DP World kumekucha Tanzania

Motowntzjpm

Senior Member
Joined
Jun 16, 2023
Posts
134
Reaction score
209
DEEPEE WELDI - Kumekucha Tanzania

Sakata la mkataba/makubaliano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu DP World – Kumekucha Tanzania.

Wanaosapoti;
  • Lugha za kebehi na dharau
  • Uzalendo ni kukubaliana na serikali yetu
  • Vitisho
  • Mnaopinga mmenunuliwa
  • Hamjui mlifanyalo
  • Wanawashangaa wakosoaji iweje hamuoni mafanikio
  • Kukimbilia kwenye hoja za kuchongea wanakosoa kwa kuligawa taifa
  • Mnadirikije kupinga uwekezaji wenye manufaa kwa taifa
Kinachowaponza;
  • Wanadai ni makubaliano na sio mkataba akati ukifuata katiba kilichopitishwa ni mkataba kinachosubiriwa ni kutungwa sharia ya utekelezaji
  • Kutumia watu ambao hawana uwezo wa kujadili hoja kina Zembwela, Steve Nyerere
  • Matumizi ya waandishi makanjanja
  • Wanapotumia wazoefu mfano mwenyekiti wa TEF hawajikiti kwenye hoja
Wanaopinga;
  • Wanasema - hatupingi uwekezaji
  • Tunapinga mkataba ovyo
  • Hatuna chuki na Rais
  • Hatupingi Muungano ila ikiwa manufaa ya taifa iweje bandari za Zanzibar hazihusiki
  • Huu ni mkataba kawa mujibu wa sharia zetu
  • Wapo tayari kukabiliana ndani nan je ya Bunge
  • Askofu Bagonza, Peter Madeleka na wengine wanaopinga wamejikita kwenye hoja
Mwananchi wa kawaida anachohitaji kufahamu;
  • Mwananchi ndio mwenye nchi, watatwala wamekasimiwa madaraka
  • Taifa linalotofautiana kwa hoja linakuwa
  • Hatimae tumeanza kutambua kwamba mjadala wa maendeleo yetu sio mali ya mtu taasisi wala tabaka ni yetu sote
  • Kilichosababisha machafuko nchi za wenzetu ni ubabe
  • Uwekezaji wa nje haukwepeki lakini na sisi sharti tubadilike ili Utanzania usiwe chaka cha upigaji
 
Hivi mikataba imefutiliwa au huu tu
Kauli hiii nalo inatumika kama utetezi . Jibu ni kwamba Tanzania tumepigwa kupitia mikataba mingi ya ovyo kisa serikali na wenye madaraka wakishasema tunatarajiwa kupokea bila kuhoji. Umeme , Nbc ni mifano tu.

Hii ndiyo mara ya kwanza mkataba kuvuja kabla athari zake kuanza kulitafuna taifa
 

Paskali kama nauona wito wako hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…