Du...Hata kamanda Mwema asingependa watu waone hii... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Du...Hata kamanda Mwema asingependa watu waone hii...

Discussion in 'Jamii Photos' started by Paulo, Feb 2, 2011.

 1. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mungu amefanya haya Misri ili askari polisi wa Tanzania nao wapate kujifunza. Maandamano yaliyotokea arusha hakupaswa kufa mtu ndugu zangu. Uhai ni wa Mungu na yeye ndo mwenye kuitoa roho ili imrudie. Majeshi ya Misri yalijifunza kupitia pigola kumi kipindi cha Musa ambapo wazaliwa wa kwanza wa kila kiumbe walikufa ndani ya usiku mmoja. Tokea hapo wanaheshimu damu! Hawaimwagi tena!

  Hizi picha ni kutoka kwenye maandamano yanayoendelea huko Misri
  source http://totallycoolpix.com/2011/01/the-egypt-protests-part-2/
  [​IMG]

  Hapa wanaruhusu waandamanaji wapande juu ya vifaru vyao.
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]

  Hapa ndo wamenikosha kabisa
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tutafika tu Inshallah!
   
 3. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tutafika huku tu, Yan Mwema na Vibaraka wake watashindwa tu! Ila tatizo la vibaraka wa mwema ni njaa! hawajui pakula kesho wakiachishwa kazi, ila wajue umma ukikasikira tupo wakujitoa mhanga.
   
 4. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
   
 5. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu trustme unadhani hata Misri hakuna njaa? The price of food has sky rocketed. Sema ni waelewa na wanajua kwa hayo maandamano watapata serikali mpya yenye kujali maslahi ya wananchi wake. Hawa wa kwetu ni elimu ndogo. wanahitaji kuelimishwa.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Kweli ni Ajabu maandamo watu wanaenda na watoto?
  Kweli kuna Somo la kujifunza hapa
   
 7. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tena mtoto mwenyewe ni kichanga!
   
 8. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Yaani nimeipenda sana hii mkuuu thanks nyingine naongesa hapa.mipolisi yetu sijui ndo minunda sijui ndo elimu yani ipo ka matahaira flani.
   
 9. terrell

  terrell Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaweza ikawa ni Elimu na njaa
   
 10. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ya huku ni kama 'Mbwa', akiambiwa kamata, piga, galagaza na ua, wala hana haja ya ku-reason sababu. Yeye anatekeleza amri ya kamanda wake bila kufikiri. Mi naona ni kama wanyama tu!

  Hukumbuki kamanda mmoja alipigwa mtama na mwanasiasa kule Maswa, lakini kwa vile hakupewa amri ya "shikamata" na mkuu wake, alikuwa mpole tu, akainuka akakun'guta vumbi makalioni akawa mpole.
   
 11. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  dooh no nooma mwana,yani watu wanaelewa na wamechoka kuonewa ,loooh in Tz inakaribia kuja lets wait for the day
   
 12. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,661
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  Lovely, mi najiulizaga hivi hawa wanajeshi wetu sio sehemu ya wananchi, hakuna ndugu zao kweli wanaokosa matibabu au kukosa elimu ya uhakika kutokana na mifumo mibovu iliyopo? Wanajeshi Wamisri nawapa BIG UP!
   
 13. LD

  LD JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Polisi na ASkari wetu, Fikirini kabla ya kutenda.
  Mkiambia nenda jiulize kwa nini unakwenda.
  Tumieni akili, kwa kweli, mnatutia uchungu sana.
  Ninyi ni jeshi la wananchi sio jeshi la mtu yoyote hapa.

  Lakini siwalaumu sana kwa sababu AMIRI JESHI MKUU WENU NI....................
  Hatutegemei tofauti sana labda kama Mtapewa Neema ya kujitambua.
   
 14. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  So long hawaelekei upande wa mjengo, hamna tabu
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hii kali sana kunasomo lakujifunza hapa kwa police wetu na majeshi yetu na ninaamini kabisa siku tukilianzisha kisawasawa nao watakuwa upande wetu kwa sana
   
 16. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakifyatua mabomu ili kuwatawanya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waliokuwa wakiandamana leo asubuhi kuelekea Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kufikisha malalamiko yao ya posho ya Sh 5,000/ ambayo wanadai ni ndogo haitoshi kwa matumizi na badala yake wanaishinikiza Serikali kuwapa Sh. 10,000/=. Hata hivyo maandamano hayo yaliishia maeneo ya Savei baada ya kukuta ukuta wa polisi hao umetanda Barabarani huku wakitoa matangazo ya kusitisha maandamano hayo na kutawanyika, baada ya kutoa matangazo hayo na wanafunzi hao waliendelea kuwa maeneo hayo huku wakiimba ndipo askari hao waliamuliwa kuanza kufyatua mabomu ili kuwatawanya. Katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa ila ni wanafunzi wachache tu waliokamatwa.
  [​IMG] Bomu la machozi limeshaachiwa hapa likianza kufyatuka...

  [​IMG] Wanafunzi hao wakitawanyika kwa kukimbia kila mtu na njia yake baada ya mabomu kuanza kufyatuliwa.
  [​IMG] Wanafunzi hao wakiandamana, kutoka chuoni...
  [​IMG] Wakiwa na mabango yao yenye ujumbe kuhusu kile wanachodai na wasichohitaji.
  [​IMG] Safari ilikuwa ni ndefu huku wakitembe, kukimbia na kuimba ili kuifanya safari hiyo kuwa fupi zaid lakini waaapi, iliishia karibu zaidi.
  [​IMG] Maandamano bado yalikuwa yakiendelea kutokea chuoni hapo.
  [​IMG] Mkusanyiko ulianza kama hivi...


  Linganisha hizi na za misri.


  Hebu tuwe serious jamani, 5,000/= per day ni peanuts,hatuhitaji kuandika "wakidai kuwa ni kidogo", ukweli ni kuwa hela nii ni njiwa mno.


  Haihitaji watoto waandame ili kuongezewa kiasi hiki na kama walioko madarakani hawaelewi kuwa hela hii ni ndogo basi for sure wako out of touch with reality.
   
 17. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Egypt ina jeshi lenye nidhamu ya hali ya juu sana katika bara la Africa. Askari wake wamejifunza na kuelewa ni wakati gani wanatakiwa kuchukua silaha na kupigana. Wamekataa kutumiwa na wana siasa. Kwa hili wanalolifanya, Gen Mwamunyange, Lt.Gen Shombo na Afande Chigonja wengineo wana mengi sana ya kujifunza. Kazi ya jeshi na polisi si kupiga raia wanapomkataa mwanasiasa hata kama ni Rais. Wanatakiwa kuwalinda raia....wanatakiwa kulinda uhuru na usalama wa nchi.
  Bravo Egyptian army!!!
   
 18. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Bravo Misri
   
Loading...