KERO Dodoma: Wakazi wa Mnada Mpya, Kata ya Nkuhungu hatuna maji wiki ya 3 sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
121
Reaction score
218
Wakazi wa Mnada Mpya, Kata ya Nkuhungu – Dodoma hatuna maji wiki ya 3 sasa

Jamii Forums naomba mtusaidie kufikisha ujumbe huu kwa mamlaka zinazohusika kuhusu shida ya maji ya muda mrefu.

Sisi wakazi wa Mnada Mpya, Kata ya Nkuhungu, Mtaa wa Afisa Elimu, hatuna maji wiki ya tatu sasa na hakuna msaada kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Dodoma.

Kabla ya shida hii walituwekea utaratibu wa kuwa na zamu, maji yakawa yanatoka siku ya zamu yetu lakini hali ilivyo sasa, shida ni kubwa na hata yanapotoka yanakuwa na kasi ndogo.
 
Huku kwetu kwetu tushazoea tumelia mpaka tumesaka kivuli tumepumzika hata masika ngungi palepale
 
Si ni wabunge wote walisema mama hawamdai kasoro mpina tu?
 
Wanasema ndasat hana deni, yeye ndo anawadai mkuu.
 
MAMA HANA DENI, BALI ANAKUDAI, NENDA KAPIGE KURA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…