Inaendelea ktukoa mwanzoni......
Kozi: Tumesema kuwa wapo watu wanaodhani ukifanikiwa kupata kozi fulani basi mambo yatanyooka. Hili linatokea kuanzia huko sekondari hadi vyuoni. Watu hawangalii uwezo wao na kile wanachokiataka kukifanya. Aghalabu utasikia nataka niwe Daktari, lawyer au Engineer pengine kwa kudhani kuwa uwepo wao huko ni alama ya heshima na uwezo
Ukweli ni kuwa unapofanya kile unachokipenda na si kile unachopendezwa nacho basi uwezekano wa kufanikiwa ni mkubwa sana. Katika dunia ya leo kinachokusaidia ni jinsi gani unaweza kutumia fursa ili kujiendeleza na si masomo gani unayosoma. Mfano mzuri ni ule wa kudhani kozi za Art ni hafifu kuliko za Science. Ukitazama kwa undani watu waliofanikiwa ni hao wanaonekana dhaifu na si wale waliong'angana ilimradi tu nao wawemo katika kundi.
Kuna kijana mmoja alianza na kozi ya diploma ya ualaimu, halafu akajiunga na chuo kikuu katika kozi ya B. Science general. Baada ya hapo akajiunga na kozi za utafiti wa wanyama. Kwasasa hivi ni mmoja kati ya wanasayansi wakubwa duniani na hakika maisha yake yamebadilika sana. Huyu alianza kama Mwalimu na sasa ni mtafiti wa kutumainiwa tena katika mataifa makubwa.
Nimesoma maoni ya watu katika nyuzi mbali mbali zikisema mwisho wa Engineering ni degree ya kwanza kwasababu master au Phd hazina mashiko. Lakini jiulize kama mtu amesoma engineer na kisha kupata kozi nyingine kama MBA unadhani soko lake lipoje. Focus ya mtu isiwe engineer bali engineering itamwezeshaje yeye kubadili maisha yake katika sekta yeyote ile.
Katika nchi yenye upungufu wa watalaam kama Tanzania, mwalimu anaweza kubadili taaluma yake na kuwa mwandishi wa habari. Tunakoelekea ni kule ambapo mtu anakuwa na taaluma za kutosha zimwezeshe yeye kusonga mbele.
Mathalani, mwandishi wa habari za afya ambaye ni Daktari anasoko zuri kuliko mwandishi tu wa habari.
Mwandishi wa habari anayejua mambo mengi ya kijamii anafursa nzuri tu kuliko mwandishi wa habari anayesubiri kuandika kilichosemwa.
Lakini pia kama umesoma Bsc general au Ba. general kwanini usifikiriekuwa kuna nafasi unazoweza kuzipata kwa kutumia fursahiyo? Unapokuwa na kitu general ni jambo jema lakini ni vizuri zaidi ukawa na speciality. Speciality inakupa nafasi zaidi miongoni mwa watu wengi. Bsc yako unaweza kuielekeza katika Biology na huko ukazama katika vitu kama zoology, wildlife, environment control n.k.
Ni muhimu ukaelewa kuwa kozi peke yake haijaweza kukupa ufumbuzi wa suala la ushindani. Ushindani ni jambo jema lakini kama una nafasi ya kupunguza huo ushindani basi fanya hivyo. Nina maana kuwa ukisoma kitu jaribu kuwa na vitu vya ziada. Huwezi kuwa archtect mzuri kama hujui kutumia computer na program zake zinazohusu fani yako vizuri.
Huwezi kuwa mwandishi mzuri kama hujui njia za kuapata habari za dunia kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano iliyopo duniani kwa sasa. Huwezi kuwa Daktari aliyefanikiwa kama hujui mbinu za utawala na usimamizi wa vitu kama miradi.
Hoja yangu hapa ni kuwa uzuri wa fani unaoutaka hautoshi ni lazima uwe na vitu vya ziada ili uwe 'total package'
Kuna vitu vingine huwezi kufikiria ni muhimu lakini dunia ya leo ni muhimu sana.
Nikupe mfano wa kuchekesha, endapo itatangazwa kazi na katika watahiniwa 299 umefanikiwa kuwemo katika 3 bora, hapo maana yake ni kuwa nyote watatu mnavigezo amabavyo mwajiri wenu anavitaka 'potential candidate'
Suala linakuja ni nani ambaye ni bora kuliko wenzake.
Mchanganuo wa kazi ni wa utafiti 'research' ambayo mtahiniwa anatakiwa asafiri kila mara ima kusimamia, kuongoza au kukusanya takwimu. Mwajiri ataangalia vigezo vyote na kuona mmefungana.
Hapo mwajiri atatoka nje ya vigezo vya kazi (CV/Resume) na kuangalia vitu vingine. Katika watahiniwa wote watatu, wakwanza ana GPA kubwa tu, wapili ni mzuri wa takwimu na watatu hafikii vigezo hivyo lakini anakitu kimoja, nacho ni leseni ya kuendesha gari.
Usijeshangaa huyu mwenye leseni akapata ajira kwasababu yeye kama wengine anauwezo wa kufanya kazi tarajiwa, lakini atalisidia shirika au taasisi kuondokana na bajeti ya kuajiri dereva.
Huyu inaweza kuonekana amependelewa lakini ukweli unabaki kuwa yeye ni msaada na si mtegemezi. Vipi kama hao wawili wa mwanzo wangekuwa na leseni hata kama hawana gari!!
Inachekesha na kuonekana kama ni ujinga, trust me, dunia ya leo mwajiri anataka assert na siyo liability.
Hapa nina maana kuwa degree yako ikusaidie kufikia malengo mengine, wenyewe wanasema 'diversify' ya kwamba wewe ni Engineer, lakini pia unauwezo na ufahamu mzuri wa computer na una certificate ya project management. Zaidi ya hapo umefanya MBA yako kwahiyo una skills zote za management.
Lakini pia jiulize, je una vigezo vya mwajiri anavyovitaka kama lugha? ni kwanini basi baada ya kupata degree yako usifikirie kunyoosha lugha yako kwa kozi ndogo ndogo, mathalani kule British council. Hutuwezi kuepuka suala la lugha vingnevyo tutabaki tukilalama, wakenya wanaajiriwa, warundi wanaajiriwa! ni lazima tuwe 'fit' kwa ushindani
Hayo tu hayajawa silaha nzito za kupambana na ushindani, bado una kazi ya kumshawishi mwajiri kuwa una haki ya kupata mwaliko wa interview. Ushawishi huo unatokana na jinsi gani umeandika taaluma yako na kumvutia mwajiri na je kweli ni wewe umeandika? hapo yanakuja masuala mawili
1.CV/resume writing
2. How do you present your CV before the panel
Itaendelea.......