Ninakupa Pongezi za dhati kabisa kwa kuwa na mawazo chanya. Ni imani yangu kwamba Dr. Slaa analifahamu hilo na yeye pamoja na Watanzania wote na si WA-CHADEMA kama wachache wanavyoamini, tupo pamoja nae katika kila hatua. Tunapaswa kulifanyia kazi kwa umakini kabisa na kwa moyo mmoja tena thabiti kuhakikisha ukweli huu unapatikana. Nitoe Pongezi binafsi kwa Dr. Slaa na kwa watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii kwa kuonyesha uzalendo wao katika kupigania haki ya wanyonge.........Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Dr. Slaa, viongozi wote wa CHADEMA, wafuasi, wapenzi, washabiki na Watanzania wote wanaotuunga mkono ktkt harakati za ukombozi wa Taifa letu.