu ni lazima. Mbona naye ananisaidia? Au mnataka tubake kuku ndio mfurahi
Kumsaidia dem wako haikatazwi, lakini sasa ndiyo uhonge kinyenyekevu kwa kumpigia hadi magoti uki provide?

Wakati huo wazazi wako huko sangamwalugesha ushawapa kisogo, hausikii wala hauelewi kisa hako kadem!

Hicho ndiyo kinachoongelewa.
 
Back
Top Bottom