Dr. Che-Mpinda Katika Mapambano Dhidi ya Ubaguzi Marekani Miaka ya Sitini

PastorPetro

Senior Member
Feb 25, 2008
189
35
Nimevutiwa na hii habari iliyo kwenye Swahili Time Blog. sikuwa na habari kabisa kuwa hata watu wa ubalozini walikuwa wananyanyaswa.

Ni kweli huyo dada anavyosema kuwa sisi tumesahau shida waliopata waafrika Marekani. Mfano, marehemu Prof. Biswalo aliwahi kuniambia kuwa alikuwa anatembea barabarani Indiana hamsumbui mtu, mzungu kamfuata na kumtemea mate usoni.

Mzee mwingine aliwahi kuniambia aliwekwa ndani Marekani, North Carolina, siku tatu kwa vile mweusi alidaiwa kumwaimbia binti wa kizungu. Alipokamatwa mhalifu wa ukweli mbona jamaa alikuwa mweupe sana zaidi yake!
 
Back
Top Bottom