Na je umeshamwona mgombea flani tajiri sana akijipitisha kwa wapiga kura wake walio masikini kwa 95%. Ulimuona anavyojifanya kuyafahamu matatizo ya wapiga kura wake hao?na jinsi alivyo hodari kuyaainisha,yes mi nimeona mgombea ubunge. Aki jaribu kutoa mchanganuo wa jinsi atakavyo jitahidi kutatua tatizo sugu la maji kwa kuwachimbia visima vitatu na jinsi atakavyoomba misaada ili kupata vijisenti kidogo vya kukarabati banda moja la kijiji ili liweze kutumika kama zahanati ikiwa ni kipindi cha mwisho cha uwakilishi. Na wakati wote huo mgombea huyu alikuwa kasimama juu ya Lexus yake huku mtoto wake akiwa kaketi juu ya bonet la HUMMER. Baada ya blaablaa tukampigia makofi tukamwimbia mapambio akaenda zake sisi tukaendelea kuumiza kichwa namna ya kupata maji japo ya kukorogea uji tunywe tulale.the world is absolutely fair, we are extremely unfair.