Dr. Slaa: Natishwa


Barua kwa Dr. Slaa

Ninaomba upate dakika chache upitie hiki kibarua kifupi ili upate mioyo ya wapenzi wako chini ya chadema inavyopiga kutokana na sintofahamu iliyopo kuhusu shughuli zako katika chama chako cha CHADEMA.

Dr. Slaa, mimi pamoja na maelfu ya Watanzania waliopo ndani ya nchi na nje ya nchi tunafuatilia kinachoendelea kuhusu kutopatikana kwako katika kusukuma hili vuguvugu la mabadiliko.

Dr Slaa ninaomba upokee ujumbe mfupi kama ifuatavyo:

1. Hakuna siri wewe ni shujaa na mtenda haki ya kweli ktk siasa za hapa nchini.

2. Hakuna siri wewe ni mtetea haki ya kweli kwa watanzania walio sahauliwa.

3. Hakuna siri kuwa katika historia itakayo andikwa kuhusu kupigania mabadiliko ya watanzania jina lako litakuwa na nafasi ya pekee.

4. Hakuna siri kuwa kwa mtu yeyote awe kiongozi wako mkuu au wa chini yako hatatenda haki kama hatakuwa tayari kufahamu mchango wako katika mafanikio ya chama chenu.
5. Dr. Slaa yapo mengi MAZURI ya kuandika kuhusu WEWE.

Hitimisho:

Dr. Slaa kilio changu na cha wengi ni kuwa tunakuhitaji haraka sana katika team ya kampeni itakayo anza hivi karibuni. Wengi wetu tunajua kuwa hata pale historia itakapokuja kukujudge wewe na viongozi wenzanko, ikiwa ni hasi (negative) wewe hautakuwepo na ikiwa chanya (postive) basi wewe utakuwepo. Wengi wetu tunajua kinacho endelea na ndiyo maana uamzi wako wa kurudi kwenye meza moja na viongozi wenzako tutauchukulia kama ushindi kwako pamaoja na sisi. Tunakuomba ujitokeze na kuwapa matumaini watanzania ambao sasa hivi mioyo yao haina utulivu.

Mhs Mbowe angalia kuwa kwa gharama yoyote ile inabidi Dr Slaa awe katika team ya USHINDI.

Kwa wale watoa matusi mnaruhusiwa hata hivyo ujumbe umefika
 
Chama kikuu cha upinzani Tanzania hakina access na katibu wake mkuu na wala hakionyeshi jitihada za kujua aliko kiko busy na Yule kiliemuita fisadi for years!
Mkuu ukiona hivo ujue ipo sababu, hawawezi tu kuwa kimya wakati wanajua kabisa mtu wao muhimu; Think Bigger!!!
 
Mkuu ukiona hivo ujue ipo sababu, hawawezi tu kuwa kimya wakati wanajua kabisa mtu wao muhimu; Think Bigger!!!

ungeweka akiba ya maneno,sasa si umemsikia mwenyekiti wake?tatizo mnajribu kufikiria kwa niaba ya mbowe,hamjui kinachoendelea kwenye chama chenu otherwise msingekua mnaropoka,mambo mengi chamani mbowe anayaendesha kwa fikra zake ndio mana huwa hamuelewi kesho kutatokea nini,mbowe mwanzo si aliwaaminisha picha ya lowassa akiwa kwenye kikao cha chadema ni fotoshop?mkamuamini mkaja hapa kuwa kasuku wake wa kudaka kila analoropoka,tukawaambia yule pichani ni lowassa na pale alipo ni kwenye mkutano wa ndani wa chadema,hamkuweka akiba ya maneno mkatushambulia kwa maneno makali na vitimbi vya kila aina,baadae ilipokuja kuonekana mbowe alikuwa kawapiga chenga msijue mkakubali kuinamisha vichwa kama mbuzi wake wa kafara ajichinjie.Hii ya slaa pia the same story ya jinsi mbowe anavyocheza na akili zenu,mwanzoni alisemaje,akaja kusemaje na kamalizia kusemaje kuhusu slaa????Hamna cha kumfanya zaidi ya kula matapishi yenu huku mkiyatia ndimu nyiiingi na chumvi!
 
Chadema A.k.a. team lowassa kulishambulia gazeti ni sawasawa na kukishambulia kioo kwa mateke kisa kinaionesha taswira yako ulivyo,mtakivunja kioo bure hakina kosa,hivyo ndivyo hali halisi ilivyo na slaa ndio aliyasema hayo,mngejikita kuendelea kumshambulia yeye na mke wake kuwa ndio tatizo sio kioo(gazeti wala mwandishi)
 
Tunamhitaji Dr SLAA ni kamanda kweli kweli ukimaliza mapumziko njoo tuing'oe ccm.mchango wako ni muhimu sana kamanda.usituangushe watanzania.
 
Mh Mbowe amesema, ametumia kila njia kumshauri na pia kutumia kila njia kumshawishi Dk Slaa lakini wameshindwa.

Chanzo: Uhuru
 
Kati ya vitu ambavyo cdm wameharbu basi ni kumtwaa lowasa na kumsimamisha mhuni lowasa kugombea nafasi nyeti. nilidhani atakaribishwa na kupewa uanachama ili apate uzoefu na itikadi ya chama.
sasa lowasa hata gwanda hajaanza kuvaa na hatovaa
 
Tatizo Mbowe anajifanya anajua kila kitu.
 
Dr.,Slaa ameona ukombozi wa nchi unakaribia anajidai kususa,, Huyu ni kibaraka wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…