Dotto Bulendu: Lowassa, individual responsibility na personal branding

The Bourne

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
1,077
Reaction score
1,322
Lowasa,"individual responsibility" na "personal branding"

Na Dotto Emmanuel Bulendu

Edward Lowasa anaweza kuwa miongoni mwa wana siasa wa aina yake ama ana watu wa mkakati wenye mbinu kali sana hasa linapokuja suala la kujenga "brand" yake.

Kwa nini nasema hivyo?

Lowasa wakati akiwa CCM,alituhumiwa sana na upande wa upinzani(Chadema),kwamba ni fisadi,jamii ilikuwa ikimuona Lowasa kilichokuwa kinakuja mbele ni tuhuma ya ufisadi.

Lowasa hakuwahi chukua hatua zozote dhidi ya wanaomtuhumu,alikaa kimya na kujijengandani ya chama ili atimize ndoto zake,Lowasa alipokatwa ndani ya CCM aliamua kwenda kwenye chama kilichomtuhumu kuwa ni fisadi na akapewa nafasi ya kugombea Urais,kuhama kwake kulitengenza siasa ngumu na zenye ushindani kwenye uchaguzi wa 2015.

Chadema iliyomtuhumu wakati akiwa CCM ilipata wakati mgumu yenyewe na washirika wa UKAWA kumkingia kifua ili akubalike mbele ya wapiga kura,CCM walizunguka nchi nzima wakimrushia Lowasa Makombora ya kila aina,walijitokeza kwenye vyombo vya habari wakimtumia Dr Mwakyembe,Humphrey Polepole kuambia umma kuwa Lowasa ndiyo mwenye Richmond na hii ni baada ya Chadema kubadili upepo na kusema anayemjua mwenye Richmond ni Kikwete!.

Nakumbuka Polepole alionekana mara kwa
mara kwenye TV akichambua kwa kina kwa nini Lowasa hapaswi kuchaguliwa kuwa Rais,nakumbuka hoja ilikuwa,ukituhumiwa tu,huna sifa tena.

Rais mstaafu Kikwete alipigilia msumali wa mwisho October 23.2015 baada ya kumbebesha mzigo wa Richmond Lowasa katika uwanja wa CCM Kirumba wakati akifunga kampeni.

Chadema wamekuwa wakipigwa kombora kuwa baada ya Lowasa kuhamia kwao ajenda ya ufisadi imekwisha.

Lowasa kama alivyocheza kwa kuwalazimu Chadema wamnadi pamoja na kuwa waliwahi mtuhumu,wiki iliyopita akatinga Ikulu!.

Kama kawaida kwa ufundi mbinu ya kumfanya mtu akujenge na wewe,Lowasa alipoona
camera na vinasa sauti hakufanya kosa,akampongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi kwamba ni mtu safi na aungwe mkono,mwenyekiti na Rais nae alipopewa Camera na kinasa sauti,akaingia kule anapopataka sana Lowasa,akamsafisha Lowasa kwa kusema maneno yaliyojenga "positive brand" ya lowasa!

Mwenyekiti wa chama na Rais wa nchi akasema,Lowasa ni mwanasiasa safi kiongozi aliyefanya mazuri na anatakiwa kuenziwa,sasa kama mwenyekiti wa chama kashasema Lowasa ni mtu safi na anayetakiwa kuenziwa,hapo nani ndani ya chama wakumsakama Lowasa huko mbeleni?

Kama wafuasi wa CCM wanavyosema," Kama lowasa kampongeza Magufuli,wewe unayepinga ni nani?" basi na wafuasi wa Lowasa naamini nao washapata hoja dhidi ya CCM ambayo nadhani wanasema,"Kama mwenyekiti wa Chama chako(CCM),Rais wa nchi na mwenye vyombo vya uchunguzi kasema Lowasa ni mtu safi na aenziwe,wewe nani umseme mabaya" hapa ngoma droo hapa.

Lowasa katumia mbinu kali sana,kishasafishwa na pande zote zilizopata msukumia makombora,Huyu ndiyo Lowasa anayejua kucheza na siasa za kumjenga!.

Tatizo la Lowasa ni nini?

Lowasa anaonekana mikakati yake mingi ni yakumjenga yeye zaidi na si taasisi,Lowasa alipokuwa CCM alizunguka nchi nzima,alitoa misaada mpaka kwenye nyumba za ibada,alizitoa kama Lowasa na si CCM,kila alichofanya alihakikisha kinamjenga yeye na siyo taasisi(CCM).

Ndiyo maana CCM walipokuja kushtuka,mtandao wa Lowasa ulikuwa umesambaa nchi nzima kuliko kada yeyote wa CCM aliyechukua fomu ya kuwania Urais.

Akiwa Chadema,Lowasa akaamua kwenda kumuona Rais Magufuli kama yeye na si taasisi aliyo chini yake(Chadema),na ndiyo maana kilichosemwa ni "Lowasa akutana na Magufuli" na siyo "Chadema wakutana na Magufuli"

Lowasa nadhani na wataalam wake wa "branding" siku zote wamewekeza katika kumjenga zaidi yeye na si taasis,ndiyo maana aliamua kwenda Ikulu bila hata kuwataarifu viongozi wa juu wa chama chake!.

Yawezekana kikao cha Lowasa na Rais Magufuli kikawa mwanzo wa siasa mpya za Tanzania,kwani si jambo baya,hata hali ya kisiasa ilivyokuwa mbaya visiwani Zanzibar,Rais Karume alilazimika kukutana na Maalim Seif ili kusaka suluhu!.

Vikao vyao viliizaa Zanzibar mpya,tofauti ya Maalim na Lowasa,Maalim alikuwa anakwenda kama taasisi(CUF),,wakati Lowasa alikwenda kama Lowasa ,kama kuna jambo lolote jema litajitokeza kutokana na kikao cha Lowasa na Rais Magufuli hiyo itakuwa turufu kwa Lowasa kwani ni aina ya siasa zake za kujijenga zaidi ili aache alama yeye kama yeye!.

Chadema ya akina Slaa waliwahi kuingia kwenye mvutano na Serikali ya Kikwete,lakini walikwenda kama taasisi na Slaa hakuwahi kwenda peke yake tena kimya kimya,walikuwa wana jenga "brand" ya taasis(Chadema) na siyo mtu mmoja.

Binafsi wapinzani kwenda kumuona Rais na kujadiliana nae kuhusu hali ya kisiasa pale wanapoona mambo hayaendi sawa naliunga mkono,ni vizuri tukajenga utamaduni wa kusaka muafaka mapema badala ya kusubiri minyukano!.

Kosa la Lowasa

Kosa la Lowasa ni la kiutawala,alifanya kosa kuiweka mfukoni ajenda yake ya kukutana na Rais,katika usiri huo huo angewashirikisha hata viongozi wakuu wakawa na taarifa!.

Hii ingeonesha ndani ya chama chao kuna uwajibikaji wa pamoja,na hata makombora haya yanayomfuata yasingeenda kwake,yangeenda kwa taasisi,uwajibikaji wa binafsi(Individual responsibility) una faida na hasara zake,jambo likifanikiwa utapata heshima,likigoma utaonekana hufai na heshima yako huporomoka.

Lowasa alikuwa anajua kabisa,ajenda ya chama chake kwa sasa,anajua haijapita hata wiki moja mwanasheria wa mkuu wa chama chake(Tundu Lissu)? aliituhumu serikali huku nyuma yake akiwa amezungukwa na viongozi wakuu wa chama chake,ile ilikuwa ni ishara kuwa Lissu alikuwa anaongea kwa niaba ya chama,Lowasa kwenda Ikulu Kimya kimya ni kuonesha hakubaliani na aliyosema Lisu Nairobi.

Hivyo ni pigo kwa ustawi wa chama,inaonesha kuna udhaifu fulani ndani ya chama chao,pia labda Lowasa angevuta muda kidogo ili kuukwepa huu mgongano wa msimamo wa chama chake na wake binafsi!ame "spin" bila kujua msimamo wa chama chake alioutoa Lissu Nairobi kabla hajaenda Ubelgiji!.

Naweza sema,Kurungenzi ya mawasialino Ikulu katika hili imeonesha jinsi ilivyo viwa kwenye PR na Propaganda,wanajua namna na kujenga taswira chanya ya Rais na Ikulu!.Wangenyofoa baadhi ya maneno aliyosema Rais kuhusu Lowasa wangepata alama zaidi na zaidi,naamini wasaidizi binafsi wa Losawa wamefurahia kupata sehemu ya Rais alivyomzungumzia Lowasa,kwao ni turufu!.

Wasalaam
 
Uchambuzi mzuri
 
Back
Top Bottom