Doto Mashaka Biteko, waziri msahaulifu

Ability JM

Member
Joined
May 10, 2019
Posts
5
Reaction score
4
Ni waziri mwenye uwezo wa kujenga hoja lakini za uongo,Mara nyingi nimekuwa mfuatiliaji wa mienendo ya waziri huyu,amekuwa akihaidi Sana bila utekelezaji,amekuwa msemaji Sana bila utekelezaji,amekuwa akihaidi bila utekelezaji

Ninayasema hayo bila uoga na bila hiyana,waziri huyu wa madini amefanya ziara nyingi Sana pahala palipo na migodi haswa migodi inayochimba madini ya Vito.

waziri amekuwa mhubiri injili asiyeeleweka aslani,akiwa katika mgodi wa North Mara Gold mine,waziri aliwaagiza Watu wa Mgodi huo kuheshim mikataba na sheria za nchi vinginevyo hatua Kali zingechukiliwa dhidi ya kile kinachoitwa DHARAU YA MGODI KWA SERIKALI

MGODI wa North Mara unaochimba huko Mara umekuwa ukilalamikiwa Sana na wananchi wanaoishi pembezoni mwa mgodi huo,waziri Doto Mara kadhaa amesikika akiwatupia lawama North Mara pasipo kuchukuwa hatua
mara kadhaa waziri analaumu bila kuchukuwa hatua.

Waziri wa madini anapaswa kulinda kinywa na sio kusema na kuhaidi asivyoweza kutekeleza,waziri anahaidi hatekelezi

Mwisho nimushauri waziri kusimamia ukweli kuliko kudanganya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…