Ninamaliza mwaka wa pili kwenye vicoba sasa baada ya kujifunza mambo mengi. Nimeona inavyonufaisha ikiwemo kuniongezea akili ya kutafuta pesa,nidhamu ya matumizi,kupata mkopo wenye masharti nafuu kwa wakati muafaka,kuwa sehemu ya umiliki wa mtaji pamoja na kujifunza mbinu kadhaa za kujiongezea kipato.
Jambo la msingi ni kuheshimu katiba,kikundi na wanakikundi.