Dry eyes, safari ya uponyaji

Ukweli1

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
550
Reaction score
333
Nimeona niwashirikishe wenye dry eyes maana hii tiba ni lishe hata kama haitakutibu macho basi mwili utafaidika.

Nilikuwa nasumbuliwa sana na tatizo la dry eyes ikanipelekea kuwa na Surfer's Eye, ambayo daktari akaniambia tiba ni operation ila haina uharaka wala ulazima. Akanipa eye drop sikuona mabadiliko.

Nikaona isiwe shida nikaperuzi tiba asili, sasa natumia mafuta ya samaki na flaxseed, ninatumia hayo kila siku kama sehemu ya mlo kuniongezea Omega 3. Ya samaki asubuhi, ya flaxseed jioni. Nachoweza kusema kuna mabadiliko makubwa sana, baada ya wiki mbili za matumizi hata macho siyasikii, nilikuwa napata shida na mishipa ya macho kuuma sababu ya jua, hata nikivaa miwani ya jua ilikuwa inapunguza maumivu ila kwa mbali unasikia kama macho yanapata stress fulani. Sasa niko fit naweza angalia jua hata nikitoka nje bila miwani najisikia kawaida tu, ila najitahidi kutokuzoea kutokuvaa miwani hata nikisahau nairudia.

Nitatumia kwa miwezi miwili nitarudi tena kwa huu uzi kwa ushuhuda zaidi, tuombe uzima na uponyaji.

Kama hauwezi kupata mafuta tumia Omega 3 na flaxseed supplements.

NB: Miwani ninayovaa ni ya jua tu. Sina tatizo la macho zaidi ya niliyotaja hapo juu.
 
Mkuu imekuwa kimya Jumla, vipi surfer's eye iliisha au ulifanyiwa operation?
 
Mkuu nilisoma mahali kuwa flaxseed kwa mwanaume zinasababisha infertility sijui ni kweli au laa... Wajuvi watuambie
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…