Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,490
I. Utangulizi
Salaam Profesa Kitila Mkumbo na Timu yako. Nimepekua kitabu cha "Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050" kilichozinduliwa Jijini Dodoma, tarehe 15 Julai 2025 (Kiambatanisho A).
Uzinduzi wake unahitimisha utekelezaji wa Dira ya Tanzania 2025 iliyoanza kutekelezwa mwaka 2000.
Baada ya kuisoma nimeona mazuri, mabaya na mapengo. Hatimaye nimejiuliza swali:
Hivi majirani zetu wa Zanzibar, Jamaica, Rwanda, Nigeria na Papua New Guinea wana nini hadi waweze kuonyesha mtiririko wa maoteo ya kitakwimu, katika ngazi ya kisekta na kitaifa, kwenye dira zao kuelekea miaka ya 2050, na sisi Tanzania tunakosa nini, hadi tufeli kiasi hiki tangu 2005 hadi 2025?
Katikati ya mshangao huu, nakuandikia kukufahamisha mazuri, mabaya na mapendekezo kuhusiana na Dira 2050 iliyozinduliwa.
Nitafanya hivyo katika maeneo yafuatayo:
- Mazingira ya kihistoria yanayoizunguka Dira 2050
- Muhtasari wa muundo na taarifa za kibibliografia
- Muhtasari wa maudhui yanayohusiana na malengo katika maeneo ya kimkakati
- Muhtasari wa maudhui yanayohusiana na matarajio ya kisekta
- Mazuri katika Dira 2050
- Mabaya ya kimuundo katika Dira 2050
- Mabaya ya kimaudhui katika Dira 2050
- Ukosefu wa uchambuzi na usanisi wa NUFU
- Ukosefu wa nadharia ya mabadiliko kwa kila sekta
- Ukosefu wa vigezo vigezo na shabaha za kuwezesha ufuatiliaji na utathmini wa kazi
- Utamaduni wa makosa haya kujirudia kwa miaka 20 mfululizo
- Hitimisho na mapendekezo
- Viambatanisho muhimu
Tangu Tanzania tupate uhuru tumeandaa na kutekeleza mipango 14 ya Maendeleo ya muda mfupi. Mipango hiyi ni kma ifuatavyo:
- Mpango wa kwanza wa miaka mitatu wa maendeleo baada ya uhuru (1962-1964);
- Mpango wa kwanza wa maendeleo ya miaka mitano (1964-1969);
- Mpango wa Pili wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wa miaka mitano (1969-1974);
- Mpango wa tatu wa maendeleo kiuchumi na kijamii wa miaka mitano (1975–1979).
- Programu ya Taifa ya Kunusuru Uchumi (NESP) (1980–1982);
- Programu ya Taifa ya Marekebisho ya Uchumi (SAP) (1983–1985);
- Mpango wa Kwanza wa miaka 3 wa Kufufua Uchumi (ERP I) (1986–1988);
- Mpango wa Pili wa Kufufua uchumi (ERP II au ESAP) (1989–1992);
- Mipango ya Miaka Mitatu Mitatu Inayopokezana na Bajeti ya Maoteo (RPFB) (1993–2012).
- Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP I) (2011–2015);
- Mpango wa Pili waTaifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II) (2016–2020); na Mpango ya Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) (2021–2025).
FYDP I, FYDP II na FYDP III ilikuwa ni mipango ya muda mfupi wa miaka mitano mitano kwa ajili ya kutekeleza mpango wa muda mrefu wa miaka 25, yaani Dira 2025. Hata hivyo, andiko la Dira 2025 lilikuwa na dosari ya ukosefu wa maoteo ya shabaha za kitakwimu kuhusu utendaji wa kisekta na kitaifa.
Dosari hii ilirekebishwa kwa kuboresha Dira 2025 kwa njia ya kuandaa mpango mkakati wa muda mrefu wa miaka 15 iliorithi Dira 2025, yaani "Long Term Perspective Plan (LTPP)." Kimsingi, LTPP (2011-2025) ilikuwa ni Revised Edition ya Vision 2025 iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka 15 kuanzia 2011 mpaka 2025.
Katika muktadha huu wa kihistoria, zoezi la maandalizi ya Dira 2050 lilizinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais, kwa niaba ya Rais, Jijini Dodoma, tarehe 3 Aprili 2023.
Wananchi wote tulialikwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Dira mpya. Lakini pia, wito wa ushiriki mpana ulirudiwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 11 Septemba 2023, Jijini Dar Es Salaam, wakati akifungua mkutano maalumu wa Baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia.
Rais Samia aliunda Tume ya Mipango ikiwa chini ya Wizara ya Mipango. Aidha aliteua wajumbe wa Tume hii. Wajumbe wanne wa kwanza walikuwa ni wafuatao:
- Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Mstaafu na mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, New York;
- Omar Issa, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Kitengo cha Rais cha "Matokeo Makubwa Sasa" (BRN) wakati wa Rais Jakaya Kikwete;
- Ami Mpungwe, Mkurugenzi wa zamani Katika Wizara ya Mambo ya Nje, aliyesimamia Masuala ya Ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati, na Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Afrika Kusini; na
- Maryam Salim, Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia huko Cambodia.
Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, akihutubia katika uzinduzi huo, aliwataja wajumbe 22 wa Kamati ya Dira 2050. Wajumbe hao 22 ni hawa:
- Prof. Lucian Ambrose , wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mwenyekiti wa Kamati);
- Prof. Joseph J. Semboja, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa REPOA na Taasisi ya Uongozi;
- Dr. Asha Rose Migiro, Mwanadiplomasia aliyewahi kufanya kazi kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa;
- Dr. Florence M. Turuka, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Kilimo;
- Dr. Amina Suleman Msengwa, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Idara ya takwimu;
- Aidan Frederick Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Afrika Mashariki.
- Dr. Yahya Hamad Sheikh, Mhadhiri katika chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) katika idara ya TEHAMA.
- Dr. Maryam Vuai, Mchumi katika KItengo cha Utafiti wa Masuala ya Uchumu-jamii na Uchambuzi wa Sera cha Zanzibar (ZRCP);
- Mr. Abdul Rajabu Mhinte, Ofisa kutoka Ofisi ya Rais;
- Mr. Emmy Kalomba Hudson, Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
- Dr. Ntuli Angyelile Kapologwe, Mkurugenzi wa Idara ya Kuzuia Magonjwa katika Wizara ya Afya.
- Mr. Godfrey Kirenga, Mkurugenzi Mtendaji katika kituo cha SAGCOT Centre Ltd;
- Eng. Ally Bondo Samaje, Kamishna Mzaidizi katika Wizara ya Madini;
- Dr.Richard Joseph Kimwaga, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Idara ya Maji;
- Dkt. Richard Shukia, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Idara ya Elimu ya awali;
- Dr. Gladness Ladislaus Salema, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Idara ya Usambazaji wa Huduma za Afya kwa Umma;
- Mr. Imani Richard Nkuwi, Kamishna wa Uhifadhi wa Mazingira kwenye Wizara ya Utalii na Maliasili;
- Ms. Amne Sued Kagasheki, Mwanasheria na Mshauri katika Masuala ya uwekezaji chini ya Kikundi cha wataalam wa Shikana;
- Mr. Zahoro Muhaji, MKurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tanzania Startup Association(TSA).
- Ms. Neema Mduma, Mhadhiri katika Chuo cha tehama na Sayansi ya Uhandisi wa Mawasiliano (CoCSE) kwenye Taasisi ya Nelson Mandela ya Sayansi na Tekinolojia katika Afrika (NM-A-IST;
- Ms. Dorice Mgetta, Mjumbe wa Bodi ya Tanzania Trade Authority (TTA); na
- Mr. Lawrence N. Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.
- Kubuni dira na miongozo ya uchumi wa Taifa;
- Kusanifu sera za kiuchumi, usimamizi wa uchumi, utafiti, na mikakati ya maendeleo ya Taifa;
- Kufanya tathmini ya hali ya rasilimali za taifa kwa ajili ya kuendeleza na kuishauri serikali juu ya matumizi bora ya rasilimali hizo;
- Kuchambua mwelekeo wa vigezo muhimu vya kiuchumi ikiwa ni pamoja na urari wa malipo, ujazo wa fedha na bei na kuishauri serikali ipasavyo;
- Kuchambua sera zilizopo kwa nia ya kuimarisha utekelezaji wake na kupendekeza sera mpya pale inapoonekana ni muhimu;
- Kufuatilia utendaji wa kila siku wa sekta mbalimbali za uchumi na kuhakikisha kuwa hatua zinazofaa zinachukuliwa ili kutatua matatizo yoyote ya kiutendaji yanayoweza kugunduliwa katika sekta hizo;
- Kuhakikisha miongozo juu ya mahusiano ya kiuchumi na mataifa mengine na mashirika ya kimataifa imeandaliwa;
- Kuandaa mikakati ya kitaifa ya idadi ya watu;
- Kutoa miongozo ya uundaji wa Mpango wa Taifa na kufuatilia mchakato wa maandalizi ya mipango ya muda mrefu, mipango ya muda wa kati na mipango ya muda mfupi;
- Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya serikali kuhusu masuala ya mipango na usimamizi wa uchumi; na
- Kuchambua masuala yoyote ya kijamii na kiuchumi na kupendekeza kwa serikali sera na hatua zinazofaa kuchukuliwa kwa maslahi ya taifa.
Jina rasmi la kitabu kinachohakikiwa hapa ni "Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050." JIna lake kwa kifupi ni “Dira 2050”.
Mwandishi wake ni “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” na ni Toleo la Juni 2025. Lakini mchapaji wake hajatajwa.
Ktabu cha Dira 2050 kinajadili maeneo ya kimkakati (thematic areas) matatu, au tuseme thema za kimkakati tatu, kuhusu maisha ya Watanzania.
Maeneno hayo ni uchumi, jamii na mazingira. Maeneo haya matatu ya kimkakati yameitwa "nguzo" za kimkakati.
Kila eneo la kikimkati linajumuisha sekta kadhaa za maisha ya watu, zenye uhusiano wa karibu.
Kwa pamoja maeneo yote matatu ya kimkakati yamebeba malengo 26. Malengo haya yanagawanyika katika madhumuni 147.
Mambo yote haya yametawanywa kati ya sura ya 8 za kitabu chenye ķurasa 62.
Mchoro ufuatao unafupisha muundo wa Dira 2050. Nimeuandaa kwa kutohoa Kielelezo Na. 1 kwenye Dira 2050.
IV. Muhtasari wa malengo katika nguzo za maeneo ya kimkakati
Ufupisho wa maudhui ya Dira 2050 unafuata hapa chini, kabla ya uhakika wake.
Malengo katika eneo la kimkakati la Uchumi imara, jumuishi na shindani
- Uchumi jumla, tulivu na unaotabirika
- Mfumo endelevu wa kibajeti
- Vyanzo anuai na bunifu vya mapato
- Mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji
- Sekta imara ya biashara
- Ushirikiano wa kimkakati kikanda na kimataifa
- Usafirishaji fungamanishi
- Nishati
- Sayansi na teknolojia
- Utafiti na maendeleo
- Mageuzi ya kidijitali
- Jamii iliyoelimika, yenye ujuzi na inayopenda kujifunza
- Jamii yenye afya
- Hifadhi ya jamii
- Makazi bora ya gharama nafuu
- Nguvu kazi yenye ari na uwezo
- Jamii yenye umoja, mshikamano na uwajibikaji
- Uhifadhi wa bayoanwai
- Uhifadhi wa ardhioevu na vyanzo vya maji
- Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira
- Usimamizi madhubuti wa ardhi
- Ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi
Matarajio katika sekta ya Utawala (Utawala bora na haki)
- Taifa la kidemokrasia linalozingatia utawala wa sheria, haki za binadamu na upatikanaji wa haki jamii.
- Utawala unaozingatia uadilifu na unaoongoza mapambano dhidi ya rushwa kama msingi wa uwajibikaji, uwazi na haki.
- Taasisi imara zinazofuata misingi ya usawa na haki, zinazotoa huduma kwa ufanisi bila upendeleo ili kujenga imani ya wananchi.
- Uongozi wenye maono, unaowajibika na wenye kushirikisha jamii, hususan vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu, katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
- Mfumo madhubuti wa kikatiba na kisheria unaoakisi muafaka wa kitaifa, ili kuhakikisha kuwepo kwa haki na usawa.
- Sekta ya habari inayofanya kazi kwa uhuru, uwazi na inayochochea uwajibikaji, uhuru wa kujieleza na upatikanaji sawa wa taarifa, kama mhimili wa demokrasia hai.
- Asasi za kiraia zenye uwezo na ufanisi, zinazochangia kwa umakini katika kuimarisha demokrasia, kukuza na kuthamini sauti za wananchi, na kuhakikisha uwajibikaji kwa maslahi ya Taifa.
- Jamii salama na iliyo huru dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na wa watoto, ambapo kila mtu, ikiwemo watu wenye ulemavu na wazee, yuko salama, ana furaha, anaheshimiwa na kuwezeshwa.
- Mamlaka za serikali za mitaa jumuishi, zinazojitegemea, kuwajibika kwa wananchi na kuendeshwa bila rushwa.
- Ushirikiano wa wazi na wenye tija kati ya serikali kuu na serikali za mitaa, unaohakikisha mgawanyo endelevu wa rasilimali na utoaji wa huduma bora kwa ufanisi.
- Serikali za mitaa zinazoimarisha mshikamano wa kijamii na kuweka mazingira wezeshi kwa biashara na uwekezaji.
- Ukuaji jumuishi na mgawanyo sawia wa rasilimali ili kukuza ustawi, kuongeza mshikamano na kasi ya utatuzi wa changamoto za kijamii.
- Mfumo wa utumishi katika serikali za mitaa uliojikita kwenye misingi ya uadilifu na unaozingatia sifa na uwezo katika kuajiri na upandishaji vyeo ili kuendeleza weledi na ufanisi katika utoaji wa huduma
- Utumishi wa umma unaofanya kazi kwa ufanisi, uwajibikaji, uadilifu, uwazi na wenye kupambana na rushwa ili kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa maendeleo na manufaa ya wote.
- Utumishi wa umma unaozingatia viwango vya juu vya weledi, unaopatikana na kuendelezwa kwa kufuata misingi ya haki, umahiri na utendaji bora.
- Muungano imara na thabiti unaoendeleza umoja wa kitaifa, amani, utulivu, na ustawi wa pamoja kwa wananchi wote kuanzia ngazi ya familia.
- Taifa lenye uwezo wa kubaini na kuchukua hatua mapema dhidi ya matishio ya usalama na maslahi ya taifa, huku likiimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kujenga ustahimilivu dhidi ya changamoto za ndani na za nje.
- Taifa linalothamini na kulinda watu wake wote, wakiwemo watu wenye ulemavu, wazee na wanawake.
- Taifa ambalo ni kielelezo cha amani na maelewano, likiwa na nafasi muhimu katika kuleta utulivu wa kikanda kupitia juhudi za ushirikiano na upatanishi, na kushiriki kikamilifu katika utatuzi wa migogoro ulimwenguni.
- Mazingira tulivu ya kiuchumi yanayozingatia uwiano kati ya uzalishaji na mahitaji ya ndani, urari wa malipo, mapato na matumizi ya serikali pamoja na viwango vya akiba na uwekezaji.
- Sera za uchumi zinazotabirika na kuzingatia uwazi , pamoja na mfumo thabiti wa kisheria, sera za kifedha na kodi, ili kuvutia uwekezaji endelevu wa ndani na wa nje.
- Mfumo wa kodi wa haki na wenye ufanisi unaochochea ukuaji endelevu na ustawi wa muda mrefu kwa kuongeza uwiano kati ya kodi na pato la Taifa, huku ukichangia maendeleo endelevu.
- Mfumo wa kodi unaotabirika na wa uwazi, unaohamasisha utii wa sheria na kurahisisha uanzishaji, usajili na ukuaji wa biashara ili kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi.
- Usimamizi madhubuti wa deni la taifa unaohakikisha uhimilivu na mgawanyo bora wa rasilimali katika maeneo ya kipaumbele ya maendeleo.
- Matumizi ya fedha za umma yanayozingatia vipaumbele, thamani ya fedha na matokeo makubwa kiuchumi.
- Uwiano mzuri wa matumizi ya Serikali baina ya uwekezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
- Taifa linalotumia kwa ufanisi ushirikiano wa ubia kati ya sekta za umma na binafsi ili kuleta mabadiliko na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
- Soko la fedha linaloongozwa kwa uwazi na ufanisi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazofanikisha shughuli zake bila upotoshaji na linalotoa fursa sawia za upatikanaji wa rasilimali.
- Soko madhubuti la mitaji linalofanya kazi kwa uwazi, lenye vyanzo bunifu na mbadala vya fedha, ili kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi, za kuaminika na za ubora wa hali ya juu kwa wadau wote.
- Ubunifu na uvumbuzi unaochochea ukuaji na ustahimilivu wa sekta za uzalishaji ili kuziwezesha kupata mikopo ya kibiashara na kujiendesha kwa ufanisi.
- Mfumo jumuishi wa kifedha unaoongozwa na sera na mikakati ya uwezeshaji wa wananchi wote, huku ukiweka mkazo maalum kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
- Jamii inayothamini ujasiriamali na yenye wajasiriamali wenye uthubutu na usimamizi bora wa biashara kwa ukuaji endelevu na urithi wa mali kwa vizazi vijavyo.
- Mfumo thabiti wa kusaidia kampuni zinazochipukia ambao unaziunganisha na taasisi za mitaji na uwekezaji ili kuongeza uwezo wao katika ubunifu, biashara na matumizi bora ya teknolojia za kidijitali.
- Kuwa moja kati ya nchi tatu zinazoongoza Afrika kwa kuvutia uwekezaji na urahisi wa kufanya biashara.
- Kuwa na sera, sheria na kanuni wezeshi zinazopunguza udhibiti uliokithiri na zinazochochea ukuaji wa biashara za ndani pamoja na kuvutia uwekezaji wa ndani na wa nje.
- Kuwa na mfumo imara wa kidijitali, unaoendeleza biashara zinazochipukia kupitia sera, ufadhili, mitaji, na sheria zinazoharakisha ukuaji ili kuongeza ajira na kuimarisha uchumi.
- Kuwa na jamii yenye utamaduni wa kuweka akiba na uwekezaji kwa ajili ya kuendeleza biashara, kuongeza kipato na kuimarisha hali ya maisha.
- Kuwa na sekta ya umma iliyoandaliwa kuwezesha na kufanikisha biashara na uwekezaji.
- Mfumo wa uwekezaji unaobainisha maeneo ya uwekezaji kati ya mashirika ya umma ya kibiashara na sekta binafsi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu.
- Utumishi wa umma unaotambua umuhimu na kuunga mkono maendeleo ya sekta binafsi, kwa kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.
- Sekta binafsi shindani, thabiti, jumuishi na inayowajibika, inayochangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
- Mashirika ya umma ya kibiashara yanayoendeshwa kwa uwazi na ushindani, yanayojitegemea na yenye kuleta faida, na yanayovutia uwekezaji huku yakishirikiana kikamilifu na sekta binafsi ili kukuza uchumi.
- Sekta ya wajasiriamali wadogo na wa kati iliyoimarika, ya kisasa na iliyorasimishwa, ikifanya kazi sambamba na makampuni bunifu na shindani kimataifa, katika kuendeleza ukuaji wa uchumi na ustawi wa kijamii wa taifa.
- Taifa linaloenzi urithi wake wa kihistoria katika ukombozi wa Bara la Afrika na kutumia vyema fursa za mabadiliko ulimwenguni ili kuongeza ushawishi wake kidiplomasia.
- Taifa linaloongoza katika kudumisha utulivu na amani barani Afrika na duniani kote, na kuchangia kikamilifu kulinda haki za binadamu na juhudi za kupambana na athari za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi huku likitetea ipasavyo maslahi ya bara la Afrika.
- Ushirikiano wa kimkakati na nchi zilizoendelea na zinazoendelea kiuchumi unaolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi, kwa lengo la kuvutia uwekezaji na maendeleo ya teknolojia.
- Tanzania kuwa lango kuu la biashara mashariki na kusini mwa Afrika ikitumia nafasi yake ya kijiografia kurahisisha biashara mipakani na kuimarisha ushirikiano.
- Taifa linaloongoza kwa biashara ya usafirishaji likiunganisha nchi za Afrika Mashariki, za kati na kusini na masoko mengine ya kimataifa.
- Mtandao wa usafirishaji fungamanishi wenye mfumo wa kisasa na shindani, unaounganisha shoroba za kiuchumi ili kuwezesha biashara za ndani na za kimataifa kwa ufanisi na kuongeza ushindani wa Tanzania katika sekta ya usafirishaji.
- Watoa huduma za usafirishaji wenye viwango vya kimataifa, wenye kutoa huduma kwa ushindani huku wakitumia teknolojia za kisasa za kidijitali ili kuongeza ufanisi na kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa katika mnyororo wa thamani.
- Mazingira bora ya usimamizi wa usafirishaji yanayorahisisha taratibu za forodha, kupunguza urasimu na vikwazo, kuzingatia viwango vya kimataifa, na kuendana na kasi ya maendeleo katika sekta ya usafirishaji.
- Mtandao jumuishi wa usafirishaji wenye miundombinu inayozingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu ili kutoa fursa sawa kwa wote katika biashara za ndani na kimataifa.
- Mfumo bora wa nishati safi ulio stahimilivu, wenye ufanisi, wa kuaminika na wa gharama nafuu.
- Miundombinu thabiti ya nishati inayochochea maendeleo ya viwanda na ustawi wa kiuchumi na kijamii.
- Taifa linalozalisha nishati ya kutosha kukidhi mahitaji ya ndani, huku likijipambanua kuwa moja ya wazalishaji wakuu wa nishati katika ukanda wa mashariki na kusini mwa Afrika.
- Ongezeko kubwa la matumizi ya teknolojia za kisasa katika ngazi zote za uzalishaji na utoaji wa huduma ili kuongeza ufanisi na kuchochea mabadiliko.
- Kuwa na vituo vya ubunifu na maeneo mahususi yenye hadhi ya kimataifa kwa ajili ya tafiti na uvumbuzi katika sekta muhimu kama kilimo, viwanda na afya, vikiwa na wataalamu mahiri na rasilimali za kutosha kukidhi mahitaji ya viwanda vya ndani.
- Jamii inayotumia teknolojia za kisasa zinazojumuisha na kukidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu, kwa kuzingatia mifumo inayowapa fursa ya kushiriki kikamilifu na kuchangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
- Taasisi imara zinazofanya ufuatiliaji na tathmini ya taarifa za maendeleo ya kiteknolojia ili kuiandaa nchi kuwa tayari kutumia teknolojia kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha ushindani.
- Mfumo jumuishi unaokuza masomo na matumizi ya sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati, ukiwa na lengo la kutoa fursa sawa na kuwawezesha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kisayansi na ubunifu.
- Uwekezaji thabiti na jumuishi katika kukuza na kutumia teknolojia zinazoibuka ili kusaidia viwanda na kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
- Mfumo imara wa utafiti na maendeleo unaovutia ushirikiano wa kimataifa, ukiimarishwa na ulinzi madhubuti wa hakimiliki ili kuchochea ubunifu na kuendeleza uwekezaji.
- Mfumo wa uhakika wa kugharamia utafiti na maendeleo, kwa kutumia kiwango kisichopungua asilimia moja ya Pato la Taifa, na unaotoa motisha kwa sekta binafsi kuwekeza katika sekta muhimu kama kilimo, bioteknolojia, nishati safi na teknolojia zinazoibukia katika TEHAMA na nyanja nyingine.
- Taifa lenye mtazamo wa kimaendeleo na lenye utamaduni wa kufanya maamuzi kwa kutegemea ushahidi wa kisayansi, likichochewa na utafiti wa kiwango cha hali ya juu ili kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
- Kitovu cha ubunifu cha kikanda kinachochochea uvumbuzi kwa wataalamu wa ndani na kinachotoa huduma kamili za ubunifu, kuanzia uvumbuzi hadi kufanya biashara.
- Vyuo vikuu na taasisi mahiri za utafiti zenye viwango vya kimataifa, na zenye ushirikiano thabiti na sekta mbalimbali kwa ajili ya kuchochea ubunifu kwenye uzalishaji na kutatua changamoto za jamii.
- Mfumo imara wa kuendeleza ubunifu unaoendana na maendeleo ya kiteknolojia, utakaoifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uvumbuzi duniani.
- Jamii yenye umahiri katika matumizi salama ya mitandao na teknolojia za kidijitali, na inayozingatia misingi bora na maadili kwa maslahi ya jamii na taifa.
- Kitovu cha kikanda cha maendeleo ya teknolojia kinachohamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuendeleza ubunifu, kuchochea maendeleo, na kuongeza ushindani wake katika soko la kimataifa.
- Upatikanaji wa intaneti ya kasi na huduma za mawasiliano zilizo na uhakika na za gharama nafuu kote nchini.
- Mfumo thabiti na jumuishi wa usimamizi wa takwimu na taarifa unaowezesha upatikanaji wa taarifa sahihi, za kuaminika na kwa wakati, huku taifa likidumisha mamlaka kamili ya kudhibiti, kuhifadhi na kutumia taarifa hizo kwa mujibu wa sheria na maslahi ya kitaifa..
- Ongezeko la matumizi ya data kibiashara kwa lengo la kuongeza thamani yake kiuchumi na kuongeza ajira.
- Taifa linaloongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini kwa uzalishaji wa programu za kompyuta na maudhui ya kidijitali, kwa matumizi ya soko la ndani na la kimataifa.
- Taifa lililo mstari wa mbele katika matumizi ya teknolojia zinazoibukia, lenye nguvukazi yenye mtazamo wa kisasa ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
- Serikali mtandao inayotoa huduma bora, jumuishi, na zenye ufanisi kwa raia na biashara, kwa lengo la kuimarisha ubora wa huduma za Serikali.
- Taifa ambalo kila mtoto anapata malezi na makuzi bora, analindwa na anapata msingi imara wa kujifunza na wa maisha, kupitia vituo vya malezi na makuzi, pamoja na elimu bora na ya lazima ya awali, inayotolewa kupitia mfumo madhubuti na endelevu unaojitegemea.
- Mfumo wa elimu na mafunzo bora, jumuishi, unaostahimili changamoto, wenye viwango vya ubora vinavyotambulika kimataifa, unaozalisha wahitimu wenye maarifa, ujuzi, na stadi za maisha pamoja na mtazamo chanya utakaowawezesha kuchangia katika maendeleo endelevu ya Taifa. Walimu na wakufunzi mahiri na wenye ari watakuwa nguzo muhimu katika mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji.
- Shule na taasisi za elimu salama na jumuishi zinazoweka kipaumbele kwenye ustawi na fursa sawa kwa watoto na vijana wote.
- Wahitimu wenye ujuzi stahiki na uwezo wa kushindana na kufanikiwa katika soko la ajira kimataifa.
- Jamii bunifu na stahimilivu inayoongozwa na maarifa katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
- Jamii yenye elimu na maarifa ya fedha ambapo watu wana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi juu ya matumizi ya fedha, kusimamia rasilimali kwa ufanisi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.
- Jamii inayojifunza bila kikomo kwa lengo la kujenga uwezo wa kila Mtanzania kukabiliana na mabadiliko ya kiulimwengu
- Kuwa na huduma bora za afya kwa wote, zenye mfumo wa uhakika na endelevu wa kugharamia na unaotoa kipaumbele kwa wanawake, watoto, vijana, wazee na watu wenye ulemavu.
- Kuwa taifa la watu wenye ustahimilivu, na jamii iliyo tayari kuimarisha afya na kujikinga na maradhi kwa kuzingatia mtindo wa maisha unaowezesha kukabiliana na magonjwa ya milipuko, changamoto za afya na mabadiliko ya tabianchi.
- Kuwa na jamii yenye afya ambapo kila mtu anapata huduma za afya kwa usawa na kwa gharama nafuu.
- Kuwa na jamii ambayo kila mtu anastawi kutokana na lishe bora na analindwa dhidi ya bidhaa zenye madhara.
- Kuwa kitovu cha kikanda katika uzalishaji wa bidhaa bora za afya na lishe, ili kuhakikisha bidhaa hizi zinapatikana kwa wingi na kwa gharama nafuu.
- Kuwa kitovu cha huduma bobezi za afya, zinazokidhi mahitaji ya ndani na nje ya nchi na kuvutia utalii wa kimatibabu.
- Kuwa na mfumo wa afya unaotumia teknolojia za kisasa kama vile akili unde katika kung’amua na kudhibiti maradhi kwenye vinasaba.
- Kuwa na elimu na huduma bora za afya ya uzazi kwa wote.
- Kuwa taifa ambalo hakuna mwanamke anayepoteza maisha wakati wa kujifungua na kila mtoto anayezaliwa anaishi na kustawi.
- Taifa ambalo kila mtu hususan wanawake, watu wenye ulemavu na wazee wananufaika na mifumo ya hifadhi ya jamii iliyo thabiti, bunifu na endelevu.
- Jamii salama dhidi ya ajira kwa watoto, ukatili, na ubaguzi, ambapo kila mtoto analelewa katika mazingira salama, yenye malezi bora na fursa za maendeleo ili aweze kustawi kikamilifu.
- Jamii ambayo makundi maalumu na yenye uhitaji yameunganishwa kupitia mifuko maalumu ya hifadhi ya jamii inayohakikisha kuwepo kwa usalama wa kipato, upatikanaji wa huduma muhimu, na fursa za uwezeshaji kiuchumi.
- Taifa linalolinda kikamilifu maslahi ya watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha upatikanaji sawia wa miundombinu, huduma na fursa.
- Jamii inayoundwa na familia imara ambazo zinawajibika na kushirikiana katika kuimarisha uadilifu, maadili na ustawi wa kila mtu.
- Taifa ambalo kila mtu ana makazi bora na nafuu yanayochochea jamii endelevu mijini na vijijini.
- Taifa lenye uwiano mzuri na jumuishi wa maendeleo kati ya miji, vijiji na kanda.
- Miji endelevu ya kisasa na ya kijani inayochochea maisha yenye ustawi kwa wote, wakiwemo watu wenye ulemavu.
- Taifa ambalo kila mtu anapata huduma nafuu za maji safi na salama sambamba na huduma bora za usafi ili kuimarisha afya ya jamii.
- Mtandao imara wa nishati unaotoa kipaumbele kwa nishati safi na mbadala, ukipunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa, kulinda mazingira, na kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu kwa sekta zote za jamii.
- Taifa lenye mifumo bora ya usafiri wa umma, inayorahisisha usafiri wa watu na usafirishaji wa bidhaa.
- Nguvukazi mahiri na yenye ujuzi, inayotumia teknolojia, inayoweza kuhimili mabadiliko na kuchochea ubunifu na ushindani katika masoko ya ndani na ya kimataifa.
- Taifa linalovutia, kukuza, na kuhifadhi vipaji na utaalamu miongoni mwa raia na wageni, ili kujenga rasilimali watu kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
- Idadi ya watu ambayo uchumi unaweza kuhimili, ili kuwa na maisha bora kwa kila mtu.
- Jamii yenye uwazi, inayothamini kujifunza kutoka kwa wengine, na inayokuza ushindani katika soko la ajira ili kujenga nguvukazi yenye ujuzi, tija, na ubunifu.
- Nguvukazi yenye motisha na ari, inayofanya kazi kwa bidii, uadilifu na maadili ili kuchochea kasi ya maendeleo.
- Taifa lenye umoja, mshikamano na linaloendeleza na kutumia kikamilifu vipaji vya watu wake katika sanaa, ubunifu, michezo, na burudani kama kielelezo cha utambulisho wake.
- Raia wanaowajibika, wenye maadili na uzalendo, na ambao wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kijamii.
- Jamii yenye fikra za kimaendeleo inayotambua muda na rasilimali kama mali adhimu na adimu, zinazopaswa kutumiwa kwa uadilifu ili kuchagiza maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kwa faida ya kizazi cha leo na vizazi vijavyo.
- Kuwa miongoni mwa nchi mahiri katika uhifadhi wa bioanuai, yenye mifumo bora ya ikolojia, ambapo aina mbalimbali za viumbe hai zinastawi katika makazi yao ya asili.
- Taifa kinara kwa matumizi endelevu ya bioanuai kwa manufaa ya ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumi kwa kizazi cha sasa na kijacho.
- Taifa linalokokotoa vyema thamani ya rasilimali za bioanuai na maliasili za nchi ili zitumike kikamilifu kuchangia katika pato la taifa na maendeleo ya jamii.
- Ardhioevu bora zinazochangia ustawi wa watu, kukuza uchumi na kutoa huduma muhimu za kiikolojia.
- Taifa lenye uhakika na usalama wa maji kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi na linalodumisha na kuendeleza uhifadhi wa ikolojia.
- Taifa lenye mfumo im
- Jamii yenye uelewa mkubwa wa athari za uchafuzi wa mazingira ili kuwa na mazingira salama na endelevu kwa wote.
- Majiji na miji yenye miundombinu na usimamizi bora wa taka na ujenzi unaozingatia uhifadhi wa mazingira.
- Taifa kinara katika matumizi endelevu ya rasilimali na linalotumia taka kama malighafi kwa manufaa ya kiuchumi.
- Taifa lenye mazingira stahimilivu linalosimamia vyema maliasili kwa maendeleo ya uchumi wa kijani.
- Nchi iliyopangwa vizuri na kuweka wazi matumizi ya ardhi, yakiwemo ya makazi, kilimo, mifugo, viwanda na hifadhi.
- Usimamizi bora wa ardhi unaoongozwa na nguvu ya soko la ardhi, mali isiyohamishika na huduma, ili kuvutia uwekezaji unaotegemea ardhi.
- Jamii yenye usawa ambapo kila mwananchi, hususan wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, wanapata fursa sawia za umiliki wa ardhi.
- Taifa ambalo mipaka imepimwa kwa usahihi, kuimarishwa kikamilifu na inayotambulika kimataifa.
- Taifa endelevu na stahimilivu linalotumia nishati safi na ya gharama nafuu na linalosimamia kwa ufanisi uzalishaji wa hewa ukaa kwa ajili ya mustakabali wa nchi.
- Taifa lenye uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, likilinda wananchi wake, miundombinu na mali dhidi ya majanga ya asili na yale yatokanayo na shughuli za kibinadamu, ambapo wanawake na vijana wapo mstari wa mbele.
- Taifa kinara katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, likiwa ni kielelezo katika ustahimilivu, uendelevu, na uwezo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
- Taifa linalotumia kikamilifu fursa za biashara ya hewa ukaa na upatikanaji wa fedha kupitia ajenda ya mabadiliko ya tabianchi duniani ili kuongeza uwezo wa jamii na taifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
VI. Mazuri katika Dira ya Tanzania 2050
Tunu za kitaifa
Nimefurahishwa na tunu kumi ambazo zimetajwa kama sehemu ya "misingi ya dira" (uk. 8), yaani tunu zifuatazo:
- demokrasia,
- haki,
- uhuru,
- utu,
- amani,
- umoja,
- utajiri,
- rasilimali asilia,
- utamaduni na
- maadili ya Taifa.
Maeneo ambayo ni nguzo za kimkakati
Aidha, nimefurahishwa na uwepo wa thema tatu zilizotajwa kwenye Dira ya Tanzania 2050, ambazo ni:
- Thema ya kwanza (ambayo imetajwa kama nguzo ya kwanza ya Dira ya Tanzania 2050), "Uchumi Imara, Jumuishi, na Shindani,".
- Thema ya pili (ambayo imetajwa kama nguzo ya pili ya Dira ya Tanzania 2050), "Uwezo wa Watu na Maendeleo ya Jamii".
- Na thema ya tatu (ambayo imetajwa kama nguzo ya tatu ya Dira ya Tanzania 2050), "Uhifadhi wa Mazingira na Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi".
Kadhalika, nimefurahishwa na malengo ya thema tatu, yaliyotamkwa kama ifuatavyo kwenye Dira ya Tanzania 2050:
- Thema ya kwanza, "Uchumi Imara, Jumuishi, na Shindani," inabeba lengo kuu la kisekta la "kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uchumi katika Afrika mashariki na bara la Afrika kwa ujumla" (uk. 10). Kitaalam, thema hii inaitwa "core theme".
- Thema ya pili, "Uwezo wa Watu na Maendeleo ya Jamii," inabeba lengo kuu la kisekta la "kujenga jamii yenye afya, elimu bora na mshikamano" (uk. 10). Kitaalam, thema hii inaitwa "core theme".
- Na thema ya tatu, "Uhifadhi wa Mazingira na Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi," inabeba lengo kuu la kisekta la "kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya maliasili za taifa" (uk. 10). Kitaalam, thema hii inaitwa "core theme" pia.
Vile vile, nimefurahishwa na "ndoto" ya kitaifa yenye kuunganisha malengo makuu ya kisekta yaliyotajwa hapo katika "maono" mapana ya kujenga "Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea" kisiasa, kiuchumi na kijamii ndani ya "mazingira" yaliyo rafiki kwa uhai wa watu (uk. 7).
VII. Mabaya ya kimuundo katika Dira ya Tanzania 2050
Baada ya kupitia Dira ya Tanzania 2050, ni maoni yangu kwamba, kuna shida katika masuala kadhaa.
Ukosefu wa dhima ya Taifa
Maono yaliyotajwa yakisomwa pamoja na malengo ,manne ya maeneno ya kimkakati yaliyotajwa hapo juu yanatupa "dhima" ya kitaifa ifuatayo.
Dhima ya Taifa kuelekea 2050 ni kujenga "Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea" kisiasa, kiuchumi na kijamii ndani ya "mazingira" yaliyo rafiki kwa uhai wa watu kwa:
- "kuboresha taasisi za kidemokrasia, kupambana na rushwa na kuhakikisha kunakuwa na uadilifu na uwajibikaji katika nyanja zote, zikiwemo sekta za umma na binafsi,"
- "kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uchumi katika Afrika mashariki na bara la Afrika kwa ujumla,"
- "kujenga jamii yenye afya, elimu bora na mshikamano,"
- "kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya maliasili za taifa," na
- Kwa kuzingatia tunu za demokrasia, haki, uhuru, utu, amani, umoja, utajiri, easilimali asilia, utamaduni na maadili ya Taifa.
Ukosefu wa nguzo ya eneo la kimkakati la siasa
Dira 2050 imetaja nguzo tatu. Hata hivyo, kuna theme moja inakosekana kwenye Dira 2050. Ni thema ya "Siasa".
Huwa tunatofautisha kati ya siasa na utawala kwa kuwa kuna siasa za aina mbili. Kuna siasa ndani ya utawala na siasa nje ya utawala.
Katika siasa za vyama vingi, sekta ya siasa huweka malengo ya kuendesha nchi, kisha utawala hutekeleza malengo hayo kupitia ilani ya chama cha siasa kilichoshinda uchaguzi.
Vyama baki vinaendelea na siasa nje ya utawala, vikiwa na ushirikiano fulani na chama tawala, vyama vya kiraia na sekta ya uchumi.
Kwa hiyo, ni muhimu kubainisha nguzo ya siasa kama eneo la kimkakati, yaani "thematic area." Dira imesahau kuitambua thema hii.
Ni dosari kubwa kwa kuwa, kwa njia hii, tunaweza kuwa tumefuta sekta ya asasi za kiraia. Tusisahau Dira 2050 kuhakikisha kwamba:
The words 'civil society' and 'civic society," which are often used interchangeably, are somehow different.
"Specifically, 'civil society,' in general, encompasses the sphere of organized social life that is voluntary, self-generating, and independent from the state and commercial interests.
They advocate for social, economic and political change which will improve the quality of life of everybody. They include: Pro-democracy groups, Labor groups, Professional groups, Religious groups, Student groups, Gender-based groups, and Human rights groups.
"Within this context 'civic society' refers to the aspect of civil society related to citizen participation in public life and governance."
Ukosefu wa majina rasmi ya kisekta
Kuna ukosefu wa majina ya sekta. Malengo ya kisekta yametajwa kwenye Dira 2050 bila kuweka bayana majina ya sekta husika.
Mifano ya majina ya sekta yanayoonekana kwenye Dira 2050 ni haya hapa, kati ya mengine:
- Ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi,
- Usimamizi madhubuti wa ardhi,
- Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira,
- Uhifadhi wa ardhioevu na vyanzo vya maji,
- Uhifadhi wa bayoanuai,
- Jamii yenye umoja, mshikamano na uwajibikaji,
- Nguvu kazi yenye ari na uwezo,
- Makazi bora ya gharama nafuu, Jamii yenye afya,
- Jamii iliyoelimika na yenye ujuzi na inayopenda kujifunza,
- Mageuzi ya kidijitali,
- Usafirishaji fungamanishi,
- Mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji,
- Vyanzo anwai na bunifu vya mapato,
- Mfumo endelevu wa kibajeti,
- Utumishi wa umma unaowajibika,
- Serikali za mitaa imara na zenye ufanisi,
- Utawala bora na haki.
Na je, Kwanini sekta iitwe "Jamii iliyoelimika na yenye ujuzi na inayopenda kujifunza" badala ya kuitwa sekta ya "Elimu"?
Dira 2050 haina majibu kwa maswali haya.
Ninachoona ni kwamba timu ya kuandaa Dira 2050 haikufanya homework yake vema katika kipengele cha kubaini idadi ya sekta kwa kila eneo la kimkakati ili majina rasmi yaweze kutamkwa bayana.
Hivyo, majina haya yanapaswa kuangaliwa upya ili kuweka mfumo wa majina sahihi ya sekta zinazohusiana na Dira 2050.
Idadi ya malengo makuu kupishana na idadi ya maeneo ya kimkakati
Dira ya Tanzania 2050 inataja maeneo ya kimkakati matatu, yaani "thema" tatu, kila thema ikiwa na lengo kuu moja. Hata hivyo Dira hiyo yenye "thema" tatu pia imetaja malengo makuu manne ya kisekta.
Lengo kuu la nne linahusu tehama wakati tehama sio "thema" kuu.
Hapo kuna shida inayopaswa kuondolewa. Idadi ya malengo ya kisekta na idadi ya sekta lazima viwe sawa.
Ukosefu wa mitambaapanya inayounganisha maeneo ya kimkakati
Dira 2050 ni kama nyumba yenye nguzo na mitambaapanya inayounganisha nguzo hizo.
Lakini Dira 2050 imetaja nguzo za kimkakati bila kubainisha mitambaapanya yote muhimu.
Kuna mtambaapanya mmoja pekee umetajwa, yaani, "Utawala bora, amani, usalama na utulivu."
Kwa mujibu wa Dira 2050, mtambaapanya huu unayo kazi ya kubeba lengo la "kuboresha taasisi za kidemokrasia, kupambana na rushwa na kuhakikisha kunakuwa na uadilifu na uwajibikaji katika nyanja zote, zikiwemo sekta za umma na binafsi" (uk. 10).
Malengo katika eneo la kimkakati la Utawala, amani, usalama na utulivu ni haya:
- Utawala bora na haki
- Serikali za mitaa imara na zenye ufanisi
- Utumishi wa umma unaowajibika
- Amani, usalama na utulivu
Hivyo, kuna uzigizaga unaoleta ukakasi kwa msomaji, kiasi kwamba msomaji hawezi kuona uhusiano ulipo kati ya "tunu", "nguzo," "misingi," "vichocheo," na sekta za "mageuzi."
Mkanganyiko huu unaopaswa kuondolewa kwa kubainisha "strategic planning methodology" iliyotumika kuandaa Dira 2050. Haijatajwa.
Napendekeza kwamba mchoro ufuatao utasaidia kufafanua methodolojia inayopaswa kutumika kuandaa Dira 2050, na hivyo kumwezesha msomaji kufananisha na kutofautisha kati ya nguzo za kimkakati (strategic pillars) zilizo na mkao wa wima na mitambaapanya ya kimkakati (strategic perspectives) iliyo na mkao wa ulalo, ikiwa inaunganisha nguzo za kimkakati.
Nyumba ya Kimkakati katika kutengeneza Dira ya Tanzania 2050
Katika mchoro huu, wenye umbo la ghorofa kuna "nguzo za kimkakati" (strategic themes au strategeic pillars), "malengo ya kimkakati" (strategic goals au strategic results), "sakafu nne za malengo ya kimkakati" (strategic floors au strategic perspectives), dari na paa.
Hizi sakafu nne ndizo narejea kama mitambaapanya inayounganisha maeneo ya kimkakati.
Mtambaapanya wa chini kabisa unajumuisha eneo la "Utawala bora, amani, usalama na utulivu" lililotajwa kwenye Dira 2050. Nitaeleza.
Nguzo za kimkakati ni maeneo ya kimkakati yanayobeba dira na dhima ya taasisi.
Ni kama nguzo na kuta zinazobeba uzito wa nyumba ya ghorofa.
Mhandisi anapokuwa anajenga nyumba ya ghorofa hujiuliza, "Je, iwapo tutajenga ukuta wenye upana huu katika eneo hili, jengo letu litakuwa imara kwa kiasi cha kubeba uzito wa simenti na mchango tunaotaka kuutumua kupandisha jengo hili?"
Vivyo hivyo, mwandaa mkakati lazima ajiulize, "Je, iwapo tutajenga nguzo ya kimkakati yenye upana huu katika eneo hili, mkakati wetu utakuwa imara kwa kiasi cha kuweza kubeba uzito wa dira na matumaini yetu?"
Malengo ya kimkakati ni matokeo yanayotarajiwa kutokea kupitia eneo la kimkakati fulani. KIla nguzo ya kimkakati inalo lengo la kimkakati moja. Lengo la kimkakati linatoa jawabu kwa swali: Tutajuaje kwamba malengo yanayohusiana na nguzo ya kimkakati fulani yametimia?
Mitambaapanya inayounganisha maeneo ya kimkakati ni kama sakafu za malengo yaliyotajwa katika maeneo ya kimkakati.
Hizi ni ngazi za matokeo yanayoletwa na michakato ya kiutekelezaji hatua kwa hatua.
Hatua hizi zina uhusiano wa sababu na matokeo kiasi kwamba hatua zote, kutoka chini hadi juu, zikikamilika ndio dira na dhima ya kitaasisi inatimia.
Sakafu ya kwanza, chini kabisa, ni ngazi ya kwanza ya matokeo ya kimkakati ambayo yakikamilika yanakuwa "kichocheo" au "dereva" wa matokeo ya kimkakati yaliyo katika sakafu ya pili.
Matokeo ya kimkakati yaliyo katika sakafu ya pili yakikamilika yanakuwa "kichocheo" au "dereva" wa matokeo ya kimkakati yaliyo katika sakafu ya tatu.
Na vivyo hivyo mpaka kwenye matokeo yaliyo katika dari na paa.
Kutokana na jadi ya uandaaji wa mipango mikakati ya kitaasisi, kwenye orofa ya mikakati ya kitaasisi, kuna mitambaapanya minne, au tuseme,kuna sakafu kuu nne zinazounganisha nguzo za maeneo ya kimkakati.
Sakafu hizo ni:
- Matokeo yanayohusu ujenzi wa uwezo wa Kitaasisi kwa kukusanya rasilimali rasilimalimvitu na rasilimali watu (institutional capacity),
- Matokeo yanayohusu kasi na viwango vya utekelezaji wa michakato ya kiutawala (Administration processes),
- Matokeo yanayohusu ukusanyaji na usimamizi wa Mapato (Financial Mobilisation), na
- Matokeo yanayohusu utoaji wa huduma kwa wateja (Raia) kwa kutumia mapato yaliyokusanywa (Quality sevices).
Kutekeleza michakato ya Kiutawala kunahusisha kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozi, kwa kufuatilia, kupima matokeo na kuchukua hatua za marekebisho stahiki.
Kukusanya Mapato kunahusisha kukusanya kodi ili kuzitumia kutoa huduma na kuzalisha ziada, kama tunaongelea sekta binafsi.
Na kutoa huduma kwa Wateja kunamaanisha kukidhi matarajio ya wateja, kama mtoa huduma ni serijkali, wateja ni raia wake na wadai wa maedndeleo wengine.
Ili kupata muundo wa mkakati usio na ukakasi, uandishi wa Dira 2050 unapaswa kuzingatia methodolojia hii inayotofautisha nguzo za kimkakati, malengo ya kimkakati na sakafu za malengo ya kimkakati, ambazo pia hapa zinajulikana kama mitambaapanya ya maeneo ya kimkakati.
VIII. Mabaya ya kimaudhui katika Dira ya Tanzania 2050
Baada ya kupitia andiko zima, sijaona mambo makuu manne niliyokuwa nayatafuta kwa bidii. Yaani:
- Maono ya Taifa hayana hayana ndugu zake katika sekta zilizotajwa.
- Hakuna uchambuzi wa NUFU, yaani uchambuzi wa nguvu, udhaifu, fursa na utisho, yaani SWOT analysis, kwa kila sekta ikiyotajwa;
- Hakuna usanisi wa NUFU, yaani SWOT synthesis, kwa kila sekta kuu iliyotajwa;
- Hakuna nadharia ya mabadiliko kwa kila sekta iliyotajwa; na
- Hakuna mfumo wa vigezo vya kufuatilia na kutathmini utekelezaji kwa kila sekta iliyotajwa.
VII. Maono ya Taifa hayana nduguze katika sekta zilizotajwa
Tumeona kuwa:
Dhima ya Taifa kuelekea 2050 ni kujenga "Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea" kisiasa, kiuchumi na kijamii ndani ya "mazingira" yaliyo rafiki kwa uhai wa watu kwa:
- "kuboresha taasisi za kidemokrasia, kupambana na rushwa na kuhakikisha kunakuwa na uadilifu na uwajibikaji katika nyanja zote, zikiwemo sekta za umma na binafsi,"
- "kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uchumi katika Afrika mashariki na bara la Afrika kwa ujumla,"
- "kujenga jamii yenye afya, elimu bora na mshikamano,"
- "kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya maliasili za taifa," na
- Kwa kuzingatia tunu za demokrasia, haki, uhuru, utu, amani, umoja, utajiri, easilimali asilia, utamaduni na maadili ya Taifa.
Pengo hili linapaswa kuzibwa kwa kuangalia Dira ya Zanzibar 2050 imeandikwaje. Mfano wa dira ya kisekta katika sekta ya kilimo kwenye Dira ya Zanzibar 2050 ni huu hapa:
IX. Ukosefu wa uchambuzi na usanisi wa NUFU
Uchambuzi wa NUFU, yaani Uchambuzi wa Nguvu, Udhaifu, Fursa na Utiisho (SWOT analysis) ungesaidia kutupatia jawabu kwa swali lifuatalo: Tuko wapi sasa hivi mwaka 2025. Yaani:
- Nguvu zetu ni zipi?
- Udhaifu wetu ni upi?
- Fursa zilizopo ni zipi?
- Utiisho unaotukabili ni upi?
- Mikakati ya kuyalinda mazuri yetu ni ipi?
- Mikakati ya kuondoa mapungu yetu ni ipi?
- Mikakati ya kuziteka fursa zilizopo ni ipi?
- Mikakati ya kuvikabili vitisho ni ipi?
Kwa pamoja, Uchambuzi wa NUFU na usanisi wa NUFU huzaa mikaka, mbinu na majukumu yanayoendana na uhalisia wa mambo katika nchi.
Bila michakato hii, mpango mkakati unakuwa umeandaliwa kwa mtindo wa mbele kwa mbele, kama wafanyavyo watu wanaodondosha maembe randomely.
X. Ukosefu wa nadharia ya mabadiliko kwa kila sekta
Kuhusu nadharia ya mabadiliko, nilitarajia kuona mnyororo wa sababu na matokeo ufuatao kwa kila sekta inayotajwa: impact, outcomes, outputs, activities, tasks, inputs and performance measurements.
Kwa Kiswahili tunaweza kusema kwamba, katika kila sekta kuna: mabadiliko, matarajio, matokeo, mikakati, mbinu, rasilimali na vipimo vya ufanisi wa kazi.
Kutokana na minyororo ya mabadiliko ndio tunaweza kupata mnyororo wa mabadiliko wa kiraifa wenye uhakika.
Na minyororo ya mabadiliko ya kisekta na hatimaye kwa Taifa zima, hutokana na majawabu ya kitafiti yanayotolewa kwa maswali ya kimkakati wakati wa kuandaa mpango mkakati. Maswali hayo kwa ufupi ni matano:
- Tunataka kitu gani ambacho hatuna kwa sasa?
- Tunacho kitu gani tunachoweza kutumia kupata kitu tusichokuwa nacho?
- Ni vikwazo gani vinaweza kutuzuia kutumia kitu tulicho nacho ili kupata kitu tusicho nacho?
- Na tunawezaje kutumia kitu tulichonacho ili kupata kitu tusicho nacho?
- Tukikipata kitu tunachokitafuta tutakitambuaje?
- Tuko wapi?
- Tunataka kwenda wapi?
- Katika njia zinazowezekana kuna vikwazo gani vinavyoweza kukwamisha safari yetu?
- Na tunaweza kutokaje tulipo na kufika tunakotaka kwenda bila kukwamishwa na vizuizi vilivyoko njiani?
- Tukifika tunakotaka kwenda tutapatambuaje?
- Sisi ni kina nani, sio kina nani, na tumetoka wapi?
- Tuko wapi sasa hivi mwaka 2025, kama tukifanya Uchambuzi wa Nguvu, Udhaifu, Fursa na Utiisho (Uchambuzi wa NUFU)?
- Tunataka tuwe tumefika wapi ifikapo mwaka 2050, kisekta na kitaifa?
- Tutatumia mikakati gani kutoka mahali tulipo sasa hivi 2025 na kufika tunakotaka kwenda ifikapo mwaka 2050?
- Tutatekeleza mbinu na majukumu yapi ili kufanikisha mikakati hiyo?
- Nani atatekeleza majukumu yapi wakati wa safari?
- Safari yetu inahitaji rasilimali kiasi gani ili kutekeleza majukumu yote yaliyopo?
- Safari yetu itatumia muda gani, na kutakuwa na vituo vingapi vya mapumziko ya njiani?
- Tukiwa njiani na tukifika mwisho wa safari yetu tutaona alama gani zitakazotuongoza ili tusipotee na kutujulisha kuwa tumefika salama?
- Na tutalindaje mafanikio tutakayoyapata kwenye safari yetu?
Chanzo: Kamati ya Dira ya Taifa ya Tanzania (2025), Dira 2050, uk. 11.
Hakuna mnyororo wa aina hii kweye andiko zima la Tanzania Vision 2025. Ule mchoro wenye jina "Kielelezo Na. 1" unajaribu kufafanua mnyororo wa mabadiliko haya. Lakini hauna majibu sahihi wala kamilifu kwa maswali haya.
Kuhusu dosari hii, naona kuwa Papua New Guinea Vision 2050 inao mchoro unaeleweka sana.
Nashauri tujifunze kutoka andiko la Papua New Guinea na kuboresha andiko letu la Tanzania Vision 2050 (Kiambatanisho D). Mchoro husika ni huu hapa:
Source: National Strategic Planning Task Force (2020), Papua New Guinea Vision 2050, uk. ii.
Mchoro huu unasomeka kutoka chini kwnda juu, na kisha kutoka kushoto kwenda kulia, katika namna ambayo inaelimisha.
Tukiusoma mchoro kuanzia chini kwenda juu tunapata majibu kwa maswali yote muhimu niliyouliza hapo juu.
Na tukiusoma mchoro kuanzia kushoto kwenda kulia tunapata majibu ya maswali yafuatayo: Kuna mikakati mingapi? Kuna vichocheo vingapi? na kuna vigezo vya kupima ufanisi vingapi?
XII. Ukosefu wa vigezo na shabaha za kuwezesha ufuatiliaji na utathmini wa kazi
Kuhusu mfumo wa vigezo vya kufuatilia na kutathmini utekelezaji, naona hakuna KPIs wala performance targets za kisekta na kitaifa zenye kuonyesha TRENDS kati ya 2025 na 2050.
Timu yako ilipaswa kutufahamisha kwa ufupi kabisa juu ya vigezo na shabaha za kupima ufanisi katika kila sekta iliyotajwa, kwa kutumia ngazi yoyote kati ya ngazi zifuatazo: mabadiliko, matarajio, matokeo, majukumu, na najeti. Hakuna kitu kama hiki kwenye andiko zima kwa kila sekta iliyotajwa.
Vigezo na shabaha za aina hii huonyesha latitudo na longitudo za mabadiliko hatua kwa hatua, mwaka hadi mwaka.
Mfano mzuri wa kontua za mabadiliko ya aina hiyo zimetajwa katika Dira ya Zanzibar kuelekea 2050. Hapa chini natumia sekta ya kilimo kuonyesha kontua za mabadiliko zinazokosekana kwenye Dira ya Tanzania 2050.
Takwimu zinazoonyesha kontua za mabadiliko katika sekta ya kilimo kwenye Dira ya Zanzibar 2050, uk. 13
Yaani, ukweli kwamba, andiko la Tanzania Vision 2050 halijataja maoteo ya shabaha za utendaji wa kisekta (sectoral performance targets) kuelekea 2050 wala kubainisha vigezo vya kisekta kwa ajili ya kupima kasi ya ufanisi (Sectoral Key Performance Indiators), ni "show stopper" kwa msomaji makini.
Fahamu kuwa mkakati usio na shabaha wala vigezo vya kufuatilia ufanisi ni sawa na nyumba isiyo na msingi.
Kwa sababu hizi zote andiko lililozinduliwa pale Dodoma halipaswi kuitwa DIRA kama jina lake linavyoonyesha. Hilo ni jina-koko. Yaani, "it is a misnomer."
Kitabu hakiwi DIRA kwa sababu tu ya jina lake bali kwa sababu ya maudhui yake kuonyesha mkondo wa mabadiliko, hatua kwa hatua, kuanzia majira leo, kupitia majira ya kesho, mpaka majira ya mbali.
XIII. Utamaduni wa makosa haya kujirudia kwa miaka 20 mfululizo
Mpaka kufikia mwaka 2025, makosa haya yamejirudia tena kwa mara nne mfululizo tangu 2005. Tulifanya makosa haya wakati wa kuandaa MKUKUTA ONE ya 2005-2010 na MKUKUTA TWO ya 2010-15.
Pia tulifanya makosa haya wakati wa kuandaa Dira ya Taifa ya 2000-2025 (Kiambatanisho B).
Kwa upande wa maandalizi ya nakala za MKUKUTA mara zote mbili lawama zilielekezwa kwenye taasisi ya utafiti ya REPOA iliyokuwa inapewa tenda za kupika chakula lakini ikawa inapakua chakula kabla hakijaiva, tena mara mbili.
Sina ushahidi wa kunimbusha kama REPOA walihusika kuandaa Tanzania Vision 2025.
Lakinj nakumbuka kuwa Profesa Mushi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndiye alikuwa mhusika mkuu.
Katika andiko la Dira 2025 dosari hii ya ukosefu wa maoteo ya shabaha za kitakwumu kuhusu utendaji wa kisekta na kitaifa ilirekebishwa baada ya kina Profesa Luhanga kusaidia katika kuandaa mpango mkakati kiraka uitwao "Long Term Perspective Plan (LTPP)" kwa ajili ya kuweka mambo sawa kwenye kipindi cha miaka 14 kuanzia 2011 mpaka 2025. (Kiambatanisho C).
Kwa hiyo, sio sawa kusema kuwa LTPP ni andiko la kawaida linalopaswa kuandikwa sambamba na Dira ya Taifa kama Profesa Mkumbo anavyojaribu kumaanisha kwenye hotuba yake.
Andiko la LTPP lilikuwa ni "andiko kiraka" kwa ajili ya kuziba mapengo yaliyomo kwenye andiko mama kwa sababu za uzembe uliofanywa na timu ya wataalam waliopewa kazi ya kuandaa mikakati ya Taifa letu, tena kwa kulipwa fedha nyingi.
Hivyo, nilitarajia kuwa tayari tumejifunza kutokana na historia hii mbaya ya kupika na kupakua chakula kibichi kila msimu wa kuandaa mpango mkakati wa muda mrefu.
Bado naona hatujajifunza au tumejifunza lakini hatujali tunachojifunza.
XIV. Hitimisho na mapendekezo
Mpaka hapo ni wazi kwamba kikosi kazi chako Profesa Mkumbo kimeshindwa kukidhi matarajio ya Watanzania.
Nashauri kwamba dosari hizi zinarekebishika. Hivyo zirekebishwe mara moja kwa kuangalia majirani zetu wanawekaje maoteo ya shabaha za kiutendaji na vigezo vya ufanisi vya kisekta na kitaifa.
Tuachane na wazo la kuandaa kira LTPP. Tuachane na msamiati wa LTPP ambao kwetu sisi wanazuoni tuliobobea katika masuala ya mipango mikakati ni kilelezo thabiti chenye kuonyesha jinsi mwaka 2010 tulivyofeli katika suala la kupanga maendeleo yetu kupitia Tanzania Vision 2025.
Sasa rekebisha andiko la "Vision 2050" lililozinduliwa leo kwa kulichukulia kama "Vision 2050, Abridged Version."
Kisha andaa "Vision 2050, Comprehensive Version" ili kuondoa dosari nilizozionyesha, pamoja na dosari zingine mtakazozigundua.
Kuendelea kuimba wimbo wa "LTPP" kutakufanya uonekane tapeli mbele ya watu tunaojua vema sabaandikokuzaliwa kwa andiko la "LTPP" la mwaka 2011.
Kuna mifano mizuri ya maandiko ya mikakata mnayoweza kutumia.
Kuna Dira ya Papua New Guinea Kuelekea 2050, Rwanda Vision 2050, Zanzibar Vision 2050, Nigeria Agenda 2050, na Jamaica 2030.
Nyaraka zote hizi zimeambatanishwa hapa chini.
Ukweli ni kwamba, Taifa linataka andiko moja ambalo ni "self-contained" kama wanavyofanya majirani zetu wa Zanzibar, Jamaica, Rwanda, Nigeria, na kwingineko.
Tanzania tumekosa andiko la aina hii tangu miaka mingi ya nyuma. Tubadilike.
Lakini nimeshangaa. Timu uliyoizindua wewe Prof Kitila ilikuwa na wajumbe wenye uanwai wa kutosha. Baadhi walikuwa watumushi wa Benki ya Dunia. Sijui pametokea nini hadi mkatupakulia chakula ambacho hakijaiva, tena bila kachumbari wala chumvi!
XV. Viambatanisho muhimu
Kwa njia ya mfano, hebu tuangalie mtiririko wa maoteo ya kitakwimu, katika ngazi ya kisekta na kiaifa, katika dira za nchi jirani: Zanzibar, Rwanda, Jamaica, na Papua New Guinea.
A. PAPUA NEW GUINEA-LOGICAL FRAMEWORK
B. RWANDA VISION 2050--KPI MATRIX
C. JAMAICA VISION 2030--HEALTH SECTOR
D. NIGERIA VISION 2050--ICT SECTOR
E. REVISED TANZANIA VISION 2025 (LTPP 2011-2025): HUMAN CAPITAL DEVELOMENT SECTOR
Attachments
-
Kiambatanisho D--Dira ya Papua-New-Guinea 2050.pdf2.8 MB · Views: 24
-
Kiambatanisho B--Dira ya Tanzania 2025.pdf3 MB · Views: 23
-
Kiambatanisho C--Long Term Perspective Plan LTPP.pdf2.6 MB · Views: 18
-
Kiambatanisho A--DIRA YA TANZANIA 2050.pdf1.1 MB · Views: 19
-
Kiambatani E--MKUKUTA ONE.pdf20 MB · Views: 29
-
Kiambatani F--MKUKUTA TWO.pdf895.4 KB · Views: 21
-
Zanzibar 2050.pdf16.3 MB · Views: 23
-
Nigeria-Agenda-2050-Report-Corrected.pdf21.8 MB · Views: 20
-
jamaica.pdf39.9 MB · Views: 28
-
Rwanda Vision 2050 Abridged.pdf1.3 MB · Views: 20