Dr. Slaa: Natishwa

Kusema kweli bila Dr. Slaa, tuliyekuwa tumemwamini kwa uongozi wake makini na shupavu kujenga mabadiliko nchini, itakuwa shida kubwa kumwamini Lowasa ambaye anaonekana kama balaa ndani ya upinzani nchini.

Ni kweli sikuona kwa nini mtu mchafu anapobadilika umma usimsupport kumjenga katika mema. Lakini Lowasa kaja CHADEMa kwa kukataliwa na ccm. Ccm nao hawajamkataa kwa ufisadi kwa sabbu ufisadi ni sera ya ccm kwa hiyo hapana wa kumsema mwingine katika hilo. Ila kukataliwa kwa lowasa ni mahusiano binafsi kati yake na wenzake akaamua kwenda kuishi ukimbizini.

Ninajua viongozi wa Ukawa wako makini watampa miongozo yote wakati anapohitajika kuiua ccm. Lakini kama viongozi wa kumdhibiti wanasambaratika, nani atasimamia maadili ya CHADEMA ili kuona Lowasa hahamishi uccm na wafuasi wake kutamalaki kambi ya upinzani na kuifanya ccm version 3?

Kunahitajika mediation kuwa weka sawa viongozi wa CHADEMA na ninaomba asiwepo wa kujiona yuko juu ya wengine kwa sababu umoja wao ndio uliofikisha CHADEMA ilipo. Wanatakiwa kushikamana kwa pamoja sana katika kpindi hiki ambacho chadema inapokea wimbi la wakimbizi wa uchafu ccm.

Hatuna budi kujikumbusha kwamba katika msafara wa mamba na kenge huwa wamo. Bila kuwa makini na kusimamia misingi na maadili ya CHADEMA, tusije kushangaa kuona tumekuwa mateka wa fikra potofu za ubadhilifu, ufisadi, rushwa na kukosa uajibikaji wa ccm.
 
Dr kalinda heshima na utu wake wa kukataa kununuliwa na mafisadi papa safi dr huo ndiyo msimamo thabiti wa mwanaume.
 
kumchukua LOWASSA na kumuondoa slaa ni sawa na kumchukua Baloteli na kumuacha Ronaldo
 

Hii inawezekana kwa kiasi kikubwa ni mbinu ya kumwangusha Lowassa kwa kusema kuwa anatishiwa maisha. Kwa nini asitoe taarifa polisi badala yake anaongea na magazeti? Na ni makundi/ mtu yeyote mwenye uadui aidha na Dr. Slaa mwenyewe, Lowassa, CCM, au Chadema waweza/ aweza kufanya uhalifu huo. Hivi lile sakata la kutaka kuwekewa sumu na mlinzi wake liliishia wapi? Na nani alikuwa nyuma ya pazia katika sakata hilo?
 
Ni Mara 100% Kumpoteza Dr. Slaa Kuliko Kumkosa Eddo Lowassa,, Tuliona 2010 Uchaguzi Ulipofanyika Hata Dr. Slaa Mwenyewe Kaa

Mgombea Urais Kupitia CHADEMA, Hakujua idadi Kamili za Kura Alizopata;

Maana yake ni Kwamba Hata kama Dr. Slaa Angesimama Kama Mgombea Kwa Ticket ya UKAWA Uwezekano Wa Kupigwa Changa la Macho ni 100% Na Kubaki Kulialia tu.

Watanzania Tuna Hamu na Mabadiriko Na Tunaona Eddo Lowassa Ndio Tu anaweza Kuleta impact ya Kile Tunachokihitaji. Tunamtakia

Safari Njema Dr. Slaa Huko Aendako; Kwani yeye Ndiye alikuwa Anajiona Anaweza Kugombea urais tu Kwa ticket ya UKAWA?
 

bila SLAA? mjiandae kisaikolojia.
 
Hivi mtu unawezaje kupoteza mda mwingi kiasi hiki kuandika ujinga kama huu????
 
Huyu Dr. Slaa ninayemfahamu mimi kama shujaa asiye muoga kukemea viongozi waovu hadharani...
Shujaa aliyejitolea kuacha marupurupu ya ubunge ili ajenge chama kitakacholeta ukombozi nchini. Shujaa asiye na uwoga wa kukemea maovu jukwaani leo hii tunampa sifa ya uwoga, sifa ya kunguru mwoga akimbizaye bawa lake?? Kwamba anaogopa kusema hiki ambacho wengi ambao wamejivika usemaji wake wanakisema???? Kweli?

Jamani hebu tumpeni nafasi na pumzi kama kipo cha kusema atakuja kukisema hadharani. Tena kwa press conference sio kwa kunong'ona na waandishi wa gazeti moja tena la Raia Mwema.
 
km ni kweli kajiuzuru its good lkn ari ya kuifanya ccm kuwa chama pinzani bado ipo pale pale mioyoni mwa wanaharakati
 
.....

TO BE IGNORED /
NI MNAFIKI MKUBWA
MTU AWAYE YEYOTE ATAKAPOFANYA JITIHADA ZOZOTE ZA KUKATISHA SAFARI YA IKULU HAFAI HATA KIDOGO
NA SI MWENZETU TENA NI MBINAFSI
ii

..
 
Watu wasishambulie gazeti ,hilo ni dhahiri ni maneno yake mwenyewe Dr. Slaa..

Jenerali Ulimwengu hawezi kuruhusu magazeti yake yaandike uwongo .

CDM muda unaenda kwa kazi, anzeni kuzoea maisha bila Dr. Slaa


Nakushauri uweke akiba ya maneno...
 
Watu wasishambulie gazeti ,hilo ni dhahiri ni maneno yake mwenyewe Dr. Slaa..

Jenerali Ulimwengu hawezi kuruhusu magazeti yake yaandike uwongo .

CDM muda unaenda kwa kazi, anzeni kuzoea maisha bila Dr. Slaa

Naomba wamwache hivyo hivyo ndiyo maana kukawepo Naibu katibu hivi vyeo vinakaribia kulingana hakuna tabu chadema tupige kazi, inabidi ajifunze kwa Prof. lipumba ambaye alikuwa ngumu kubadilika sasa ameona mazingira kabadilika.

Safari nyingine tuweke sheria kwamba ukichaguliwa kuingia kwenye ulingo ukafeli basi uchie ngazi waingie wengine.
 
Wamuache tu mbona alidai wanataka kumuua kumbe kutafuta kick nani amuue yeye. Anaendeshwa na mke wake
Anaonyesha hafai kuwa rais
 

Unajitambua?
 

Kwa hili la Dr ishu sio Lowasa

Nadhani kuna ishu nyingine zaidi ya hii

Lazima kuna msukumo Mwingine...Narudia Lazima

Dr ni mtu makini anayejua kucheza karata zake kisiasa...Hata Hio List of shame anajua ilikua ni siasa waliyoicheza

Siku ya Jumapili baada ya Lowasa kupokelewa Dr Alikuwepo kikaoni

Kesho yake Jumatatu alipost Tweets za kuonesha ana support Na ana defend msimamo wa chama

What happened ni Ghafla Twitter account yake ikasemekana ilikuwa hacked...Na thread tuliiona humu

Baada ya thread kuwa hacked...Posts zake zikabadilika na kuanza kuponda Uamuzi wa UKAWA na CHADEMA

Swali la kujiuliza;NINI KILISABABISHA THAT SUDDEN CHANGE?

From that Day Dr Slaa hakujitokeza hadharani

Ninavyomfahamu Dr Slaa ni mtu wa kusimamia maamuzi ya Vikao halali vya chama...And that is what he was doing katika siku ya Jumatatu.

Ninashawishika sana...tena sana ...kuamini kuwa Dr Slaa kafika bei.......

Ninashawishika kwa sababu sioni sababu ya Msingi ya daktari kususia kiasi hiki

Kwa move ya Lowasa kuja CHADEMA na UKAWA kuwa moja....hicho kilikua kifo cha CCM

Kuna uwezekano System ilireact haraka na kumuwahi Dr Slaa......

Swali lingine la kujiuliza Dr Slaa yuko wapi? Yuko na nani? nani alimuona? Nani anamiliki mawasiliano yake kwa sasa?

Pamoja na hayo yote...Nauheshimu sana Mchango wa Dr Slaa hadi hapa tulipofika

Nenda salama BABA

Mchango wako utakumbukwa sana katika historia ya Tanzania

Sisi Vijana tumejifunza mengi kutoka kwako...Lakini hii ni Vita...Adui yetu ni CCM.....Wewe ulikua jemedari wetu wa vita...Ukipigwa risasi na kuanguka...Vijana tutaendeleza mapambano.

Unaweza kuwa hujui ni kiasi gani kuondoka kwako muda huu kunaahirisha kuondoka kwa CCM...

Kwa watu wenye uelewa mpana watapata shida sana ya kuelewa nini chanzo cha kususa kwako huku.

Ninavyokufahamu wewe sio mroho wa madaraka...Hukuwahi kuwa na Tamaa ya ikulu...Naamini kuna force behind you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…