Dr. Slaa: Natishwa

Akijitoa basi Gwajima ni nabii!! Alisema Slaa ni Musa na Lowassa ni Joshua.
 


Ukimchukua Malaika Leo ukamshusha CCM.
Baada ya Mwezi tu anakuwa Ibilisi.

Freeman Aikaeli Mbowe
 

Makongoro nawe ni mnafiki mkubwa na ndio maana ukashindwa kura za maoni ccm na huku ukimkaribisha Slaa ccm. Kwa unafiki wako huo jana tu umetoka ccm na kujiunga chadema huyo Slaa ulikuwa na nia gani kwake kumkaribisha ccm?
 
Hizo nukuu sisi tutajuaje kama ni za kweli? Tumuone live kwenye TV, akiyasema hayo.
 
ukifanywa!! Utafanywa vilevile pole slaaa;
 
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Ajigambe kila fani, kwamba ameisaini,
Mtimilifu moyoni, hana ila asilani,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Naulizia sioni, hapa kote duniani,
Mbona mwainama chini, na kupooza machoni,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Sioni mwema jamani, tukipima kwa makini,
Wote tuna walakini, japo wa ndani kwa ndani,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Mtu asiyetamani, cha ndugu wala jirani,
Mwenye pendo kwa fulani, bila kuchagua dini,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Aso mkaidi nani, mtiifu namba wani,
Mkunjufu wa usoni, aso chuki nafsini,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Hana doa fikirani, ni timamu matendoni,
Mchapakazi saini, mwenye mipango mwanani,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Shujaa huko vitani, jemadari wa nishani,
Mfalme wa amani, pote pote duniani,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Asiyekosa siini, kwa Mola na duniani,
Aliyejaa imani, upendo nayo hisani,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.

Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Moja moja abaini, alofanya bila soni,
Lisilo na walakini, dosari wala huzuni,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.

Nani mwema duniani, ajitoe hadharani,
Asiye mteti nani, mroho na mshindani,
Ukweli bila utani, simuoni duniani,
Nani mwema duniani, ajitoe hadharani.
 
HAHAAAAAAAAAAA lakini pia zingatia hii:

wananchi wa kijiji cha jirani
midomo yao na matako yao hayatofautiani
awezaye kutambua kama wanakijiji hawa wanasema au wanajamba ni nani
pengine ni wanasayansi wa hali ya juu na wenye maarifa mengi
wanaweza kutofautisha kama akina fulani wanasema ua wanajamba
maana harufu za midomo na matako yao zafanana
 
Tuwe waungwana japo kidogo....Dr.Slaa alistahili kugombea Urais hata kama LOWASA kajiunga na CHADEMA,kwanza bado mgeni katka chama chenu hata wiki hajamaliza.
Sidhani kama Dr.Slaa ni mjinga kiasi hicho asijuwe hila zilizotumika kumuengua?

Hiyo ni laana mbaya sana....naamini Dr.Slaa angeleta upinzani wa kweli katika uchaguzi huu,lakini sasa hivi CCM inasubiri kuapishwa kwa Dr.JP Magufuri mapema kabla hata ya jua kuzama.


Mwenye picha ya Mchumba wa Dr.Slaa akiwa amepata majeraha katika fujo zakutengenezwa na M4C aiweke hapa tuweze kuwaombea uvumilivu katika janga hili.....

Honestly,nampenda Dr.Slaa kwa ushupavu wake hata kama CCM tulikuwa tunampa changamoto ni kwa itikadi tu...but he deserve to be respected forever !

Kura za maoni zilituondolea hazina ya taifa,lakini anaweza kurudi japo tumpe ubalozi kule CANADA apumzike na mchumba wake
 
Prof.Lipumba kila siku jela na kuvunjwa mikono kwa maslahi ya watanzania mbona hajang'ang'ania urais?
 
KUNA KAULI ISEMAYO USITUKANE WAKUNGA NA UZAZI UNGALIPO.
DK alikua mstari wa mbele kumtuhumu ZITO kwamba anatamaa yamadaraka
je DK unakumbuka ya ZITO ?
ama kweli mkuki kwa nguruwe. utendavo ndivo utendewavo.
 
Hivi ni lini hasa Josephine ataanza kuitwa Mrs Slaa badala ya mchumba wa Slaa? Maccm hata kama hammpendi Slaa ifikie hatua dhihaka ya namna hii mnaacha.
 

Kati ya waji.nga we ni moja wao.... kama hiyo ndio hoja basi apewe Makaidi....
 
Mkuu...Dk wamemuonea sana...wamemkatalia kuchukua form alafu wanasema kesho wanaenda kukaa kikao cha kupitisha mgombea mmoja..amakweli hiki ni chama cha demoghasia na malumbano
 

Attachments

  • 1438618842425.jpg
    34.5 KB · Views: 361
Na bado zito yupo juu na october anarudi mjengoni sasa babu ???????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…