Dr Molel azidi kuipasua CCM jimbo la Siha

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Katika kile kilichotarajiwa na wengi kama ndio mshahara wa usaliti ndicho kinacho mkuta Dr Molel kwa wananchi wa Siha,hali imezidi kuwa mbaya kwa mgombea Ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Dr Godwin Molel.

Ndugu yangu jana huyu mpuuzi (Dr Moleli) amewatukana sana watu wanaojitolea nguvu na muda wao kumuombea kura za nyumba kwa nyumba kwa madai hawaombi kura zake bali wanaomba kura za mgombea wa CHADEMA,(Elvis Christopher Mosi) anasema mnyetishaji wetu.

Katika kikao hicho kilichofanyika ofisi ya Wilaya ya Ccm hali ilikuwa mbaya zaidi kiasi ambacho viongozi kadhaa walifukuzwa kwenye kikao cha ndani kwa barua kwa madai kwamba wanatoa siri za chama nje kwa viongozi wa CHADEMA.

"Ndugu yangu yani jana ilikuwa balaa tupu, hadi mwenezi wetu alishikwa na tumbo la kuharisha kwa presha ya kuhisiwa nayeye ni mmoja watoa siri za chama" anasema mtoa taarifa.

Anasema kama hali itaendelea kuwa hivi sidhani kama chama kitabaki salama hapa Siha, viongozi wanaotaka kuvuliwa uanachama (majina nayahifadhi) katika kikao kijacho wameshapewa barua wanaushawishi mkubwa sana hasa kwa vijana lakini wameapa kutompigia kura Dr Moleli wao na wafuasi wao wote hivyo hakuna njia ya kumsaidia Moleli kushinda labda waibe kura Molel hauziki na haeleweki hata kidogo.

Mtoa taarifa kwa kuonesha umahiri wake katika fani ya ushushu amenikabidhi barua na majina ya wanaotarajiwa kufukuzwa na walioteuliwa kuja kushiriki kampeni Siha muda wote nitaziachilia hewani.

"Kaka barua zote hizi hapa na jana wametuletea magari 6 na kuna vijana wapo na Noah nyeusi na Rav4 ya kijani namba (zimehifadhiwa) ila kunavijana wengi sana wa nakuja kutoka Arusha ambao walipelekwa Dodoma kwa mafunzo maalumu ya vurugu na kuiba kura nitakupatia majina yao na mahali watakapo pangiwa, mimi siwezi kuwa sehemu ya laana ya Dr Moleli kwa watu wa siha " anasema mtoa taarifa.

Moleli hawezi kututukana sisi kwenye vikao aliondoka CCM akatuacha, leo anarudi tena halafu anapewa nafasi agombee ubunge wakati kunawatu huku wanasifa kuliko zake,huyu ni msaliti haaminiki tena ndio maana hawakuruhusu kura za maoni sasa tutawaonesha kuwa hiki chama sio cha mtu mmoja we subiri tu" anasema mtoa taarifa wetu.

Nikiripoti kutoka Jimbo la Siha

Mwakilishi

Back
Top Bottom