Dr. Slaa aliondoka na akili zote CHADEMA, chama kimebaki gulio!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,582
2,000
Msigwa alipokuwa akisema "akili ndogo haiwezi kuongoza akili kubwa" hakujua kuwa katika Chadema akili kubwa ilikuwa ni ya Dr.Slaa.Nasema hakujua sababu hakuwa chochote ndani ya chama zaidi ya mbunge.Sasa ni mmoja wa viongozi wakuu,naam ni mkuu wa kanda ya Nyasa,ni kigogo japo kwa mbeleko ya Mbowe na Lowassa.

Kuna sinema zinatokea chadema kwa sasa na badala ya watu kuja na hoja jadidi vinaibuka vikundi ndani ya chama kutengeneza fulana na kuuza.Kikundi cha UGT kikiongozwa na Malisa ndicho kinaratibu utapeli huu angali kikijua "kupotea" kwa Ben ni maigizo yaani "Ben Kajiteka".Wao wamefanya gulio!.

Kuna gulio la nafasi za uongozi ndani ya chama,ati siku hizi kwa mujibu wa Mbowe "nafasi moja ikigombewa na watu wawili italeta mgogoro ndani ya chama" hivyo mwenyekiti anaangalia nani ana uwezo wa kifedha kati ya wagombea kisha anashindanishwa na kivuli.Gulio la uongozi.

Siku hizi kila mwezi mwenyekiti anakuja na operesheni mpya lengo kubwa ni kuhalalisha matumizi ya ruzuku.Alianza na ukuta baadaye ukuta remix mwisho tukaambiwa ukuta upo moyoni sasa mbona mamilioni yametumika? Kisha akaja na kata funua na sasa kata funua remix hatuoni chochote japo matumizi ni makubwa.Gulio la operesheni na matumizi.

Kuna hili la kujiteka,alianza "Jasusi" na sasa "mwanaharakati" kutoka afisi ya mkuu.Gulio la kujiteka.Gulio la kujiteka.

Hakika akili ya CHADEMA aliondoka nayo Dr.Slaa na sasa tumebaki na gulio.
 

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,640
2,000
Kama brain ya CDM ni Mbowe, basi wajue imekula kwao!
Bado wapo wenye maono, lakini hawapewi nafasi
Kuingia kwa Chief the big Laigwanani imekuwa msumari wa mwisho kwenye coffin. Akina Mnyika wameyeyuka ghafla
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom