The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumapili Julai 6, 2025 ametangaza kwamba ataweka ushuru wa mpya wa 10% kwa nchi zinazoambatana na sera za BRICS "za kupinga Marekani".Rais wa Marekani Donald Trump ametishia siku ya , Julai 6, 2025, kuweka ushuru mpya wa 10% kwa nchi za BRICS, kundi la nchi kumi kuu zinazoinukia kiuchumi.
"Nchi yoyote inayoambatana na sera za BRICS dhidi ya Marekani itatozwa ushuru wa ziada wa 10%. Hakutakuwa na ubaguzi kwa sera hii," Trump ameandika kwenye jukwaa la Truth Social siku ya Jumapili, bila kutoa maelezo zaidi.
Pia alitangaza kwamba barua za kwanza zinazotishia kutoza ushuru mkubwa kwa nchi zinazosita kuhitimisha makubaliano ya kibiashara na Washington zitatumwa siku ya Jumatatu saa 12 jioni saa za Ufaransa.
Siku ya Jumapili viongozi wa nchi za BRICS wamelaani mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran na kuitaka serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuondoa wanajeshi wake katika Ukanda wa Gaza, wakitaka suluhu la "haki na la kudumu" la mizozo ya Mashariki ya Kati.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa siku ya Jumapili jioni, viongozi hao waliokutana nchini Brazili walikubaliana kushutumu mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, mwanachama wa BRICS tangu Juni 13, wakati Israeli ilipoanzisha mashambulizi ambayo yalisababisha mashambulizi ya anga ya Marekani siku tisa baadaye.