MK254Hapa hamna ubishi wala nini, kivumbi kitakua baina ya Wakenya na Waethiopia kwenye mbio za Olympic marathon kule Rio mnamo Agosti 21. Mashabiki wote duniani wanasubiri kwa hamu kuona mchuano baina ya hizo team mbili, japo kutakua na wakimbiaji kutokea nchi zingine, ila hao watakua wapambe tu. Lakini lazima tuwe makini na Mganda fulani kutokea kwa jamii ya Wakenya.
Marathon ya wanaume huwa kama hitimisho au fainali ya Olympics.
Mashujaa wa Kenya tunategemea:
Eliud Kipchoge
Stanley Biwott
Kutokea Ethiopia tunaye:
Tesfaye Abera
Eritrea nao hawachelewi, wanaye:
Ghirmay Ghebreslassie
Uganda kuna huyu jamaa mwenye majina ya Kikenya jamani, anaogopesha kiaina:
Stephen Kiprotich
Yote tisa, timu zote hizi za Mashariki mwa Afrika, hivyo ni fahari kwa ukanda huu.
MK254
Tupia basi hapa Jamiiforums their '' personal best times'' tuweze kuona kasi na pia ubora wao.
Je mchuano huo marathon KM 42.2 unaweza kuweka rekodi ya Olympics kuwa 2:00:00 au 1:58:57 ? the world record for the marathon is 2:02:57, set by Dennis Kimetto in Berlin 2014 and second fastest 2:03:38 by Patrick Makau in Berlin 2012.
Kenya ina watu zaidi ya milioni 40 hivyo hatuwezi kwenda wote kule. Wengine inabidi tuwe mashabiki na kuwakilisha kwa mambo mengine.Mbona akina Wamae, Githimba, Gichinga na Munyui hawapo kwenye majina ya Kenya?
amesema (eluid) Rio iko na polution na pia iko na humidity kwahivyo inaweza affect forign athlete,,,, alisema yeye mwenyewe ashawai kuishi brasil kwa miezi sita lakini alikua akiishi sao pailo, lakini Rio iko poluted sana mpaka unaskia hewa ikiingia... but anyway good thing ni owamba local athletes ndo wako na advantage pekee, the rest suffere the same fate, lets pray hio siku ya 21st mawingu yatachulua humidity yote na ile mvua ilikua inanyesha jana imeenda na hio polution yote, alafu tuombe mungu all goes well atleast pia sisi tuvunje rekodi kwa hii olympic, BTW nani anajua steeplechase ya 3000m men iko lini? hapo its nothing else other than 1-2-3 and posibly 4 finish at the podium ..Mwaka huu wa 2016 Eliud Kipchoge ndiye anashikilia taji ya kasi zaidi kwa kuwa na rekodi ya 02:03:05. Labda tusubiri tuone kwenye hii ya Olympic ataikwenda vipi, naona kama atavunja rekodi zote maana dogo yuko fomu sana.
Kenya ina watu zaidi ya milioni 40 hivyo hatuwezi kwenda wote kule. Wengine inabidi tuwe mashabiki na kuwakilisha kwa mambo mengine.
Ni jinsi tu hautapata kila Massawe, Mrema n.k. kwenye timu ya mpira ya Tanzania.
hili swali la kijinga ni kama kuuliza kwa nini wamarekani weusi wanashiriki kwenye sprints na sio wamarekani weupeMbona akina Wamae, Githimba, Gichinga na Munyui hawapo kwenye majina ya Kenya?
Kilomita 42 ni nyingi sana, anything can happenGold ni yenu huyo Kipchoge ni habari nyingine
Kilomita 42 ni nyingi sana, anything can happen
Tanzania ya akina Kiyomo,Filbert Bayi,Gidemas Shahanga,Zakaria Barrie,Juma Ikangaa... Ilitutoa kimasomaso.Inabidi tuwe wapole kizazi cha mashujaa wa mbio ndefu,kati na fupi kimetoweka.
Hahaha....funny but very correct.kilam
Sawa,Wakalenjin washangilie...... Je, wanapokuwa huko huwa wanabeba, kupeperusha bendera na kuimba wimbo wa Kikalenjin? Ama kipindi cha Rugby Sevens,unataka wajaluo,waluhya na wakisii waimbe wimbo gani? Yule Mkenya of Indian descent anayewakilisha Kenya kwenye kurusha mishale amebeba bendera ya Kihindi?Kumbuka ni wanasiasa ndio hujaribu kutugawa, wanamichezo ndio hutuunganisha.
Mkuu, kweli hapo inatakiwa tujipange wabongo. ,Ngongo Vipi na kwenye kurusha mishale au hata kuogelea, yaani chochote kile maana kutokea kule Rio bila medali hata moja inakua aibu jamani.