DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Watu watano wamejeruhiwa baada ya pikipiki ya magurumu matatu (guta) waliyokuwa wakisafiria, kugongana uso kwa uso na basi la abiria lenye namba za usajili T355 DCP lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Kijiji cha Kwala Msanga, Mkoa wa Pwani.
Inadaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni dereva wa guta aliyeingia barabarani bila kuchukua tahadhari, ambapo inadaiwa kuwa dereva wa basi alimpigia honi lakini hakusikia kwani alikuwa amevaa 'earphones' masikioni.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe leo Julai 13, 2025 ambapo watu hao watano waliojeruhiwa ni waliokuwa kwenye guta.