MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 922
- 1,094
DKT.MPANGO: BAJETI HII ITAIMARISHA MSINGI KUELEKEA UCHUMI WA KATI.
WAZIRI wa Fedha, Dk Philip Mpango juzi alitangaza bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ya Sh trilioni 31.7.
Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la shilingi trilioni 2.6 za bajeti inayoishia Juni, mwaka huu. Katika bajeti hii mpya kiasi kilichotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo kimeongezeka kutoka Sh trilioni 11.8 kwa bajeti ya mwaka jana hadi kufikia Sh trilioni 11.9 kwa bajeti ya mwaka wa huu wa fedha.
Waziri alivitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa vimejikita hasa katika uimarishaji wa miundombinu ukiwamo ujenzi wa reli na kuhuisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kukamilisha ununuzi wa ndege tatu.
Hata hivyo, baadhi ya watu wameipongeza huku wengine wachache wakiikosoa kuwa haijagusa maisha ya watu moja kwa moja kupitia sekta za afya, elimu, na huduma nyingine za kijamii.
Sisi tunasema, wanaoitazama bajeti hii kwa jicho la upungufu , hawajatazama vizuri kwa kuwa kitendo cha Serikali kuweka kipaumbele katika ujenzi na uimarishaji wa miundombinu, ni kielelezo na njia sahihi kuelekea kukua kwa uchumi na huduma bora za kijamii kupatikana na kuwafikia wanyonge.
Tunasema Serikali imeona mbali kutoa kipaumbele hiki kwa sababu hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo kwa kutegemea usafirishaji wa mizigo kupitia miundombinu ya barabara, bali reli.
Sisi tunaamini kuwa, miundomnbinu ya usafirishaji ikiwa imara, bora na inayopatikana na kufikiwa kirahisi na kila mhitaji, usafirishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali utafanyika kwa urahisi, haraka na kwa gharama nafuu.
Kwa mfano, reli ikiwa imara, gharama zinazotumika kutengeneza barabara zinazoharibiwa na magari utapungua au kuisha kabisa. Gharama hizo zitaelekezwa katika huduma nyingine za kijamii.
Matumizi ya reli katika usafirishaji ni ya uhakika, kwa kiasi kikubwa na kwa gharama nafuu hivyo, kupunguza gharama ya usafirishaji bidhaa na huduma hali inayohitimishwa na gharama ndogo za huduma za kijamii. Vivyo hivyo katika ndege.
Kwa kuwa na shirika imara la ndege tunajiweka katika nafasi ya kutoa usafiri wenye kasi na uhakika kwa watu wenye uwezo na wanaotaka kasi katika shughuli zao za ujasiriamali na uwekezaji, ili waweze kuwekeza zaidi kutokana na kuwa na uwezo wa kusafiri eneo lolote la Tanzania kwa kasi wanayoitaka.
Tunasema Bajeti ya Serikali imeona mbali kwani uhakika wa usafirishaji unapokuwapo, basi uhakika wa uzalishaji wenye tija na utafutaji masoko huimarika na hivyo, kufanya upatikanaji wa bidhaa na huduma kuwa mkubwa kwa gharama nafuu.
Kimsingi, hayo na mambo mengine mengi ambayo hatujayasema hapa, ndiyo yanatufanya tuseme kuwa, hii ni bajeti iliyoona mbali kwa kuwaandalia wanyonge mazingira salama ya kuishi na ndiyo maana tunasisitiza kuwa, bajeti hii imeona mbali.
Kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba wabunge ambao ndio wanaoipitisha, kuangalia kwa makini namna ya kufanikisha bajeti hiyo na kuisaidia serikali kuweza kukusanya fedha hizo kwa ajili ya kuendelea kujenga misingi ya uchumi madhubuti tukielekea kwenye uchumi wa kati.
source habarileo