Athleticss Kenya yatangaza kikosi matata cha wanariadha waliofuzu kuiwakilisha Kenya kwenye Marathon ndani ya mashindano ya Tokyo Olympics 2021

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,264
2,000
Matayarisho ya kukwapua medali na kuendeleza heshima ya Kenya kimataifa kwenye riadha yameanza kwa bashasha. Baada ya muda mrefu wa kimya kikubwa kwenye ulingo wa michuano ya riadha kimataifa, kisa athari za janga la COVID-19. Hii ni baada ya Athletics Kenya(AK) kutangaza rasmi wanariadha watakaojumuishwa kwenye #TeamKenya kwa kitengo cha marathon ndani ya mchuano wa Olympiki Tokyo 2021.

Mashindano hayo yataanza rasmi tarehe 23 Julai 2021 baada ya kuhairishwa kwa mwaka mzima. Kenya itawakilishwa kwenye marathon na mabingwa wanane(wanne kwa kina dada na hivyo hivyo kwa wanaume), wakiwemo mabingwa Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei ambao wanashikilia rekodi za dunia kwenye mbio za wanaume na wanawake mtawalia.

AK ina matumaini ya mafanikio makubwa kule Tokyo na sio kwenye mbio za marathon tu. Ikizingatiwa kwamba wanariadha wa Kenya wamekuwa wakiendelea na mazoezi ya kujitayarisha kwa mashindano ya Olimpiki, bila kusitasita, kwa muda wote huo. Matayarisho yanaendelea kwa kina kwa michuano ya kufuzu kwa wanariadha wengine wa Kenya, kwenye mbio zingine zote ambazo watajitosa uwanjani na kushiriki kule Tokyo.

All the best to our beloved CHAMPIONS! Bendera mashuhuri ya Kenya lazima itapepea juu zaidi, bila shaka.

Athletics Kenya names Olympic marathon team - Canadian Running Magazine
 

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,074
2,000
Safi sana hii....
Hebu tuambiwe matokeo ya Kilimanjaro marathon, nina uhakika Wakenya wachache waliojitoa mhanga na kwenda lazima walifanya yao.
 

kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,025
2,000
Wote Wakalenjin kama kawaida, Bantu jiwekeni kando na miguu yenu mizito kama ina funza.
 

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,264
2,000
Wote Wakalenjin kama kawaida, Bantu jiwekeni kando na miguu yenu mizito kama ina funza.
Labda miguu yako na wabantu wenzako huko Tanganyika. Wabantu wa Kenya wanang'aa kwenye raga na mpira wa wavu pia. Timu ya Kenya raga 7s kwa kina dada ndio mabingwa wa Afrika na wanaume nao wapo kwenye nafasi za juu duniani.

Bila kusahau kwamba kina dada wa Kenya ndio mabingwa wa mpira wa wavu barani Afrika. Timu zote hizo za Kenya, kwenye michezo niliyoitaja, zilifuzu kuliwakilisha bara la Afrika kwenye Olimpiki kule Tokyo.
 

kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,025
2,000
Labda miguu yako na wabantu wenzako huko Tanganyika. Wabantu wa Kenya wanang'aa kwenye raga na mpira wa wavu pia. Timu ya Kenya raga 7s kwa kina dada ndio mabingwa wa Afrika na wanaume nao wapo kwenye nafasi za juu duniani. Bila kusahau kwamba kina dada wa Kenya ndio mabingwa wa mpira wa wavu barani Afrika. Timu zote hizo za Kenya, kwenye michezo niliyoitaja, zilifuzu kuliwakilisha bara la Afrika kwenye Olimpiki kule Tokyo.
Acha ujinga wewe, hapa tunazungumzia riadha wewe unaleta mambo mengine.
 

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,264
2,000
Safi sana hii....
Hebu tuambiwe matokeo ya Kilimanjaro marathon, nina uhakika Wakenya wachache waliojitoa mhanga na kwenda lazima walifanya yao.
Niliona wa kwanza kwenye kitengo cha wanaume alimaliza marathon kwa muda wa 2:18:04. Huyo akija Kenya ashiriki Nairobi Marathon au Lewa Marathon hata nafasi ya 50 tu hataiona. Alafu akijitosa kwenye mbio za wanawake itakuwa bahati akihesabiwa kwenye Top 30.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom