EAC to revive stalled talks on expelled Rwandans

ah, sasa wewe unawaonea huruma wanyarwanda, je wabongo halisi waliyotimuliwa utasemaje, huku wahindi na hao waarabu unaosema wanapeta? mi namuonea huruma na namuombea kwa Mungu Mh. Magufuri afanikiwe kuokoa jahazi! kwani mambo mengine yananizidi uwezo, hebu tazama...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzanians-mistaken-for-illegal-immigrants.html
 
"Prof. Sempebwa further contended that the expelled Rwandese were and still are bonafide citizens of an EAC member state "and therefore infringes the Treaty because they are entitled to the right of residence and the right of establishment as well as other rights within the Treaty and the Common Market Protocol of the Community".

..tatizo liko hapo kwenye hayo madai.

..mkataba wa EAC hauko juu ya sheria za Tz zinazohusu uraia na ukaazi.

..hao wanasheria wanadai Wanyarwanda na raia wengine wa nchi wanachama wa EAC wana haki ya kuingia, kutoka, na kuishi Tz vile wanavyoona inafaa na mamlaka za Tz hazina haki ya kuwazuia.

..msimamo wa Raisi Magufuli ni kwamba, anayetaka kuishi na kufanya kazi Tz, basi afuate sheria za Tz.

cc Geza Ulole, MK254, mchambawima1, Ngongo
 
JokaKuu nafikiri kabla ya kutupatia msimamo wa Raisi ingekuwa ni busara ukaanza kwa kutufahamisha sheria za Tanzania kuhusiana na hilo swala kwani ndio la muhimu zaidi, na kama zinatofautiana je ni kwenye nini haswa? NB: nchi yoyote ile utakapo kwenda, upende usipende utafwatisha sheria zao tu, hakuna jipya hapo!
 
Maswali ya msingi .... Je, kuna sheria ya nchi inayoitwa EAC? Kama hiyo sheria ipo hawa waliofukuzwa na kwenda Rwanda/Burundi hiyo right haipo huko walikokwenda? Je, ni sheria ipi ambayo inapewa kipaumbele kwenye maswala ya ukaazi? Je, sheria za Tanzania kuhusu ukazi ni batili? Hawa wanaojifanya ma-professor wa sheria wasituzingue, wapo hapo kufaidi pesa za walipa kodi wahamiaji wote haramu warudi kwao wafanye kazi na walipe kodi, hii ndio mirija ya kuwa na jumuia ambayo haina meno na sheria zake ni legelege. Tanzania hatuwezi kukubali kuwa na wananchi wa nchi za Kenya, Rwanda, Burundi, na Uganda ambao ni economic migrants ambao kwao hawawezi maisha wanakuja huku kupenda dezo. JPM sasa kashika hatamu hatutaki mchezo ni kazi tu fukuza wahamiaji wote haramu na wale wanaojifanya ma-expart wanaofanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na wazawa.
 

Wewe ndie unayeleta ligi za kipumbavu, hizo ni errors zilizofanyika wakati wa ku round up ndugu zako, na wote waliokamatwa kimakosa waliachiwa before the processing stage. Either onyesha mtanzania mmoja aliyefukuzwa Tanzania kwenda Rwanda or shut up already. You have no proof just like your other arguments! Hakuna nchi hata moja duniani (Rwanda included) inayokubali kupokea Raia wasio wake unless ni wakimbizi. Ili ndugu zako wapokewe Rwanda ni lazima rwanda ijithibitishie kuwa hao ni wanyarwanda. Unataka kusemaje? kuwa wale mliowajengea nyumba na kuwapa sijui ng'ombe (your own thread) ni watanzania?
 

Mkuu achana nao.Mwishowe sheria za Tanzania zitaheshimiwa Tu!! Hata Rwanda we ingia tu.hukai hata siku tatu bila kutimuliwa aisee..Hiyo ni kawaida.Tunaposema kuwa kuna uhuru wa kuishi kokote haimaanishi usifuate sheria za huko unakokwenda kuishi.Ukitaka kuishi Tanzania fuata sheria za Tanzania..kama hautaki rudi kwenu.Kama hautaki tutakurudisha kama mhamiaji haramu..Hapa kazi tu
 

JokaKuu Mimi nakusoma vizuri sana, kila nchi ina sheria zake na ni lazima zifuatwe na hata wageni wanaokuja. Huwezi kwenda kung'ang'ania uishi nchi ya watu bila kuzingatia sheria zao za huko, unafaa aidha ufunguliwe mashtaka au ufukuzwe. Hata Kenya tumewaruhusu wageni wengi tu, wanapiga shughuli zao kila siku na bila kuzinguliwa, lakini wakipinda kidogo huwa wanajipata mashakani.

Lakini pamoja na hayo, huoni kuna makosa yalitendeka kwa kuwafukuza watu waliozaliwa Tanzania na kuishi zaidi ya miaka arubaini. Jameni mtu kama huyo hata kama asili yake Marekani, lazima utakua unamchanganya kabisa na atang'ang'ania kubaki hata kama kwao ni nchi ya maziwa na asali.
 
Pamoja mkuu,ulichosema ni sahihi mkuu,kuzaliwa hapa kuishi hapa nk kama hukuomba uraia na ukakubaliwa hakukufanyi uwe raia. Siku wakifanya mambo yao watakutoa tu.
 
according to EAC treaty people have the right to live anywhere in east africa? really?

hakuna hiyo kitu, pamoja na kwamba nchi za eac lakini kwenye mambo ya uraia kila nchi ina sheria zake. Raia yeyote ambaye sio mtanzania lazima afuate sheria za kukaa nchini kwa maana ya kibali cha kuishi. kuwa kwenye shirikisho hakumaanishi kunaruhusu wanyarwandwa wazurure na waishi kwenye nchi za wengine bila utaratibu.
Na kwanini wasikae nchini kwao kuna nn??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…