its MalekoGJ
Senior Member
- Aug 27, 2020
- 135
- 285
DNS ni Nini na Inafanyaje Kazi?
By MALEKOGJ
Unapofungua browser na kuandika “x.com” au “google.com”,
Laptop yako haiifahamu jina hilo kama lilivyo.
Inahitaji anwani ya IP (mfano: 142.250.190.78) ili kuifikia server ya tovuti hiyo.
Lakini kwa sababu hatuwezi kukumbuka mamilioni ya IP kama namba za simu, ndipo DNS (Domain Name System) inapokuja kutusaidia.
DNS ni kama kitabu cha simu cha mtandao.
Kazi yake kubwa: Kutafsiri majina rahisi ya tovuti kuwa anwani za IP ambazo kompyuta zinaelewa.
Mfano Halisi: Unataka Kutembelea X.com
Hebu tuone hatua kwa hatua DNS inavyofanya kazi – ukiandika “x.com” kwenye browser:
1. Unapoandika “x.com” kwenye browser yako:
Computer yako haitumii jina hilo moja kwa moja.
👉 Inatuma ombi (query) kwa DNS server ya mtoa huduma wako wa intaneti (ISP)
Swali: “Ni ipi anwani ya IP ya x.com?”
2. DNS Server ya ISP Inakagua Cache
DNS server ya mtoa huduma wako huangalia kama tayari ina kumbukumbu (cache) ya IP ya x.com.
➡Kama ina
– Inarudisha IP hiyo kwa kompyuta yako
– Browser yako inaunganika na website ya x.com
Safari inaisha hapo.
➡Kama haina
Inaendelea kuchunguza kwa niaba yako kwa kutumia mchakato unaoitwa recursive query.
3. Inatuma Ombi kwa Root DNS Server
Dunia ina 13 root DNS servers kuu
– Hizi ni servers zinazoongoza mfumo mzima wa DNS
– Hazijui IP za kila website, bali zinajua DNS za “Top Level Domains” (TLDs) kama .com, .org, .tz, nk.
Root server inasema:
4. DNS Server Inatuma Ombi kwa .com TLD Server
Inamuuliza:
TLD server inarudisha:
➡Hii hapa ni authoritative DNS server ya x.com”
5. DNS Server Inamfuata Authoritative DNS Server ya x.com
Sasa anayeulizwa ni “mwenye nyumba”.
Authoritative server anasema:
Hii server kwa kawaida huwekwa na registrar wa domain au mwenye hosting.
6. DNS Server ya ISP Inarudisha IP Hiyo kwa Kompyuta Yako
– Kompyuta yako sasa inajua kuwa x.com = 147.75.40.150
– Browser yako inaunganisha na tovuti ya x.com
– Halafu: DNS server ya ISP inaweka IP hiyo kwenye cache kwa siku zijazo ili iwe rahisi zaidi
Kwa Nini DNS Ni Muhimu Sana?
Bila DNS, tungekuwa tunakumbuka namba za IP kwa kila tovuti (kama kukariri namba 20 za simu)
Inafanya mtandao kuwa rahisi, haraka, na unaoeleweka
Inasaidia kuunganisha milioni ya websites na watumiaji duniani kwa sekunde chache
Bila DNS, hakuna Google, Facebook, X, wala WhatsApp kama tunavyovifahamu leo
Changamoto ya DNS (Na Sababu ya Kuijua)
– DNS ni mfumo muhimu sana, lakini pia ni mlango wa mashambulizi ya mtandao (DNS spoofing, hijacking)
– Watu wanaweza kubadilisha “anwani halali” na kukupeleka kwenye tovuti feki
– Kwa usalama zaidi, unashauriwa kutumia DNS za kuaminika kama Google (8.8.8.8) au Cloudflare (1.1.1.1)
DNS ni kama mkalimani kati ya wewe (mtumiaji) na ulimwengu wa mtandao.
Inawezesha mawasiliano ya binadamu na mashine kwa njia rahisi.
Kwa kuelewa mchakato huu, unakuwa si mtumiaji wa kawaida tena – unakuwa mjuzi wa msingi wa intaneti.
Unahitaji Laptop Bora Yenye Speed, Cooling Nzuri na Security ya Kutosha?
Kama umeelewa umuhimu wa DNS, usalama wa data, na performance ya kifaa chako—ni muda wa kuwa na laptop yenye kuaminika.
Tunauza laptops mpya na refurbished zenye specs kali, SSD, battery nzuri, na bei kama bure.
Pia tunayo accessories zote: chaja original, cooling pad, wireless mouse, antivirus license, na zaidi.
📞 Wasiliana Nasi Sasa:
0675 031 229 – Fontana Computers, Kariakoo
🚚 Tunafanya Delivery Tanzania Nzima
💳 Lipa kwa awamu – tunakuelewa
Kama unataka laptop ya kazi, masomo, gaming au freelance – Fontana ndiyo plug ya uhakika.

➡Inarudisha IP ya .com TLD server“Sijui IP ya x.com, lakini naijua server inayosimamia .com”
4. DNS Server Inatuma Ombi kwa .com TLD Server
Inamuuliza:
“Naomba IP ya authoritative DNS server inayosimamia x.com”
TLD server inarudisha:
➡Hii hapa ni authoritative DNS server ya x.com”
5. DNS Server Inamfuata Authoritative DNS Server ya x.com
Sasa anayeulizwa ni “mwenye nyumba”.
Authoritative server anasema:
“Sawa. IP ya x.com ni 147.75.40.150” (mfano)