Dr. John aliwahi 'kuwachana' UHAMIAJI

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,435
8,886
Washkaji zangu wawili wa maskani wanafuatilia kupata passport ili wajichanganye bondeni kwa Madiba kwenda 'kuchukua maisha'. Leo wakadondosha apdeiti maskani kuwa ni mwezi mzima sasa wanazebezwa tu na kupigwa kabobo nyepesi. Ghafula nikakumbuka 'pini' murua kabisa kutoka kwa Dr John iitwayo 'Uhamiaji', track ambayo aliipika na kui-release karibia miaka 7 iliyopita lakini hadi leo hii maudhui ya wimbo huo bado yanaakisi kabisa UHAMIAJI ya leo.

Na mara nyingi sana huwa najiuliza bila kupata majibu, WHY nyimbo 'kuntu' kama hizi huwa hazipati airtime kwenye mainstream? Ni ngoma tamu sana. Msikilize Dr John...

Ubora wa picha sio kiviile. Audio is hereby attached as well. Long live Dr. John, long live Wagosi wa Kaya a.k.a wazee wa Tanga-kunani. Huwa naenjoy sana ladha za wakongwe hawa since back in ze dei nikiwa chalii.

HIP-HOP... The good music I like most.

-Kaveli-
 
Attachments

  • Dr John Ft Mr Ebbo - Uhamiaji..mp3
    4.2 MB · Views: 57
Wamedondosha nyingine (WAGOSI) inaitwa UPEPO SIO

'Upepo Sio' nimeshaiona mkuu. Aisee ni bonge la pini. Wagosi ni mafundi.

''... siku hizi watu wanarudi nyumbani mapeeeema na kukagua daftari za watoto. Vimada wangu wote siku hizi wakinibeep sipigi. Upepo sio...''. hahahaa hatareee

-Kaveli-
 
Nafikiri Roma aliwapenda sana hawa jamaa na akataka afuate msimamo wao wa kuikosoa serikali. So sad serikali imemuwahi Roma. Wagosi watabaki kuwa wakosoaji pekee wa serikali wasio yumbishwa na upepo wa kisiasa
 
Nakubaliana nawe mkuu. Wagosi ndo wasanii pekee waliobakia kuikosoa serikali kupitia sanaa. Na ni kama wapo 'makini' fulani hivi katika uwasilishaji wao wa sanaa. Huwa wapo 'non-alignment' kwenye mambo ya kisiasa, nadhani hii pia imewasaidia sana kwenye music mileage yao. Japo waliwahi kufungiwa ule wimbo wao uitwao 'Wauguzi'.

Ukisikiliza nyimbo zao kama: Lidandasi, Tanga Kunani, Umeme & Maji, Walimu, Wauguzi, Soka la Bongo, Traffic, Nyeti, n.k zinakumbusha mbali sana.

Roma yeye amekuwa 'too vocal' ... nadhani hii imechangia sana kuonekana 'anaizingua' serekali.

-Kaveli-
 
Nakubaliana nawe mkuu. Wagosi ndo wasanii pekee waliobakia kuikosoa serikali kupitia sanaa. Na ni kama wapo 'makini' fulani hivi katika uwasilishaji wao wa sanaa. Huwa wapo 'non-alignment' kwenye mambo ya kisiasa, nadhani hii pia imewasaidia sana kwenye music mileage yao. Japo waliwahi kufungiwa ule wimbo wao uitwao 'Wauguzi'.

Ukisikiliza nyimbo zao kama: Lidandasi, Umeme & Maji, Waugusi, Soka la Bongo, Nyeti, n.k zinakumbusha mbali sana.

Roma yeye amekuwa 'too vocal' ... hii imechangia sana kuonekana 'anaizingua' serekali.

-Kaveli-
Hakika, kuna kipindi nyimbo zao zilipendwa sana japo tulizichukulia upande wa comedy jinsi walivyo act (traffic hao ngoja tijaribu kama tutapita) lakini kiuhalisia traffic ndio wanatutesa barabarani. Je, kuna funzo lolote tulilipata kutokana na wimbo huo au tulifurahia tu jinsi walivyo jazana kwenye buti? Mungu awape uhai waendelee kuwapigania wanyonge kupitia nyimbo zao
 
Washkaji zangu wawili wa maskani wanafuatilia kupata passport ili wajichanganye bondeni kwa Madiba kwenda 'kuchukua maisha'. Leo wakadondosha apdeiti maskani kuwa ni mwezi mzima sasa wanazebezwa tu na kupigwa kabobo nyepesi. Ghafula nikakumbuka 'pini' murua kabisa kutoka kwa Dr John iitwayo 'Uhamiaji', track ambayo aliipika na kui-release karibia miaka 7 iliyopita lakini hadi leo hii maudhui ya wimbo huo bado yanaakisi kabisa UHAMIAJI ya leo.

Na mara nyingi sana huwa najiuliza bila kupata majibu, WHY nyimbo 'kuntu' kama hizi huwa hazipati airtime kwenye mainstream? Ni ngoma tamu sana. Msikilize Dr John...

Ubora wa picha sio kiviile. Audio is hereby attached as well. Long live Dr. John, long live Wagosi wa Kaya a.k.a wazee wa Tanga-kunani. Huwa naenjoy sana ladha za wakongwe hawa since back in ze dei nikiwa chalii.

HIP-HOP... The good music I like most.

-Kaveli-

Huyu jamaa ana kipaji sana inasikitisha umri unaenda na hajafaidika na ubunifu wake wa kazi..walikua wanahojiwa kwenye mkasi jamaa ni kama wamepoteza muelekeo kbs hawajui hata wafanye nini..inasikitisha!
 
Hakika, kuna kipindi nyimbo zao zilipendwa sana japo tulizichukulia upande wa comedy jinsi walivyo act (traffic hao ngoja tijaribu kama tutapita) lakini kiuhalisia traffic ndio wanatutesa barabarani. Je, kuna funzo lolote tulilipata kutokana na wimbo huo au tulifurahia tu jinsi walivyo jazana kwenye buti? Mungu awape uhai waendelee kuwapigania wanyonge kupitia nyimbo zao

'Traffic' ni wimbo ambao uliakisi uhalisia kwa % zote. Wimbo huo unaishi hadi leo.
Mi nadhani jamii ilijifunza kitu kwenye wimbo ule, japo watu wengi waliuchukulia kama comedy baada ya video yake kuonekana.
Wagosi ni mafundi, ila media inawabania sana. Huwa nikisikiliza 'Wauguzi' nastuck on 'replay'.

-Kaveli-
 
Huyu jamaa ana kipaji sana inasikitisha umri unaenda na hajafaidika na ubunifu wake wa kazi..walikua wanahojiwa kwenye mkasi jamaa ni kama wamepoteza muelekeo kbs hawajui hata wafanye nini..inasikitisha!

Kuna media fulani kujifanya ndiyo 'mastermind' wenye master plan ya industry nzima.
Kweli Dr John sasa umri unaenda na hajafaidi matunda ya kipaji chake. Na kuna track yake inaitwa 'Siwezi' kazungumzia masuala haya.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom