S
Unregistered said:Tanzania does not like EAC yet they have become a backyard South African supermarket
Unregistered said:Nadhani mumemsikia au kumsoma wenyewe namna mkenya alivyo "arrogant". Anasema Kenya ni super power ya Afrika Mshariki. Anasema kuwa watanzania kazi yetu ni kukaa chini ya minazi kusubiri ruzuku ya serikali kama ilivyokuwa wakati wa vijiji vya ujamaa. Anasema kuwa katika eneo hili la Afrika mashariki inayofahamika ni Kenya tu iwe michezoni na kadhalika. Huyo ni Mkenya halisi na lugha yao siku zote.
Lakini Mkenya huyo hakusema upande wa pili kwamba wao pia ni wezi; kwamba katika jiji la Nairobi pamoja na kuwepo mjumba mazuri ya ghorofa pia kuna nyumba za maboksi; ambapo watu huweka vinyesi kwenye mifuko ya plastiki kwani hawana vyoo; kwamba wizi wa Kenya pia upo katika fikra zao ambapo ukipanda Kenya Airways unapoingia Tanzania huwa hawasemi kuwa sasa unaingia Tanzania isipokuwa utasikia tu upande ule wa kushoto au kulia kuna mlima Kilimanjaro ili abiria wafahamu kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.
Mkenya huyo licha ya kuikashifu Tanzania hajazungumzia umaskini mkubwa uliopo Kenya. Hao ndio Wakenya wanaotaka Shirikisho la Afrika Mashariki kwa manufaa yao ya kiuchumi na kibiashara.
Je, mnawataka Wakenya hao? Hiyo ndiyo sura yao halisi. Lugha ya jeuri na majivuno kwamba wao wamesoma sana na kwamba watanzania hupeleka watoto huko Kenya. Ni kweli watanzania hupeleka watoto wao huko Kenya na pia Uganda, kwa hiyo kwa Wakenya hiyo ni sifa tosha kweli kweli. Wao ni Super Power.
Nawathibitishieni wao ni super power katika wizi na "arrogance". Vipi Kijeshi? Sina hakika na hilo, pengine pia ni Super power. Labda siku moja wakati wa Shirikisho tutakuja ona ni nani super power kati ya tanzania na Kenya, kwani kwa maoni yangu kama ndio tabia hii ya wakenya ya kuwadharau watanzania itaendelezwa ndani ya shirikisho ni lazima litajitokeza jambo na hapo ndipo super power wa kweli atakapofahamika. Wakenya hao waje, Tanzania na watamke lugha hiyo vijijini ndani ya Tanzania waseme nyie watanzania hamjasoma, hapo ndipo watatambua maana ya kuzuia ulimi wao.
mzalendo halisi
Claud Gwandu said:Charles Obbo Onyango namfahamu kwa muda mrefu amekuwa mtu mwenye mawazo hasi kuhusu Tanzania na Watanzania na hilo linajionyesha katika moja ya article zake alizotoa baada ya kifo cha Baba wa Taifa,mWALIMU jk Nyerere okotba 1999.Yeye,kama walivyo nyang'au wengi wanachotaka ni ardhi na rasilimali bikira zilizo Tanzania na wala si kitu kingine chochote