Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Baada ya Donald Trump kuapishwa kuwa Rais wa 45 taifa kubwa la Marekani hebu tuangalie athari ya uongozi wake kwa dunia hii. Marekani kama taifa kubwa duniani kijeshi na kiuchumi ilikuwa mstari wa mbele katika harakati zote kusimamia amani na kutoa misaada ya kibinadamu kwa mataifa mbali mbali duniani. Tukianzia ndani ya Marekani enyewe kuna mgawanyiko mkubwa umetokea baada ya Donald Trump kuingia madarakani na hilo ni tishio kwa Umoja na demokrasia uliodumu kwa zaidi ya miaka 241 tokea nchi hiyo ipate uhuru, wakati wa kampeni Donald Trump alitumia lugha za kejeli,matusi na kibaguzi dhidi ya mpinzani wake na baadhi ya raia wa kimarekani kama walatino,waislam na wanawake, Donald Trump alipata upinzani mpaka ndani ya chama chake na pamoja na wengi wa majenerali waliotoa maoni yao kwamba Donald Trump hafai kuwa Rais wa Marekani na si mtu wa kumuamini katika kusimamia silaha za nyuklia za Marekani.
Toka utawala wa Rais Reagan mwaka 1989 ni mara ya kwanza kwa serikali ya Marekani kuwa na mawaziri bila kuwa na waziri mwenye asili ya kilatino, sehemu kubwa ya mawaziri wake ni wahafidhina ama lugha ingine ni wabaguzi ni hatari kwa taifa hilo kubwa lenye mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Katika sera zake za nje inaonekana bara la afrika halipo katika agenda yake kwani Donald Trump ameshafanya ziara moja tu katika bara hili na alitembelea South Africa katika shughuli zake za kibiasha tofauti na watangulizi wake Rais George Bush na Barack Obama ambao waliona bara la afrika kwa jicho la huruma na ndipo serikali zao zilifanya ushirikiano na nchi nyingi za bara hili katika masuala ya kiuchumi, kiusalama haswa kwenye vita dhidi ya ugaidi na kwenye masuala ya afya katika vita dhidi ya Ukimwi na malaria.
Donald Trump ameingia madarakani bila kuwa na uzoefu wowote wa siasa ya mambo ya nchi za nje na hiyo imewapa mashaka makubwa washirika wake haswa NATO katika masuala ya ulinzi wa ulaya ndio maana wiki za mwisho wa utawala wa Rais Barrack Obama alihakikisha Marekani wanajizatiti kijeshi katika nchi za ulaya, silaha na wanajeshi wengi wamepelekwa kwenye nchi za jumuia ya NATO. Kuhusu mashariki ya kati sasa suala la amani halipo tena tayari Donald Trump ameshaonyesha anaiunga mkono serikari ya Israel.
Leo serikali ya Israel imetupilia mbali Azimio la Umoja wa Mataifa la kuzuia ujenzi katika ardhi ya wapalestina na mpango wake wa kuhamishia ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem italeta madhara makubwa sana.Donald Trump amesema atafutilia mbali mktaba wa Marekani na Iran katika masuala ya nyuklia na amesema atarudisha vikwazo dhidi ya taifa hilo.
Kwa kumalizia kwa Donald Trump kuwa Rais wa 45 wa Marekani dunia itakuwa katika hali ya hatari sana.