Dkt. Mpango simama kwenye safu yako, mwache Rais afanye kazi yake

Mheshimiwa tunakuomba usimame kwenye safu yako.

Mwache mh Suluhu afanye kazi aliyotumwa.

Usilete mfumo dume utakao mmeza Rais mama Samia akashindwa kutekeleza yampasayo.

Nimekuona na kuusikiliza wakati wa kuthibitishwa na bunge na baada ya kuapishwa.

Kuna viashiria vya kujiona ndiye Rais kamili.

Tunakufahamu vizuri sana wewe binafsi lakini kama haitoshi waha ni watu wataka kitawala na kuongoza na siyo kuongozwa.

Tabia hii ndiyo inayowapa kina Zitto, kafulila, machali na wengine.

Kwa hayati chukua yaliyo mema ambayo watu wamelalamjkia yaache kabisa
Kiongozi, nakukumbusha tu kuwa kiti cha Urais ni TAASISI
Kam hujaelewa uliza tu uelekezwe
 
Unataka Mpango ajitokeze aeleze nini kuhusu uraia wake zaidi ya kile alichokiongea Bungeni mara tu baada ya jina lake kuteuliwa kuwa Vice President.

Nikukumbushe tu, alisema alizaliwa mwaka 1957 tena kabla ya Uhuru katika kijiji cha Kasumo wilaya Kasulu na sasa wilaya mpya ya Buhigwe, na bila shaka unajua sifa za mtu kua Mtanzania. Amesomea Muyama primary.
Sasa mnataka awaeleze nini Tena!!
Tokea lini uthibitisho wa uraia wa mtu ukatolewa kwa kuongea kwa mdomo peke yake?!Una kichaa?Yaani mimi ninaweza kulalamikiwa kule Marekani kwa uraia wangu kutiliwa mashaka halafu niseme tu kwa mdomo kuwa nimezaliwa Las Vegas halafu yaishe niendelee kuishi Marekani?
 
Kwani watu mnataka Dr Mpango afanye nini? Mnapolalamika hapa mnajuaje kama hicho anachofanya sio kati ya vile alivyotumwa na kiongozi wake?

Chochote anachokifanya Dr Mpango, Waziri mkuu, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya, watendaji wa kata hadi mtaa ni kwamba wanatekeleza maagizo ya serikali ya rais wetu Samia Suluhu Hassan.

Na mafanikio yote yatahesabika kama mafanikio ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote

Nilichogundua watu wengi humu ndani kwa hoja zao sio viongozi. Na kama ni viongozi basi wanoongozwa hawana wanalofanya sababu nia aina ya wale wanaajiri mtu halafu wanarudi kufanya majuku yake
Huo ni uoga na utumwa wa viongozi wasiojiamini
 
Mama angemtuma huyo jamaa ziara ya nje ya nchi kuanzia Jumatano arudi mwezi wa nne katikati.
 
Tokea lini uthibitisho wa uraia wa mtu ukatolewa kwa kuongea kwa mdomo peke yake?!Una kichaa?Yaani mimi ninaweza kulalamikiwa kule Marekani kwa uraia wangu kutiliwa mashaka halafu niseme tu kwa mdomo kuwa nimezaliwa Las Vegas halafu yaishe niendelee kuishi Marekani?
Kumbe we ni K. Ndo kashakua Vice President sasa. Kelele za 🐸🐸 izo dhidi ya 🐊. Punguza wivu, utakufa bure.
 
Back
Top Bottom