KWELI Dkt. Slaa anadaiwa kusafirishwa Usiku huu (August 14, 2023) kuelekea Mbeya

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Hii ndio Taarifa ya sasa tunayokunong'oneza kutoka kwenye vyanzo vyetu vya Uhakika zinadai Kwamba Balozi Dkt. Wilbrod Slaa ambaye ni miongoni mwa Watetezi wa Bandari za Tanganyika, anasafirishwa Usiku huu kuelekea Mbeya, kwa lengo la kuunganishwa na 'wahaini' wenzake ili wafikishwe Mahakamani .

Utetezi wake wa Mali za Tanganyika umempa kesi ya Uhaini .

 
Tunachokijua
Baada ya kutokea kwa tetesi za Dkt. Slaa kusafirishwa na kuhamishiwa Mbeya JamiiForums imewasiliana na Wakili wake Dikson Matata ili kupata taarifa hii ambaye naye amesema:

Hizi tetesi zinaweza kuwa kweli kwasababu:

1. Walienda Oysterbay hawajamkuta, Mkuu wa kituo akawaambia amepelekwa Mbweni.

2. Wameenda Mbweni pia hawajamkuta.

Aidha, alipoulizwa kuhusu hatua gani itafuata baada ya kutopatikana kwa Dkt. Slaa Wakili Matata amesema:

Wakishindwa kukupa ushirikiano unaenda mahakamani kufungua maombi ya kulazimisha aletwe mahakamani na polisi (habeas corpus).

Ni maombi ambayo mahakama inalazimisha jeshi la polisi kumleta mtuhumiwa mahakamani ili awe dealt with kwa mujibu wa sheria.

Update
Leo tarehe 16/08/2023 JamiiForums imefanya mawasiliano na Wakili wa Dkt. Slaa ambaye amethibitisha kuwa mteja wake alihamishiwa Mbeya.

Wakili anasema:

Wakili wa Balozi Dkt. Wilbroad Slaa, Dickson Matata amesema mteja wake yupo mkoani Mbeya katika Kituo cha Polisi cha Kati (Central Police).

Wakili Matata amesema kuwa Dk.Slaa yupo alifikishwa mkoani Mbeya jana na upo uwezekano wa kufikishwa mahakamani leo huku akisema hajaelezwa sababu za mteja wake kupelekwa mkoani Mbeya.

Update
Dkt. Wilbroad Slaa ameachiwa kwa dhamana tarehe, 18,08, 2023 baada ya kukamatwa akituhumiwa kwa makosa yaliyoelezwa kuwa ni uhaini na uchochezi.

Taarifa za kuachiliwa kwa Dkt. Slaa zimekuja ndani ya saa 24 baada ya jopo la Mawakili wanaomtetea yeye na wenzake watatu kufungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mwendesha Mashtaka Mkuu, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Polisi Kituo Kikuu cha Mbeya Mjini kwa kuendelea kuwashikilia wateja wao kinyume na taratibu za kisheria.
Serikali ya CCM inapenda kujiabisha sana Kila wakati, aibu nyingine inawajia very soon. Hii itaongeza tu hasira dhidi ya waarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…