Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267

Majukwaa ya vyama 9 vinavyounda muungano wa Rassemblement, wamemchagua Felix Tshisekedi, mtoto wa Etienne Tshisekedi kuwa rais wa Muungano huo na pia kumteua Pierre Lumbi kama rais wa kamati ya mazungumzo
Uteuzi wake umekuja wakati huu bado kukiendelea kushuhudiwa mvutano kuhusu uteuzi wa jina la waziri mkuu wa mpito
Rais wa Muungano huo atakuwa na jukumu la kufuatilia utekelezwaji wa makubaliano ya Desemba 31 mwaka jana, nafasi ambayo alikuwa akishikilia marehemu Tshisekedi kabla ya kufariki dunia
Hata hivyo vyama vitatu vya kwenye muungano huo havikukubaliana na mabadiliko mapya yaliyotangazwa, ambapo wajumbe wake waliamua kutoka kwenye mkutano uliokuwa ukiendelea kupata viongozi
Watu wa juu kutoka kwenye muungano huo wanasema kuwa, mgawanyiko huo ulioshuhudiwa wakati wa mkutano huo, ulitokana na Felix kukosa uzoefu mkubwa kisiasa hali ambayo wanasiasa kadhaa wamehoji utendaji wake.