Kwa muelekeo wa matokeo ya Urais inaashiria JK Kushinda kwa asilimia 65 mpaka 73. Eneo la Makadirio la Synovate na Redet. Hii inatuambia kuwa watu wakifanya utafiti wa Kisayansi tunahitajika kuutafakari utafiti huo na kuufanyia kazi, kuliko hatua iliyochukuliwa na wapenda mabadiliko wengi wa kuubeza na kuudharau. Limekuwa funzo jema lililogharimu wapenda mabadiliko miaka 5 ya kujipanga upya. Kama wapenda mageuzi wa kweli tujifunze kutokana na hili na kujifunza kuwa mabadiliko hayaji kwa kulazimishwa, bali kwa ushawish wa hoja na mipango madhubuti ya ushindi. Tuepuke kushabikia tusiyokuwa na ushahidi nayo na tuepuke kujiona tupo sahihi zaidi ya wengine. Kwani sio lazima wote tubadilike, wanaooona mabadiliko yanafaa wabadilike ile wale wasiohitaji mabadiliko wafaidi Mafanikio ya mabadiliko hayo. Kidumu Chama cha Mapinduzi, Kidumu Chama Tawala. Hongera Rais Kikwete. Tehe tehe tehe